Uongo wa Masoud Othman waumbuliwa. Kadanganya taifa kwamba "+259" ndiyo "Code" ya Zanzibar na "+255" ni ya Tanganyika wakati sivyo

Sina digrii,sina gari wala chochote cha maana kama walivyo wana JF wengi.
Kwangu hii habari ni ya kutengenezwa tu kwa lengo mahususi.
Cha muhimu ktk habari hii ni elimu tu! Ule uwezo wa kuweza kutafsiri ulichosoma.

Z'bar wanajiliza-liza sana! wanapewa favour nyingi sana kuliko watu wa Tanganyika, lakini kila siku ni kulia-lia tu! Shida ni nini?

Leo hii kuna wa-Zenj kibao wanafanyakazi ktk wizara ambazo siyo za muungano. Wakati huo huo hutakuta m-Tanganyika anafanyakazi SMZ, hata mmoja! Bado wanajiliza-liza na namba za simu.
 
Namba hii inatumiwa na nchi gani kwa sasa? Ili ikiwa kuna inchi inatumia itakuwa kweli Masoud ni muongo kinyume chake hiyo namba iko wazi, hivyo Masoud hatokuwa muongo

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
1630932681013.png
 
Unadai Zanzibar ilianzisha televisheni yake 1974! Pia ilipewa code no. yake mwaka 1968 lakini ikanyang'anywa mwaka 1999 kwa vile walishindwa kuitumia hapo hapo unadai Zanzibar haiwezi kurudishiwa hiyo code kwa sababu si mwanachama wa UN,je wakati huo wakipewa walikuwa wanachama wa UN?
Naomba ufafanuzi zaidi.
Jamani mueleweni mtoa mada yeye amenukuu tu
 
Cha muhimu ktk habari hii ni elimu tu! Ule uwezo wa kuweza kutafsiri ulichosoma.
Z'bar wanajiliza-liza sana! wanapewa favour nyingi sana kuliko watu wa Tanganyika, lakini kila siku ni kulia-lia tu! Shida ni nini?

Leo hii kuna wa-Zenj kibao wanafanyakazi ktk wizara ambazo siyo za muungano. Wakati huo huo hutakuta m-Tanganyika anafanyakazi SMZ, hata mmoja! Bado wanajiliza-liza na namba za simu.
Wakati umefika pande mbili hizi za muungano zikae chini kujadili maboresho ili muungano uendelee kuwa thabiti kuliko hali ilivyo sasa kila upande kulalamika juu ya hiki na kile.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi lakini habari yenyewe kwa maana ya hayo yaliyosemwa kama yalifanyika hivyo kweli au la maana hapo alipozungumzia televisheni ndio kumenipa ukakasi kwani ninavyofahamu televisheni ya Zanzibar ilianzishwa na uongozi wa Karume akiwa hai na Karume amekufa mwaka 1972 sasa najiuliza kama ameongopa hapo vipi hayo maelezo mengine? Hasa ukizingatia Wabongo wengi si wafuatiliaji wa mambo lakini pia imekuwa ni kawaida mambo mengi ya huko nyuma kuelezwa ndivyo sivyo kwani hata historia ya harakati za kutafuta uhuru inadaiwa mengi yamefinyangwa finyangwa kwa sababu wanazozijua hao wahusika hivyo si ajabu kuona hili nalo likawa ni hivyo hivyo.
Atakuwa alikosea kuhusu kuanzishwa kwa televisheni.

Mimi naona tatizo ni wazanzibari kutaka kuwatwika watanganyika mzigo wa matatizo yao yote! Hata yale yanayotokana na uzembe na unadhirifu wao wanasingizia JMT. Juzi juzi tuu Mwinyi ameamuru meli zilizonunuliwa na SMZ ziuzwe kwa sababu ni hasara tupu. Wote tunajua matatizo ya bandari ya Unguja yanatokana na usimazi mbovu wa SMZ. Na tunajua chuki kati ya wapemba na waunguja ndio imechangia kwa kiasi kikubwa matatizo yaliyokuwepo. Sasa hili la code nalo linataka kugeuzwa kuwa ni ushahidi kuwa JMT haiitakii mema Zanziba wakati sio kweli.

Amandla...
 
Punguwani mkubwa, umekaa kiubishiubishi ndiyo maana huelewi researcher alivyoturahisishia kuielewa hii habari.

Karume alizindua ujenzi wa mitambo ya televisheni mwanzoni mwa mwaka 1972 kabla hajauawa.

Aboud Jumbe akaizindua TV ianzr utangazaji January 12, 1974 siku ya kuazimisha miaka 10 ya mapinduzi.

Joseph amefanya utafiti wa uhakika na mimi siyo mara ya kwanza kusoma tafiti zake.

Masoud ni mwongo kaumbuliwa na researchers wanaomzidi.

Kulikuwa hamna haja ya kumtukana.

Amandla...
 
Hajaanzisha uzi.

Kaleta habari kama research ilivyotumwa kwenye gazeti na mtafiti.

Sasa jina na namba ya mwansidhi imo unaweza kumuuliza.

Amenukuu akaamua aje kuanzisha uzi sasa tumuulize nani kama sio mwenye uzi wake? Sisi huyo mwingine hatumjui.
 
TITLE: UKWELI KUHUSU NAMBA YA SIMU YA KIMATAIFA "+259"
ANALYST: JOSEPH MAGATA
Cell: +255 75 4710684
PUBLICATION: RAIA MWEMA, pg. 12

Juni 8, mwaka huu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud alitoa hotuba ambayo sehemu ninayoinukuu anasema,

"Kwenye serikali hiihii ambayo tumekuwa nayo ndiyo vikwazo vya kila aina, miye nawapa kimoja tu kwa mfano.Tulipoanza simu, zile zilisosajiliwa Bara, TRITEL, sijui nani, walipewa leseni mara moja. Ilipokuja ZANTEL ikasajiliwa Zanzibar. Kosa lake kusajiliwa Zanzibar. Ukawa ugomvi, ikawa vita vikubwa kwelikweli".

"Mpaka tukafika Geneva kwenye Shirika la Simu duniani, ITU, kwenda kusuluhishwa na baada ya kutishia kwamba tutakwenda kudai namba yetu 259." Maana hii tunayoitumia leo, "255" ni ya Tanganyika, ya Zanzibar ambayo mpaka leo hii ipo hajapewa mtu mwingine ni "259". Na ilibidi kwenda (ITU) kutishia kuidai ile namba kwa sababu wenzetu wamekataa kutupa leseni".

Je ITU walikoenda Masoud na wenzake wa Zanzibar ina majukumu gani?

Teknolojia ya "telegraph" iliyovumbuliwa mwaka 1837 ilitoa huduma za kutuma maandishi (telegram), kutuma pesa (moneygram) na baadaye "telex". Hivyo mwaka 1865 ITU ikaundwa ikiitwa "International Telegraph Union" kusimamia viwango vya teknolojia hii.

Mwaka 1876 teknolojia ya simu nayo ikavumbuliwa, kisha ikafuata ya redio na baadaye ya televisheni. Kufikia mwaka 1934 zikawepo teknolojia hizi nne, redio, "telegraph", simu na televisheni. Japo ITU ilianzishwa kusimamia "telegraph" ikajikuta inasimamia na hizi tatu, hivyo ikaitwa "International Telecommunication Union".

Teknolojia ya simu iliposambaa ilikosa mfumo unaofanana wa simu zinazoenda nje ya nchi, kila nchi iliunda wake. ITU ikaunda mfumo unaoitwa sasa "E.164" wa nchi kuwa na namba ya simu. Hivyo ITU ilipokutana Mei 25 hadi Juni 26, 1964 ilizipa nchi 129 namba za simu, ikiwemo Tanzania iliyopewa namba "255". Mkutano huo ulipogawa namba za "telex" Tanzania ilipewa "989". Taarifa ya mkutano huo imo kwenye ripoti inayoitwa "Blue Book".

Mkutano uliofuata wa Septemba 23 hadi Oktoba 25, 1968 uliipa Zanzibar namba ya simu "259". Ndugu Cromarty wa Tanzania aliushiriki kama inavyoonyesha ripoti inayoitwa "White Book". Hivyo mtu aliyepiga simu Zanzibar alipaswa sasa aache kutumia namba "255" ya Tanzania atumie "259" ya Zanzibar.

Je kwa nini Zanzibar ilipewa namba yake kama vile ni nchi tofauti na Tanzania? Muungano wetu uliipa dola ya Zanzibar mamlaka kwenye masuala yasiyo ya muungano ambapo teknolojia ya simu haikuwa suala la muungano.

Kwa kuwa "telegraph" ndiyo iliyokuwa suala la muungano, Zanzibar haikupewa namba ya "telex" ambayo ni huduma na "telegraph", ikabaki na mamlaka kwa teknolojia tatu zilizobaki yaani televisheni, redio na simu.

Je dola ya Zanzibar ilitumiaje mamlaka yake kwenye televisheni, redio na simu? Tangu siku ya muungano Zanzibar ilibaki na redio yake. Mwaka 1974 ilianzisha televisheni yake. Kitu ambacho haikukifanya ni kuweka teknolojia inayopokea simu zinazoanzwa na "259". Matokeo yake Zanzibar ikaendelea kutumia ya namba ya Tanzania "255".

Simu zetu zote duniani ziko katika ule mfumo "E.164" ambao kwa kirefu unaitwa "ITU-T Recommendation E.164". ITU hutangaza taarifa ya mfumo huu panapotokea mabadiliko ya simu katika nchi yoyote. Taarifa ya Novemba 15, 1995 ilionyesha kwamba "259" ilikuwa bado ni namba ya Zanzibar. Baada ya taarifa hii ITU iliweka viwango vipya kudhibiti matumizi ya namba vilivyoanza kutumika Machi 9, 1998 vikiitwa "E.164.1". Tuone vifungu vitatu ndani ya viwango hivyo yaani kifungu cha 5.13, 5.14 na 6.2.1.

Kifungu cha 5.13 na 5.14 kinasema ITU itanyang'anya namba zote duniani zisizotumika vizuri. Je Zanzibar ilitumia vizuri namba yake "259"? Zanzibar si tu haikuitumia vizuri bali haikuitumia kabisa kwa miaka thelathini. Hivyo Machi 1, 1999 ITU iliinyang'anya Zanzibar hii namba "259" kupitia tangazo "ITU Operational Bulletin No. 687".

Hii maana yake taarifa ile ya Novemba 15, 1995 ilikuwa ya mwisho kuionyesha Zanzibar kama nchi inayotumia namba "259". Hivyo haijulikani kwa nini Masoud anapotosha kwamba "259" bado ni namba ya Zanzibar wakati Zanzibar ilishanyang'anywa namba hiyo tangu mwaka 1999.

Waliohamasishwa na hotuba ya Masoud walitamka palepale wanavyotaka Zanzibar irudishiwe hii namba yake. Je, kurudishiwa huko kunawezekana? Kifungu cha 6.2.1 cha viwango vile kinasema nchi isiyotambulika Umoja wa Mataifa (UN) au ITU haipewi namba. Zanzibar haitambuliki UN wala ITU hivyo haiwezi kupewa namba yoyote.

Uzoefu ulioonekana kabla ya mwaka 1998 unaonyesha kuwa Hong Kong ilibaki na namba yake "+852" ilipoungana na China kama Taiwan ilivyobaki na "+886" ilipoondolewa UN. Kote huko kitendo cha kutotambulika UN kimekuta taifa lilishazoea namba yake, hivyo ITU haikuwanyang'anya.

Kuanzia mwaka 1998 ITU ilizingatia miungano kwa kifungu cha 6.3.2 cha vigezo vile kinachosema nchi zikiungana zitabaki na namba moja tu. Hivyo Hong Kong nayo ingechelewa kama Zanzibar, ingelazimika kutumia namba ya China "+86".

Ukiwa katika sekta ya mawasiliano unalazimika kusoma sana na kutafiti sana kila siku. Wazoefu wa sekta hii wanajua inapotokea fursa unalazimika kuisoma palepale, kuielewa palepale na kuitumia palepale.

Tumeona Zanzibar ilivyopata fursa ya mamlaka kwenye redio, televisheni na simu. Fursa hiyo iliyowaletea televisheni haikutumika kuwaletea teknolojia inayoelekeza simu za namba yao zifike Zanzibar. Kama wangeitumia, basi mwaka 1999 ungekuta namba "259" inatumika hivyo ITU isingewanyang'anya kama Taiwan na Hong Kong.

Hivyo namba "255" siyo ya Tanganyika kama anavyohamasisha Masoud bali ni ya Tanzania. Vilevile "259" siyo namba ya Zanzibar bali ilipewa kihalali mwaka 1968 na ikanyang'anywa kihalali mwaka 1999.
Elimu nzuri kabisa. Nakupa big up
 
Mbona Tanganyika Law Society iko hadi leo?!

Tanganyika bado ipo bwashee usihadaike na wanasiasa.

Othman yuko sahihi.

..sitashangaa nikisikia Othman Masoud, Hussein Mwinyi, na Samia Suluhu, lao ni moja kuhusu Znz kutumia code ya 259.

..Wazn huwa ni kitu kimoja ktk mambo mengi dhidi ya Tanganyika, isipokuwa suala la serikali 2 au 3.

..Na kukumbushia, mikutano ya chama cha upinzani cha Znz, ACT-Wazalendo, inafanyika bila bugudha na mazuio ya vyombo vya dola.
 
Sasa huko kuumbuliwa kuko wapi? Wakati mwingine mihemko ndio huonesha picha halisi ya mhusika
 
Ndugu Paschal Mayala, Unatuzingua wazenji, Utumbu usituletee na kuitwa kiongozi wetu muongo halikubaliki. Sisi wazenji tuna mila na desturi zetu na kuna lugha ya kutumia ambayo haileti hisia za chuki. Mwandishi wa nakala hii na mletaji wake ni watu dhaifu sana. Ni watu wenye chuki na ubaya wa roho juu ya zanzibar. Kwa ufupi wazanzibari wamechoka kuhusu kero za muungano na usanii wa viongozi watanzania. The first opportunity we get, we'll be out of this UNION."
 
Tokeni, kwani nani anawataka
 
Namba +259 siyo yenu Masoud ni mwongo kaumbuliwa na Joseph.

Back
Top Bottom