Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Hii ni kwa tathmini yangu fupi ya harakati za hawa wanamziki kwenye mbishe zao za kungiza kipato; i) kwenye kutoa nyimbo, ii) Matamasha, iii) Endorsement., iv) Album
Kwenye list yangu mpaka sasa namba moja ni huyu Mmakonde
1. Harmonize (Mmakonde) - Ukiweka ushabiki pembeni, nimekuwa nikimfuatilia huyu dogo tangu atoke WCB. Jamaa amekuwa humble Guy, ana discpline, ana jielewa, ni hard worker wa ukweli, anajua kuusoma mchezo unavokwenda na nimegundua ameweza vema kusoma alama za nyakati.
Jamaa kwa miezi 5 iliyopita ameachia ngoma kwa speed kama alama za nyakati zinavotaka kwa wakati huu. Alama za nyakati, zinasema unatakiwa uwe kila saa masikioni mwa watu kwa ngoma nzuri au hata mbaya. Ndio siri kubwa ya mafanikio ya WCB na naona na dogo ameiga vizuri sana hii sifa. (Hapa ndo alipofeli Alikiba - amekuwa na kiburi cha kushindwa kusoma alama za nyakati)
Matamasha - hapa management yake wanajitahidi sana sana sana, wanafanya kazi mnoo (Yule Dr. Jembejembe hapa nimemkubali, kuna kitu anampa dogo, hii ndo tofauti ya kuwa na Manager Msomi na Manager wa Ramli). Yaani dogo at least kabla ya hii Corona ilikuwa kila wiki mbili anapiga tamasha. Kumbuka kila tamasha kuna mpunga flani unaingia. Nilichogundua ni kwamba dogo hajagui pesa hata kama sh. mia, na hapo sasa ndo kitu kinamfanya huyu mwamba mi niweze kusema ni mmoja wa wasanii wenye mpunga mrefu kwa sasa. (Bisha na wivu wako - ila hii ndo fact)
Angaliwa pia kwa issue ya albam aliyoachia - hiyo ni investment kwake tayari. Inaendelea kutengeneza pesa.
Angalia issue ya label yake - Kondegang. Inazidi kukuwa taratibu taratibu. Kama sahivi imeanza kumuinua huyu dogo 'Ibra'. Watu wanaweza wasiote ila ndo ndege imeshanyanyuka hivo, mwendo wa mlevi ila inapaa.
Kwenye familywise jamaa pia nampa heko, naona wapo poa sana na mke wake. Uongo mbaya mastaa wengi wa kike watakuwa kwa sasa wanamwangalia Harmonise kwa jicho la tatu kabisa. Sema hakuna anathbutu kushoboka maana jamaa yupo determined na mambo yake na mke wake. Wanamuonea wivu sana Sarah wa watu.
Ila mwisho kabisa, mi ntazidi kumpongeza sana Diamond. ame play part yake vizuri sana kumlea huyu bwana mdogo, ila inanihuzunisha kuona kwamba nyimbo za dogo hazipigwi wasafi tv, hapa ndipo Diamond anafanya makosa makubwa. Haijalishi labda anaumia dogo ametoka WCB ila anatakiwa aendelee kumpa support hata kama hayupo chini yake.
Na hili ndo tatizo la waafrika, yaani mkizinguana kimahusiano mtu anakuwekea kisasi cha milele. Mi ningemshauri Diamond, kama kuna walikoseana na dogo yeye kama kaka aliyemtoa dogo aendelee tu kumsuport, ahakikishe ngoma za dogo bado zinapigwa wasafi.. yaani Diamond anatakiwa sahiv amchukulie harmonise kama wasanii wengine na sio adui.
Maana mi naamini kabisa Harmonise bado anamuheshimu Diamond ndo mana sijawah kumsikia akimkashifu hadharani. Hii ina maana bado anakumbuka mchango wa Diamond kwenye maisha yake ya music tofauti na watu labda wanavofikiri.
Ni hayo tu kwa leo, mdogo wangu Harmonize, keep moving forward.
Wasanii wengine mjifunze kuchapa kazi sio ku-log in Instagram, mtaumbuka pabaya sana. Mjifunze kwa dogo