Mwandishi katoa mawazo tena mazuri tu. Sioni kwa nini umwambie kavuta bangi. Hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha uwepo wa Mungu. Siri kubwa ya dini ni IMANI. Wafuasi wote wanafuata bila kuhoji wala kudai uthibitisho. Na hii ni kwa dini au IMANI zote. Iwe dini ya Kikristu, Kiislamu, Kihindu, au ile ya Kikabila kila kitu chake kimejikita kwenye siri. Yaani kukubali bila kuwa na uhakika au uthibitisho. Mara nyingi utaona waumini hulazimishwa kwa vitisho, hasa wakiogopa kwenda motoni (dini za kigeni) au kulipwa kwa adhabu na mateso makali (dini za kienyeji) hapahapa duniani. Mimi sina hakikaki na ukweli, maana sina vikokotoo vya kunisadia kuona kama dini hizi ni za kweli au siyo. Hakuna vikokotoo vya kutosha kuthibitisha kama Mungu yupo au hayupo. Hapa duniani tunasukumwa tu na uoga.