Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Adam alitumia kitabu/mwongozo upi mana umesema nae alikuwa islam

Sio kila mitume au manabii au wanadamu walipewa vitabu.

Adamu alikuwa anapewa maelezo ya Moja kwa moja toka kwa Allah. Kitendo Cha kujisalimisha kwake kwa kumtii pasi na kumshirikisha na chochote huo huitwa "UISLAMU".
 
Mtoto asingekufa adhabu ingekua haijafanyika kabisa.
Baadhi ya adhabu zinaweza kuonya na kukemea. Hivyo nia yake ni njema, kukemea na kuonya ili kosa lisijirudie.

Nia ya kumuadhibu kwa kifo ni njema? Kuna jema gani kwenye hiyo adhabu?

Tusitoke kwanye mada.
Nilitaka kujua tu kile kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kama adhabu ni kitendo cha upendo?
Elewa neno kitendo. Ni hilo tu. Huko kwingine tuachane nako.
 
Sasa kwanini unajadili katika namna ya ujuaji na hujui ?

Maana haukupaswa kujadili mjadala huu.
Mjadala ni dini...na najua dini ni za uwongo na hata siendi mbali nasoma bible na Quran tu najua ni uwongo. Hata bila kuhangaika Sana... it's so easy to disprove religion
 
Hili swali la uongo. Uliza swali sahihi, ushaambiwa hakuna kinachozidi uwepo wake, wewe unakuja kuuliza hawezi kuumba kinacho mzidi ? Unaakilo kweli kijana ?

Au huwa unafurahi kuleta utoto katika mada za wakubwa na za kielimu ?
🤣Si ndo hawezi asa...mbona unakimbia
 
Sio kila mitume au manabii au wanadamu walipewa vitabu.

Adamu alikuwa anapewa maelezo ya Moja kwa moja toka kwa Allah. Kitendo Cha kujisalimisha kwake kwa kumtii pasi na kumshirikisha na chochote huo huitwa "UISLAMU".
Basi mi namtii Buddha
 
Mara ngapi watu wanakusudia kuua na mtu hafi ? Na unaweza kuadhibu na mtu aside kama ulivyo kusudia ? Kwanini unaleta ubishi wa kitoto ?

Jema katika hiyo adhabu ni kuondoa uovu, na kuukemea ila njia aliyo itumia haikuwa sahihi.

Unataka nikujibu mara ngapi kuhusu hicho kitendo ? Hivi unasoma ninacho kiandika au unabishana uonekana upo kwenye mjadala ?

Kwani hapa naongelea sifa au jina ? Bila shaka naongelea kitendo, Sasa kwanini unapoteza kwenye hakuna ?
 
Mjadala ni dini...na najua dini ni za uwongo na hata siendi mbali nasoma bible na Quran tu najua ni uwongo. Hata bila kuhangaika Sana... it's so easy to disprove religion
Leta huo uongo tuuone hasa katika Qur'an.
 
Sio kila mitume au manabii au wanadamu walipewa vitabu.

Adamu alikuwa anapewa maelezo ya Moja kwa moja toka kwa Allah. Kitendo Cha kujisalimisha kwake kwa kumtii pasi na kumshirikisha na chochote huo huitwa "UISLAMU"

Leta huo uongo tuuone hasa katika Qur'an.
Tushasema Mara kibao . Ila unaishia kujikosha tu..so tumechoka.
 
🤣Si ndo hawezi asa...mbona unakimbia
Hawezi vipi ? Unajua maana ya swali la uongo ? Ushaambiwa hakuna kinachozidi uwezo wake, wewe unakuja kuuliza je anaweza kuumba kitu kinachozidi uwezo wake ? Hii akili au wendawazimu ?

Maana yake wewe unae uliza swali hili huna akili.
 
Tushasema Mara kibao . Ila unaishia kujikosha tu..so tumechoka.
Weka nukta Moja baada ya nyingine, na uhakikishe unacho kiweka unalijua, maana nyinyi mnashida ya kuokoteza vitu mitandaoni pasi na kuvifanyia uhakiki, mkivileta humu mkibanwanakimbia.

Wewe, weka nukta Moja baada ya nyingine tuijadili.
 
Katika mjadala wenye maelewano, kuna mwendelezo wa mjadala,

Ili tutoke hapa nmekuuliza swali ili tuuelewe mfano,

Kwasababu hujui chochote umerudi hapa hapa,

Umerudia tu kusema kwamba mfano hauendani.

Ila nlikuuliza kwamba unaelewa hata mfano nliokupa ulikuwa unalenga kujadili nini/dhana ipi?

Weww kama ni mwerevu Jibu hili tutoke hapa.
Kwanza umeshaelewa kuwa jua ni nyota?
 
Kitu gani ambacho sikijui nje ya Qur'aan nimekipinga ?

Mimi kitu ambacho sikijui huwa nakiri ya kuwa sikijui, sababu sishindani na mtu.

Onyesha kitu hicho ambacho sikijui nje ya Qur'an, katika mjadala huu ?
Hujui kuwa jua ni nyota!!
 
Na Mimi nikakujibu ya kuwa ili uone kama sijakuelewa kosoa ule ukosoaji wangu juu ya mfano wako.

Katika mjadala unatakiwa uweke wazi mambo kama navyo fanya Mimi, ukitoa mfano wa filimbi, hakuna ambaye haijui filimbi umbile lake, sifa zake na kazi zake, ukaja kutokea mfano ule ukaulinganisha na suala la Mungu. Mfano ambao haukai katika suala hili, kwa wewe kukanusha kutokuwepo kwa Mungu wakati humjui na hajawahi kutokuwepo.

Sasa unaposema ya kwamba huenda sijaelewa mfano wako, ulitakiwa ukosoe nilicho kiandika katika ule mfano wako.

Suala la jua hili ni jambo lingine na Kuna maswali nimekuuliza kuhusu kuhusu nusu vipenyo vya jua. Jua kuitwa nyota ni kwa mujibu wenu nyinyi Wanasayansi na hizi ni dhana tu sababu nyota zinajulikana na kazi kadhalika, ndio maana ili kukuonyesha ya kuwa nyinyi mnasema Jua ni nyota ni kulipia jina la "Big Star" ukaja na ngano za wanasayansi ya kuwa Kuna nyota kubwa kuzidi Jua, ukaleta tena ngano za nusu vipenyo, nikakuuliza maswali kuhusu nusu vipenyo naona unaruka ruka tu.
 
Hii Dunia bhana inampa taabu sana mwanadamu hususani ya yeye ni nani?, kwann anaishi humu panapoitwa duniani na hatima yake ni nini?, Hii so called Dunia inamambo mengi sana ikitaka kujua angalia toka mwanadamu wa kale mpaka Sasa yako mambo mengi yamevumbuliwa ambayo yanaonekana kuusaidia mwili wa mwanadamu katika shughuli zake za kila siku lakini bado mamboya msingi yanabaki hayana majibu, ukumbuke ulikuja duniani si kwa maamuzi yako basi hivyohivyo uwepo wako au Dunia hii sii maamuzi yako, utateseka na mambo mbalimbali si kwa sababu umependa ila yapo na yataendelea kuwepo, utakufa si kwa sababu umependa ila yaliyomo humu ndio yatapelekea wewe kufa.
Sasa basi uwepo/kutokuwepo kwa Mungu hakukufanyi wewe kuigeuza Dunia bali itabaki vilevile, kukashifu haikusaidii kitu kila kilichopo humu kinasababu zake ambazo wewe/Mimi hatuna maamuzi nazo kama zilivyo study mbalimbali na kuongeza maarifa na ufahamu vilevile Imani ya rohoni humasidia muhusika katika kutafuta na kujua mambo mbalimbali nje ya haya, technolojia nyingi tunazotumia waafrika zimetokana na ngozi nyeupe sisi huku ni watumiaji tu, usiishie kupiga kelele nenda kwa juhudi na maarifa na Imani ya kweli utakuja hapa na majibu hakuna kitu cha bahati mbaya/nzuri hap dunianikila kitu kipo kwa sababu yake na hakuna utakacho leta hapa toka nje ya boksi lililopo kwa kuwa hakitakuwa cha mazingira haya.
Kazi kwako mleta mada.
 
Hili swali lingine Sasa, usiseme kwamba swali hili sijajibu.

Nakujibu Sasa swali hili, siwezi kumuua sababu kuua adhabu ya moto ni kwa Allah tu na mwanadamu harusiwi kutumia moto kuadhibu.
Kisai, hilo swali nimeuliza post #1595. Hapo nimelirudia kwa mara ya pili. Either hausomi kwa makini au ni muongo kupindukia.

Nilikuuliza awali kama kitendo hicho ni cha huruma. Ukasema ndio, ni cha huruma. Rejea post yako mwenyewe #1505

Nikauliza;
Wewe unaweza kumuua mtoto wako kwa kumchoma moto mpaka afe pale anapokosea kwa kumhurumia??
Unajibu;
"Siwezi kumuua kwa sababu adhabu ya kuua ni ya Allah tu na mwanadamu hatakiwi kutumia moto kuadhibu" wakati ulisha sema mwanzo kwamba kumuua mtoto kwa moto ni kitendo cha huruma.

Post yako mwenyewe #1505

Je, Allah hataki watu wawe na huruma?
 
Sawa.
Vipi mtoto wako kipenzi akiuliwa na jirani yako kwa kuchomwa moto kama adhabu.
Je kitendo hicho kitakua cha furaha kwako? Kisai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…