Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
Ni habari gani sasa unaweza kuipokea mikono miwili kutoka Yanga? Nje ya nje uliyoishuhudia mwenyewe? Hii haijaanza leo, ila sikutegemea kama ingeendelea hadi leo.
Taasisi yeyote kuwa katika midomo ya watu ni jambo bora sana. Ni miaka mingi imepita sasa tuliaminishwa kuwa ' There is no such thing as a bad publicity. Hii kusema chochote ambacho kitakufanya uzungumziwe wewe fanya tu, haiwezi kukuletea madhara yeyote bali ni faida pekee. Taasisi nyingi zimepoteza uaminifu, zimeangukia katika mikono ya sheria na nyingine hadi kufilisika kabisa sababu ya kufuata hiyo kauli.
Turudi sasa kwa Yanga. Yanga imekuwa ikitafuta attention kwa jamii kwa kuzusha mambo makubwa, mengi kutoka kiongozi wa juu kabisa , Rais wa Klabu. Yes, umesoma vizuri kuwa ni Rais wa klabu ya Yanga, na mengine kutoka kwa vijana wake ngazi ya chini ili Klabu ya yanga ipate kuzungumzika, au kupitisha ajenda fulani lakini baadae mambo yanakuja kuwa tofauti.
Je madhara yake ni yapi kwa sasa? Watanzania wamepoteza imani na taarifa zinazotolewa na viongozi wa Klabu. Leo taarifa ya Ali Kamwe ya kujiuzulu inatoka, kila mtu anajua simple tu ni attention tu kwa ajili ya Siku ya Wananchi. Rais wa Klabu wakati anatangaza kuwa Aziz Ki haja-saini mkataba, jamii nzima ilijua kuwa ni kutafuta attention.
Hata issue ya Chama kabla hajatangazwa watanzania waliamini kuwa ni maneno tu maana misimu yote walikuwa wanatangaza ku-msign lakini mambo yakawa tofauti, hadi pale alipokuja kutangazwa. Hii sio bahati mbaya, bali tayari wananchi wamepoteza imani na taarifa za viongozi wao. Maana ni hao hao walimtangaza Bernard Morrison kama sehemu ya mchezaji wao siku ya Mwananchi, lakini msimu mzima alicheza Yanga.
Mfano hata ile taarifa kutoka kwa Boss wao (Magoma), wengi waliamini ni attention tu, sababu uongo uongo imekua tabia yako. Lakini unajiuliza jambo kubwa ambalo linahusisha mahakama ila bado watu hawaamini. Hofu yangu kubwa kuwa kuna kesho, unaweza kuwa na taarifa kubwa, lakini watu bado watahisi michezo ni ile ile.
Bahati mbaya attention nyingi zinazitengenezwa unakuta zinaleta maumivu kwa mashabiki zao weinyewe, kwa wale ambao mwanzo huwa wanaamini taarifa hizo.
Kuweni wabunifu, hizi attention za uongo uongo zinaharibu nembo ya Klabu. Haya mambo waachieni wale vijana wa You Tube - vloggers(Youtubers). Tunajua hakuna amsha amsha kuelekea tamasha lenu, ila tafuateni namna ya kuvuta watu na sio kuleta uongo uongo.
Jifunzeni kwa majirani zenu. Hapa kitengo cha habari kimepwaya kidogo.
Hivi mnakumbuka msimu ulipita tamasha leo lilizimwa na jambo la kishezi la "Kibegi- msafara wa uzinduzi wa jezi?
Amkeni. Ila acheni uongo uongo.