Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Kwa nini ni hadithi za kusadikika?

Havina ushahidi wa uwepo wake

Na hadithi hizo hazina uhalisia haziendani wala kuleta MANTIKI

Unaambiwa shetani anatufanya tufanye dhambi...... anatufanya kwa vipi haswa? Wewe amewahi kukuhadaa? How?
Yaani napiga tungi kwa hiyari yangu hapo shetani anaingiaje? Mbona sijawahi kumuona au kumuhisi tu akiniambia kamata demu ukazagamue?

Roho ndio lidubwana gani linathibitikaje kuwa lipo?
 
Umepunguza hasira yangu dhidi ya uyu jamaa!

Yuko Blank kabisa!

Nitamjibu kwa kumsaidia baadaye!

Ila umempa kitu cha maana sana!

Kwamba Uchawi ndiyo lakini Mungu hayuko...Bogus a hundred times!!!
Umefatilia Uzi tokea mwanzo ama umebagua tu vya kusoma!
 
Haya yote unayoyasema na unayoyafikiria na unatamani yawe kama wewe unavyotaka hizo zote ni sifa ambazo binadamu ameumbwa nazo

Yani kama usingekuwa na hivyo vitu akili mwako basi wewe usingekuwa binadamu ungekuwa ni kiumbe mwingine labda Ndege au Mbuzi hiyo inaitwa nafsi/matamanio ni viumbe wawili tu wamepewa binadamu na majini na ndio maana wamewekewa moto na pepo chaguo ni lao wapi wanataka waende

Malaika hawana nafsi/ matamanio na ndio maana wao wanaishi peponi na wataishi huko milele

Malaika anafanya Yale tu aliyoamlishwa na Mungu afanye asiyoamlishwa na Mungu hafanyi

Ila binadamu amepewa option

Kumbukumbu la Torati 11:26
Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;

Kumbukumbu la Torati 11:27
baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo leo;

Kumbukumbu la Torati 11:28
na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Hapo umesema malaika hawana nafsi je ni viumbe? Na je Wana mwili?
 
Mbingu Haipo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

If you fail to live on Earth, Heaven is an illusion.
Kwani mbinguni ni nini? Halafu kuishi kwa nini kuna mpaka. Yaani Kwa nini viumbe haviishi milele badala yake vikifika umri fulani hufa?

Mduara wa maisha (life circle) unajisimamia ama unasimamiwa na nani?
 
Chukua kamba funga shingon yaani tia kitanzi halafu ita watu wawili wawe karibu na kisu kikali kwelkwel na kamera ya kurekodi, jitundike wategue kigoda cha kusimamia, wahesabu mpaka 10 kama zilivyo amri alizopewa Musa milimani..then wakate kamba udondoke..kaa nusu saa akili ikae sawa, fanya review ya video...usipokuta mahali umemtaja Mungu aliekuumba basi uje utoe ushuhuda hapa hakuna Mungu.[emoji23][emoji23][emoji23]
Lazima atajwe si ndio malezi tuliokuwa nayo. Neno mama linatajwa zaidi kuliko Mungu, ama utabisha
 
Kwani kutokuwepo kwa Mungu kuna maana mimi ndio niwe na hizo nguvu?
Ulivyo sema baada ya kuona watoto wanaumia namna ile.. na wewe ulisema uliumia sana.... Ukajiuliza huyu Mungu vipi huyu?... KWa maana hiyo.. una jawabu la tatizo la hao watoto.... Au uliumia tu na ukakosa la kufanya na KWa kwakuwa ukweli usiopingika ya kwamba huna la kufanya?
 
Nimesoma maoni yako vzr rafiki yangu ...lakini kumbuka mambo mabaya yanayotupata msabibishi si mungu ...

Mungu anapenda watu wamwabudu kwa hiari yaani kwa kupenda ,alikuwa na uwezo kutuumba tuwe ka roboti ili kwamba tufanye atakacho yeye lakini yeye ametupa uhuru wa kuchagua tumtii au tusimtii

Pia mungu hakumuumba shetani ,aliumba malaika wakamilifu huko mbinguni ila malaika mmoja alitumia uhuru wake vibaya ,kwakutamani kuabudiwa awe ka mungu ndo huyo malaika mwovu anaitwa Shetani

Na matokeo yake huyo shetani alipinga enzi ya mungu kutawala akamwasi Mungu.Akaja duniani akanzisha uasi kwa wanadamu wasitii maagizo ya mungu.

Kumbuka pia mungu alimwambia mwanadamu matokeo yangekuwa nini ikiwa angekosa kutii maagizo hayo

Kwa hiyo Mungu ameacha muda upite kuthibitisha ikiwa wanadamu bila mungu wanaweza kujitegemea wenyewe? Mungu sio mtawala wa ulimwengu huu anayeoongoza ni shetani

Hivyo mambo yoote mabaya tunayopata sasa ni matokeo ya utawala wa shetani ..suluhisho ya matatizo haya ni kusubiri utawala wa mungu uje tena unaoitwa Ufame wa mungu ..


Kwa maongezi zaidi 0624009037/0717382740
Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya?

Unataka kusema Mungu angeshindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekni!?

Je Mungu hakujua kama kutatokea uasi!?
 
Ni hadithi za kusadikika kwa sababu Hazipo kwa namna yoyote ile,

Hazionekani, Hazishikiki, Hazisikiki, Hazihisiki.
Kuonekana kukoje. Kama kuonekana ni kizingiti kwa upeo wa macho kwa kweli Mungu haonekani.

Lakini kama Mungu kuonekana kwake kunatokana na fikira ya binadamu kuhusu maumbile ya ulimwengu na jinsi ulimwengu unavyotenda kazi, basi Mungu anaonekana.

Kwa nini umewaza kuwa Ili Mungu awepo ni lazima awe anashikika? Kwa ivo Kwa kuwa Mungu hashikiki basi ndiyo kwamba hayupo.

Unataka kuiona Mbingu Ili ufanyaje wakati unaambiwa kuwa Mbingu ni suala la kiroho??
 
Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya?

Unataka kusema Mungu angeshindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekni!?

Je Mungu hakujua kama kutatokea uasi!?
Wewe unataka ulimwengu usio na mabaya uumbwe na Mungu usiyeamini kuwepo kwake??

Kama huamini kuwa kuna Mungu basi amini pia kuwa hakuna shetani. Na kama hakuna Mungu Wala shetani basi hakuna uwezo wa kupima mema ama mabaya.

Maana jambo linakuwa jema ama baya kwa kigezo gani? Mtu akizini, akiiba, akisema uongo, akiua au akisingizia mtu, haliwezi kuwa jambo jema ama baya Kwa kuwa hakuna chanzo cha kuonesha jambo husika kama ni jema ama baya

Kama huamini kuwa kuna Mungu, basi usiuchukie ushoga!!!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] bas Kama ni mmoja wote tungekuwa na Imani sawa...,[emoji1787]so roho yangu ndo imeumba ulimwengu...hii analogy mbona inaanza kuvunjika yenyewe umedanganywa na mchungaji gani
Wewe unahisi kile Mungu alipulizia kwenye udongo aliofinyanga kumuumba Adam ktk maandiko ilikua ni pumzi ya uzima kutoka respiratory za nani?
 
Kuonekana kukoje. Kama kuonekana ni kizingiti kwa upeo wa macho kwa kweli Mungu haonekani.

Lakini kama Mungu kuonekana kwake kunatokana na fikira ya binadamu kuhusu maumbile ya ulimwengu na jinsi ulimwengu unavyotenda kazi, basi Mungu anaonekana.

Kwa nini umewaza kuwa Ili Mungu awepo ni lazima awe anashikika? Kwa ivo Kwa kuwa Mungu hashikiki basi ndiyo kwamba hayupo.

Unataka kuiona Mbingu Ili ufanyaje wakati unaambiwa kuwa Mbingu ni suala la kiroho??
Ndio maana nakwambia hivi 👇

Mungu huyo, Hayupo katika uhalisia ila katika mawazo ya kufikirika tu.

Mungu ni dhana ya kufikirika, Imagination just an illusion.

Hayupo kwenye uhalisia.
 
Kwani mbinguni ni nini? Halafu kuishi kwa nini kuna mpaka. Yaani Kwa nini viumbe haviishi milele badala yake vikifika umri fulani hufa?

Mduara wa maisha (life circle) unajisimamia ama unasimamiwa na nani?
Mbingu ni dhana ya kufikirika ambapo watu hudhani kwamba baada ya kufa watakwenda huko.

Viumbe lazima vife ili vingine vipate nafasi ya kuishi.

Fikiria kwamba, Kungekuwa hamna Kifo Population ya watu, wanyama na viumbe wengine duniani leo hii ingekuwa kiasi gani?

Vuta picha kwanza hilo nyomi la watu lingekuwa kiasi gani?😄

Si kungekuwa hakuna hata nafasi ya kupita, Yaani tungekuwa tumebanana sana.

Yani tungekuwa billions of billions ya watu na wanyama.

Sasa unategemea hapo tunge ishije?

Watu na wanyama lazima wafe, ili viumbe wengine wapate nafasi ya kuishi.

Babu yako mzaa babu yako wa babu yako asinge kufa, Leo hii wewe ungeweza hata kumiliki ardhi hapo nyumbani kwenu?

Usinge pata hata hiyo nafasi.

Kifo ni muhimu ili nature iende na uwiano wa viumbe hai wote.
 
Swali lako la uongo. Kwa mujibu wa Imani yangu Mola pekee ndio anaadhibu kwa kuchoma na hayo kwa kuchoma. Kingine Mola wangu Hana mtoto Wala watoto, kama unamkusudia Mola.

Kama unamaanisha mwanadamu, kwa Imani yangu mwanadamu haruhusiwi kuwa kwa kuchoma moto. Kwahiyo kwangu Mimi siwezi kuua mwanangu au kuadhibu kwa kuchoma moto, sababu ni haramu jambo hili.
Je, kitendo cha kumchoma moto mtoto wako kama adhabu kitatafsiriwa na jamii kama cha upendo?
Ndugu na jamaa zako watakuona kama baba mwenye upendo au vinginevyo?

Vipi jirani yako angefanya kitendo kama hicho. Je, utaamini ukiambiwa jirani huyo alikua ni mtu mwenye upendo sana kwa mtoto wake??
 
Dunia hii imepitia uongo/utapeli/propaganda kubwa sana na zikapita lakini uongo pekee ulio dumu kwa muda mrefu ni huu

Hebu fikiri unaambiwa kuna MUNGU muweza wa yote yupo sahihi na hajawahi kukosea

Ameumba dunia kwaajili yetu na ataiangamiza dunia kwaajili yetu
Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza,
Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na UWEZO wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie Pepo tu tukale bata

Anajua tunacho hitaji lakini lazima tumuombe ili atupe, lakini hata tukimuomba hatupi tunavyo taka sisi maana tayari amekwisha tupangia kila mtu atampa nini, ataishije na atakufaje

Ndio muumba wa kila kitu(magonjwa, bangi, majini, ulabu nk) na anaweza kudhibiti chochote lakini anamlaumu msaidizi wake muasi(Shetani) kuleta mambo hayo mabaya duniani(magonjwa nk) kwa watu wake aliyewaumba wakati yeye ndiye aliye mtupa msaidizi wake huyo huku duniani
Yaani yeye kashindwana naye huko mbinguni kaja kumtupa kwetu sisi viumbe dhaifu tupambane naye na tukishindwa tutachomwa moto milele, lakini anasisitiza anatupenda sana kama mtu anavyopenda na kujali mboni ya jicho lake

Hebu tafakari hili, kawaumba Adam na Hawa na wakati bado wageni duniani akawatupia Nyoka(Shetani) ili awarubuni, na kwa ugeni wao wakarubunika matokeo yake katupa adhabu ya shuruba watu wote hata ambao tulikua hatupo na hata ambao hawajazaliwa chamoto watakiona...... Not fair

Mungu muweza wa yote hayupo WAZI PASI NA SHAKA kwa watu wote kujua huyu ndio MUNGU badala yake Mungu ndio amekua sehemu kubwa ya mgawanyiko wa watu na kusababisha kuwa na imani za MIUNGU zaidi ya milioni dunia nzima
Na kibaya zaidi unatakiwa to blindly believe him, usihoji wala kuwa na shaka juu ya uwepo wake(ni laana na kufuru) vinginevyo moto wa milele unakuhusu

Yaani kuna Fundi Kapenta mmoja huko Galilaya eti kafa kwaajili ya dhambi za watu wote duniani.... seriously [emoji15]?
Akaitwa Mungu lakini Mungu huyu akajaribiwa na shetani[emoji15]
Fundi kampenta huyu hakuandika kitabu chochote ila wahuni walio kuwa wanampinga ndio wakaja kuandika vitabu kuhusu fundi huyu na vinaitwa “Bibilia Neno la Mungu takatifu”
Mabilioni ya watu dunia kote wanakesha makanisani wakimlilia na kumuomba awape uponyaji, mali, waume/wake nk

Hebu fikiria huko Arabia kuna Maamuma mmoja hajui kusoma wala kuandika alidai anashushiwa maagizo na Mungu kukata vichwa watu wote watakao pinga na kutokutii maagizo yake, “akashushiwa” aya za vitisho na neema kwa watakao tii, yaani ukifa unampigania Mungu unakwenda kupewa mbikra 72 kazi yako ni kuzagamua tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Mabilioni ya watu duniani wanasujudu mara 5 kwa siku na kushinda njaa mwezi kila mwaka ili wakale naye bata Peponi

Kwamba maisha yako hapa duniani ni ya mpito tu maisha yako yapo baada ya kufa
Unachotakiwa kufanya ni kumuamini na kufanya aliyoa agiza ili ukale bata sana baada ya kufa

This is the biggest scam ever
Ni Watu wajinga tu wasioamini uwepo wa Mungu na mwanaye yesu kristo
 
Back
Top Bottom