Uongo upi unaoukumbuka uliambiwa wakati ukiwa mdogo na ulijua ni ukweli

Uongo upi unaoukumbuka uliambiwa wakati ukiwa mdogo na ulijua ni ukweli

fizo talent

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
2,255
Reaction score
3,889
Naam wakati tukiwa ktk maombolezo ya ndugu zetu waliopoteza maisha ktk ajali iliyotokea ktk ziwa victoria ikihusisha kivuko cha MV Nyerere.Mungu azilaze roho za marehem mahala pema peponi Aamiin.
Tukija ktk mada wakati tukiwa watoto wadogo hususani ktk kipindi ambacho hujaanza kung'amua mbivu na mbichi huwa una maswali mengi ambayo huwa unayauliza,na maswali yenyewe huwenda yakawa na maana au yasiwe na maana ila majibu unayopewa mengine ni ya ukweli ama mengine ni uongo/chai.

Baadhi ya maswali niliyouliza na nikapewa majibu ambayo baada ya kujitambua nilikuja gundua kua ni chai/uongo wa kutupwa;

swali:mama mimi nimetoka wapi
jibu;umetoka humu(hapo mama anapanua kinywa na kunionesha nilipotokea)

swali:baba shuleni ulikuwa unatoka mtu wa ngapi
jibu;mimi nilikua mwalimu kazi yangu kufundisha(hata taaluma ya ualimu hana[emoji13] [emoji13] [emoji13])

swali;bibi kwa nini huna meno
jibu;meno yangu kachukua kunguru

Nitaongezea kadri nitakavyokumbuka,weka na ww uongo uliokua unapewa au unawapa wanao kutokana na maswali yao
 
kuna zile ndege zikiwa angani zinatoa moshi mweupe na kutengeneza kama barabara fulan hv. sa walitudanganya ni za mizigo tuu na viwanja vyao vipo S.A na Egypt.
aisee Mungu anawaona
 
  • Thanks
Reactions: ywf
Duu na mpaka leo hulipendi au umebadili mawazo
sasa hivi nakula ila silipendelei sana yan hata papai nilokua naambiwa ukimeza mbegu mpapai utaniota bas na mm nauliza kwa hiyo ntakaa na mpapai kichwa watu watakua wanarembea mawe kuangusha mapapai kichwan mwangu halaf ntalalaje humu ndani baba ananambia tutakua tunaupunguza matawi uweze kupita ndani jaman sikutaka shida yake matunda sikuyala nimekuja kiyala nikiwa naelewa ukubwani tena
 
aisee...ushawahi kujua kwa nini ulipewa majibu ya kuogopesha hivyo
 
aisee...ushawahi kujua kwa nini ulipewa majibu ya kuogopesha hivyo
hata sikua najua sema nikiwa napewa chungwa kitu cha kwanza baba alikua annambia hakikisha umetoa mbegu ndio ule mm ule muda sina wa kutoa mbegu nakula tu ndio ikaja hio mfano wa tikiti maji pia siwez kaa chin nitoe mbegu nabugia tu baada ya kuambiwa hivo ndio kama wakanambia usile hivi vitu
 
kumbe ulikua wa kutoa mbegu ndio maana alikua anakupa vitisho ili ukumbuke kutoa
 
Back
Top Bottom