Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Watu wanataka Mungu awe kama wanavyotaka wao aweje

Jibidiishe sana kumtamfuta Mungu badala ya kutoa kufuru kwamba hayupo
 
Dunia hii imepitia uongo/utapeli/propaganda kubwa sana na zikapita lakini uongo pekee ulio dumu kwa muda mrefu ni huu

Hebu fikiri unaambiwa kuna MUNGU muweza wa yote yupo sahihi na hajawahi kukosea

Ameumba dunia kwaajili yetu na ataiangamiza dunia kwaajili yetu
Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza,
Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na UWEZO wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie Pepo tu tukale bata

Anajua tunacho hitaji lakini lazima tumuombe ili atupe, lakini hata tukimuomba hatupi tunavyo taka sisi maana tayari amekwisha tupangia kila mtu atampa nini, ataishije na atakufaje

Ndio muumba wa kila kitu(magonjwa, bangi, majini, ulabu nk) na anaweza kudhibiti chochote lakini anamlaumu msaidizi wake muasi(Shetani) kuleta mambo hayo mabaya duniani(magonjwa nk) kwa watu wake aliyewaumba wakati yeye ndiye aliye mtupa msaidizi wake huyo huku duniani
Yaani yeye kashindwana naye huko mbinguni kaja kumtupa kwetu sisi viumbe dhaifu tupambane naye na tukishindwa tutachomwa moto milele, lakini anasisitiza anatupenda sana kama mtu anavyopenda na kujali mboni ya jicho lake

Hebu tafakari hili, kawaumba Adam na Hawa na wakati bado wageni duniani akawatupia Nyoka(Shetani) ili awarubuni, na kwa ugeni wao wakarubunika matokeo yake katupa adhabu ya shuruba watu wote hata ambao tulikua hatupo na hata ambao hawajazaliwa chamoto watakiona...... Not fair

Mungu muweza wa yote hayupo WAZI PASI NA SHAKA kwa watu wote kujua huyu ndio MUNGU badala yake Mungu ndio amekua sehemu kubwa ya mgawanyiko wa watu na kusababisha kuwa na imani za MIUNGU zaidi ya milioni dunia nzima
Na kibaya zaidi unatakiwa to blindly believe him, usihoji wala kuwa na shaka juu ya uwepo wake(ni laana na kufuru) vinginevyo moto wa milele unakuhusu

Yaani kuna Fundi Kapenta mmoja huko Galilaya eti kafa kwaajili ya dhambi za watu wote duniani.... seriously [emoji15]?
Akaitwa Mungu lakini Mungu huyu akajaribiwa na shetani[emoji15]
Fundi kampenta huyu hakuandika kitabu chochote ila wahuni walio kuwa wanampinga ndio wakaja kuandika vitabu kuhusu fundi huyu na vinaitwa “Bibilia Neno la Mungu takatifu”
Mabilioni ya watu dunia kote wanakesha makanisani wakimlilia na kumuomba awape uponyaji, mali, waume/wake nk

Hebu fikiria huko Arabia kuna Maamuma mmoja hajui kusoma wala kuandika alidai anashushiwa maagizo na Mungu kukata vichwa watu wote watakao pinga na kutokutii maagizo yake, “akashushiwa” aya za vitisho na neema kwa watakao tii, yaani ukifa unampigania Mungu unakwenda kupewa mbikra 72 kazi yako ni kuzagamua tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Mabilioni ya watu duniani wanasujudu mara 5 kwa siku na kushinda njaa mwezi kila mwaka ili wakale naye bata Peponi

Kwamba maisha yako hapa duniani ni ya mpito tu maisha yako yapo baada ya kufa
Unachotakiwa kufanya ni kumuamini na kufanya aliyoa agiza ili ukale bata sana baada ya kufa

This is the biggest scam ever
Mpumbavu Namba moja duniani naweza kusema pacha wa firauni wewe. Wewe mtoa post ni firauni wa pili, mwenzio aliomba poo kwasbb aliletewa mtu wa kumuonya na akakana. Wewe ujumbe umeukuta na shuhuda za waliopita umezisikia na zipo vitabuni ila unajitia ubazazi dawa yko iko jikoni.
 
Wewe umemfanyia nini Mungu aliyekuumba, akakujaalia uhai, chakula, malazi, afya, pumzi and all you have!??? Zaidi ya kukufuru tu na kukithirisha UASI!!!!!
Hivi Kati ya alietengeneza Gari na Gari lenyewe yupi alikuwa anamuhitaji mwenzake? Of course ni alietengeza Gari ndie alikuwa anahitaji sana Gari! Na sio Gari kumuhitaji mtengenezaji, Sasa unaposema amemfanyia nini mungu hili swali linakosa mantiki! Hapo kiuhalisia anaemuhitaji mwenzake sana ni Mungu ndio anamuhitaji sana binadamu ndio maana akamuumba!
 
Kwahiyo hili ulichokiandika unasema hoja. Sasa njoo tujadili kwa masharti haya mawili tu :

1. Hakikisha kila swali ninalo kuuliza unajibu
2. Hakikisha unamjua huyu Mungu ambaye unamkana.

Naanzia hapa, Wapi kimeandikwa kama Dunia itaangamizwa kwa ajili yetu ? Mimi ni Muislamu, nataka ujadili jambo kwa mujibu wa Uislamu, maana Kuna sehemu ulijinadi kwamba unajua Uislamu ( Ila kiukweli kwa ulicho kiandika unaonyesha wazi huujui Uislamu).

Nukta ya kuiangamiza Dunia kwanza unatakiwa ulete ukweli wake.

Nakuja kwenye kuumba Moto, Mola wetu ametuumba kwa malengo, na akaweka utaratibu ya kuwa watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli wataingizwa motoni, hili alilijua na anajua fulani wa motoni na fulani wa peponi.

Lakini alipo tuumba akatupa akili, matashi na hali wezekano ya kufanya mema na kufanya maovu. Katika hayo akaweka mlango wa kusamehe pale mtu utakapo kosea.

Hakuna sehemu ambapo kimeandikwa kwamba Mola wetu ametuumba ili tukosee, hili halipo. Haya maneno umeyapata wapi ? Bali ametuumba katika hali zote za kupatia na kukosea, na ukikosea ukiombwa msamaha kwake unasamehewa.

Sahihi kabisa na angetaka wote tumuamini angefanya hivyo, akatuumba na kutupa uhuru wa kufanya tunayotaka, ndio maana wewe Leo hii unamkana na humjui, lakini anakupa pumzi na kukulea.

Kwa akili ya mwanadamu, ungeumbwa katika hali hiyo unayo itaka pia ungelala, na Mola wetu ni Mjuzi wa kuumba.
Hivi Kati ya mungu na binadamu ni nani aliyekuwa na uhitaji na mwenzake? Kati ya mtengenezaji na mtengenezwa?
 
Sahihi kabisa, huu ni utaratibu ambao ameuweka ili tufikie ukamilifu.

Kingine yapo mengi tu amekupa na hujamuomba, amekupa uhai, je ulimuomba akupe uhai ? Amekupa rizki je ushawahi kumuomba akupe rizki ?

Kingine Allah anafanya yote, kwanza unaweza kuombwa unachotaka ukapewa, na ukaomba unachotaka usipewe, vyote kwake anafanya. Shida yenu mnampinga Mola msie mjua.

Kujua kwake Allah hayo hayakuzuii wewe kufanya unacho taka.
Unaposema amekupa uhai je ulimuomba akupe uhai? Hapo naona huyo alah ali force mambo sababu, je kama mimi nilikuwa sitaki huo uhai? Je, Alinipa uhai kwa kujua kuwa nitafurahi sana? Je kama nilikuwa sitaki? Hapa alah amelazimisha mambo!
 
Mtume hakuwa maamuma, unajua maana ya Maamuma ? Mtume alikuwa hajui kusoma Wala kuandika na hakuwa Maamuma. Halafu unataka kujadili kuhusu jambo hili na hujui maana ya maneno unayo yatumia ?

Haya hakuwa anajua kuandika, hoja yako Iko wapi ?

Nakupa kazi hapa uje uonyeshe ya kuwa Mtume hakuwa anashushiwa maagizo.

Sasa uongo hapo uko wapi ? Kwamba kupewa Wanawake 72 ni jambo baya ? Kuzagamua ni jambo baya ?
Na wanawake wanapewa nini huko peponi maana naona ahadi nzuri ni kwa wanaume tu!
 
Yesu hawezi kuwa Mungu hajawahi kuwa Mungu na hatokuwa Mungu.

Kijana nasisitiza hatuishi kwa kubahatisha, leta mfano hai.
Bwana kisai naomba unisaidie majibu haya, chanzo cha dhambi ni nini! Shetani ni nani alitokea wapi! Kama dunia hapo mwanzo ilikuwa na watu wawili tu mbona Kuna races mbali Bali mfano waafrika, wahindi, wachina nk. Asante
 
Bwana kisai naomba unisaidie majibu haya, chanzo cha dhambi ni nini! Shetani ni nani alitokea wapi! Kama dunia hapo mwanzo ilikuwa na watu wawili tu mbona Kuna races mbali Bali mfano waafrika, wahindi, wachina nk. Asante
Kisai unahitajika hapa ndugu
 
Mpumbavu Namba moja duniani naweza kusema pacha wa firauni wewe. Wewe mtoa post ni firauni wa pili, mwenzio aliomba poo kwasbb aliletewa mtu wa kumuonya na akakana. Wewe ujumbe umeukuta na shuhuda za waliopita umezisikia na zipo vitabuni ila unajitia ubazazi dawa yko iko jikoni.
We mfia dini firauni sio Jina la mtu ni cheo ama wadhifa...ni kama Rais au mfalme, ukitaja firauni lazima utaje ni firauni yupi mana Egypt ya zamani ilitawaliwa na firauni kadhaa.
Halafu pia utuambie huyo mtu alieletwa Kwa firauni alikuwa wa dini ipi? Alikuwa mkristo ama muislamu?
 
Mpumbavu Namba moja duniani naweza kusema pacha wa firauni wewe. Wewe mtoa post ni firauni wa pili, mwenzio aliomba poo kwasbb aliletewa mtu wa kumuonya na akakana. Wewe ujumbe umeukuta na shuhuda za waliopita umezisikia na zipo vitabuni ila unajitia ubazazi dawa yko iko jikoni.
Mkuu kwa umri wangu huu unadhani nitatishika na vitisho vya kitoto kama hivyo? 😂😂😂
 
Back
Top Bottom