Uongo na Usanii wa Bw.Raila Odinga!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Niliposikia hili swala nilistaajabu sana ya kwamba Bw.Raila Odinga ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kibera (Slum ya Nairobi) alishawahi kuwa Waziri wa Nyumba huko Kenya na bado hakuweza kuwapatia watu wa Jimbo lake la Kibera/Slum makazi bora iweje leo hii Mtu huyo huyo anasema kwamba anataka kutawala Kenya na kwamba atakuwa Raisi (Raila) bora wa Kenya, ni kwa nini Wakenya hawamuulizi kama Kibera ilimshinda atawezaje Kenya yote?
 


Little knowledge sometimes is very dangerous
 


huyo raila odinga wenu huko kenya hana tofauti sana na mtanzania wetu mmoja ambaye anautaka " urais " kwa udi na uvumba tena hadi anawahonga watu lakini cha kushangaza kijiji au eneo analotokea watu wana " umasikini " mkubwa hadi katika " kope " zao za macho. ni usanii mtupu!
 

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Wewe hapa juzi tu ulitokwa na povu wakati wenzio walimkashifu mgombea wako wa urais Lowassa ambaye pia aliwahi kuwa waziri mkuu Tanzania, na hiyo nchi bado ipo kwenye lindi la umaskini. Sasa iweje leo wewe hapa umekua na ubavu wa kumsuta Raila na kwa lawama kama zile zinazomfuata huyo huyo Lowassa.
 

Ni nani amekwambia nina Mgombea Uraisi? Bw.Lowasa siyo mgombea uraisi wangu na wala siyo chaguo langu kwanza mimi hata kura huwa sipigi na ndio maana nawashangaa wanaopoteza muda kuwapigia kura watu kama Bw.Raila Odinga ambao wakati walikuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko hawakufanya hivyo ila sasa wametoka ndiyo wanawaambia wapiga kura kwamba watakuwa tofauti wakipata uraisi!
 
Huyu mzee toka Moi am castrate akili imemruka kabisa
 

Haujui historia na siasa za Kibera vizuri ndio uweze kutoa matamshi kama haya.
Yeye ndiye alikuwa mmoja wa wanzilishi wa Kibera Slum Upgrading Programme mwaka 2003 ambalo kwa sasa limekwama. Fanya research ni kwasababu gani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…