Uongo mbaya. Kwa huu mwaka huyu ndiye msanii anayeingiza pesa nyingi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Hii ni kwa tathmini yangu fupi ya harakati za hawa wanamziki kwenye mbishe zao za kungiza kipato; i) kwenye kutoa nyimbo, ii) Matamasha, iii) Endorsement., iv) Album

Kwenye list yangu mpaka sasa namba moja ni huyu Mmakonde

1. Harmonize (Mmakonde) - Ukiweka ushabiki pembeni, nimekuwa nikimfuatilia huyu dogo tangu atoke WCB. Jamaa amekuwa humble Guy, ana discpline, ana jielewa, ni hard worker wa ukweli, anajua kuusoma mchezo unavokwenda na nimegundua ameweza vema kusoma alama za nyakati.

Jamaa kwa miezi 5 iliyopita ameachia ngoma kwa speed kama alama za nyakati zinavotaka kwa wakati huu. Alama za nyakati, zinasema unatakiwa uwe kila saa masikioni mwa watu kwa ngoma nzuri au hata mbaya. Ndio siri kubwa ya mafanikio ya WCB na naona na dogo ameiga vizuri sana hii sifa. (Hapa ndo alipofeli Alikiba - amekuwa na kiburi cha kushindwa kusoma alama za nyakati)

Matamasha - hapa management yake wanajitahidi sana sana sana, wanafanya kazi mnoo (Yule Dr. Jembejembe hapa nimemkubali, kuna kitu anampa dogo, hii ndo tofauti ya kuwa na Manager Msomi na Manager wa Ramli). Yaani dogo at least kabla ya hii Corona ilikuwa kila wiki mbili anapiga tamasha. Kumbuka kila tamasha kuna mpunga flani unaingia. Nilichogundua ni kwamba dogo hajagui pesa hata kama sh. mia, na hapo sasa ndo kitu kinamfanya huyu mwamba mi niweze kusema ni mmoja wa wasanii wenye mpunga mrefu kwa sasa. (Bisha na wivu wako - ila hii ndo fact)

Angaliwa pia kwa issue ya albam aliyoachia - hiyo ni investment kwake tayari. Inaendelea kutengeneza pesa.

Angalia issue ya label yake - Kondegang. Inazidi kukuwa taratibu taratibu. Kama sahivi imeanza kumuinua huyu dogo 'Ibra'. Watu wanaweza wasiote ila ndo ndege imeshanyanyuka hivo, mwendo wa mlevi ila inapaa.

Kwenye familywise jamaa pia nampa heko, naona wapo poa sana na mke wake. Uongo mbaya mastaa wengi wa kike watakuwa kwa sasa wanamwangalia Harmonise kwa jicho la tatu kabisa. Sema hakuna anathbutu kushoboka maana jamaa yupo determined na mambo yake na mke wake. Wanamuonea wivu sana Sarah wa watu.

Ila mwisho kabisa, mi ntazidi kumpongeza sana Diamond. ame play part yake vizuri sana kumlea huyu bwana mdogo, ila inanihuzunisha kuona kwamba nyimbo za dogo hazipigwi wasafi tv, hapa ndipo Diamond anafanya makosa makubwa. Haijalishi labda anaumia dogo ametoka WCB ila anatakiwa aendelee kumpa support hata kama hayupo chini yake.

Na hili ndo tatizo la waafrika, yaani mkizinguana kimahusiano mtu anakuwekea kisasi cha milele. Mi ningemshauri Diamond, kama kuna walikoseana na dogo yeye kama kaka aliyemtoa dogo aendelee tu kumsuport, ahakikishe ngoma za dogo bado zinapigwa wasafi.. yaani Diamond anatakiwa sahiv amchukulie harmonise kama wasanii wengine na sio adui.

Maana mi naamini kabisa Harmonise bado anamuheshimu Diamond ndo mana sijawah kumsikia akimkashifu hadharani. Hii ina maana bado anakumbuka mchango wa Diamond kwenye maisha yake ya music tofauti na watu labda wanavofikiri.

Ni hayo tu kwa leo, mdogo wangu Harmonize, keep moving forward.

Wasanii wengine mjifunze kuchapa kazi sio ku-log in Instagram, mtaumbuka pabaya sana. Mjifunze kwa dogo
 
Nilitaka kuweka list hapa ila uvivu wa kuandika. Anyway

2. Diamond & WCB

Namba tatu kushuka chini sijaona kwa kweli msanii mwingine anayeingiza mkwanja kama hawa wanyama hapo juu.

Embu labda mjaribu kuongeza list na nyie wanazengo. Maana nafikiria sana hawa wasanii wengine waliobaki naona kama wanacheza makida makida
 
uzinduzi wa afro east umekula pesa ndefu bt mapokezi ya album yamebuma nakumpa hasara kubwa, pia mauzo ya nyimbo zake kwenye platform zote yameshuka sana, now kinachombemba harmo ni hizo balozi alizobahatika kupata ndo zinazijazia hizo hasara vinginevyo angekua na wakati mgum zaidi kuliko ulivomsifia hapa.
 
Watu wanaangalia mapato tu hawaangalii matumizi, halafu show karibu zote alizozifanya Harmonize baada ya kutoka WCB ni za bila kiingilo (bure) so sitegemei malipo makubwa kwenye hizo show hata kama alikuwa na wadhamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiasi fulani harmonize ameshuka kiperfomance tofauti na alivyokua wcb
Nadhani unaweka siasa na ushabiki,unasemaje kashuka wakati dogo kabla ya corona ni show kila siku duniani huko,huyu jembe ni jembe ni meneja bora sana,harmonize anapiga show nyingi sana nje ya nchi kuliko ata diamond(ambazo zinamuingizia pesa ndefu pia).Kiasi kwamba kama angebak wcb show zote hizo baadhi ziingeeda kwa bosi wao km kawaida yake

Nyanja ya utajiri hiyo haina ubishi,ata kw macho tu unaona bila ata kuuliza bank account zake,ambalo ili ni funzo kwa Rayvanny inabidi achanganye akili yake sasa na muda ndo huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Show gani nzito harmonize amefanya, tangu atoke WCB???, The last bumping show Kwa harmonize ni Ile ya south Sudan na alikuwa Wasafi , hzi za mikoani hamna kitu , za EFM sjui fiesta chenga tupu , au unasemea Ile ya Burundi ??, ukweli ni kwamba Harmonize na meneja wake wameloose lot of 💰 hawana hamu , target yao ilikuwa-kumbrand konde ili aburst kwenye show outside the country, Corona imewaharibia kila kitu , dili lililomfanya Kondeboy apumue ni lile la CRDB tuu , nguvu kubwa imetumika afro East lakn ameangukia pua vibaya sana, ametumia nguvu nying but with in short of time yupo out of trending ....Harmonize alikuwa juu ya Rayvanny kwenye social platforms but now Rayvanny yupo juu ya Kondeboy , even All kiba now chasing the boy, ila nampa credit condeboy Kwa kufight back

 
Konde boy anajitahidi kwa kiasi fulani lakini sio kama ulivyoandika hapa

Na wewe utakua ni shabiki wa kiba tu ,mnatumia nguvu kuipinga wcb pamoja na diamond

Muda mwingine lazima muelewe tu kwamba alietangulia katangulia tu
 
we ndio unaleta ushabiki mavi hapa..

Kabla ya Corona Diamond alikuwa anapiga show ulaya, Europe Tour ... Nchi karibia zote ulaya at the same time Jembe ni Jembe na Harmonize walikuwa wanapiga show ya sayona Twist mbagala...

Sada usitake utufanye watu hatuelewi huu muziki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Show alizopiga harmonize ni show
Ile aliyofungia mwaka huko kwao
Fiesta
twist juice na moja ya One Africa ambayo aliipata akiwa chini ya WCB labda na moja ya uganda
alipata show kenya haikufanyika
wakati huo mond alikuwa akifanya show zake huko duniani
ukiachana na swala la show usitake niambia mmakonde keshaanza kula matunda ya lebo yake.
Tukiludi YouTube hauwezi ukamlinganisha na Mond hata nusu haingii
kwenye mauzo ya Albam hana tofauti na African boy ya Jux tofauti ni kwamba alitumia gharama ndefu katika kuizindua ukiifananisha na ya Jux
ko kwa fact zako ushatudanganya hawezi kuwa zaidi ya Diamond
Labda anaweza akawa analingana na Nandy ila sio zaidi ya Mond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…