Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Kuna siku moja nilikuwa naskiliza redio majira ya saa 4 usiku, sikumbuki vyema mada iliyoko mezani ililenga nini haswa, ila nakumbuka kulikua na maswala ya ufumbuzi wa matatizo katika njia ya asili.
Siku ile studioni alikua ameambatana na mganga ambaye alikuwa amealikwa kwa ajili ya kutoa mchango wake wa mawazo kulingana na mada iliyokua kikaangoni ni sehemu ya taaluma yake.
Wasikilizaji waliweza kuchangia changamoto zao ambazo wanapitia ili watatuliwe. karibia kila mmoja aliyeeleza matatizo yake alipewa jibu ambalo linaonesha kama matatizo yake yamechangiwa na ushirikina au kurogwa.
Kuna matatizo mengine waliyokua wanayataja yalikua hata mimi nishawahi yapitia lakini huyo mganga aliwapa jibu kua chanzo chake ni umetupiwa jini, na mwisho anakupa adress mahali camp yake ilipo uende akakutibie katika njia za kiganga.
Sasa mwishoni wakati mtangazaji anamalizia kipindi akatoa kinyang'anyiro cha fursa kwa simu mbili za mwisho kutoka kwa wadau wasikilizaji waweze kuongea na mganga.
Simu ya kwanza, jamaa alipiga simu kisha studio ikapokelewa na yule mganga aliyealikwa hapo redioni.
Mganga akamuambia jamaa kua nitajie majina yako matatu halafu mimi nitakufanyia online scanning kujua matatizo yako pasipo wewe kuniambia.
Jamaa akamtajia majina yake yote kisha mganga akapiga chafya afu akasema mizimu yangu inasema wewe unashida na pesa NDIYO au HAPANA jamaa kinyonge akasema ndiyo.
Sasa hapa ndio nilianza kuona huyu mganga ni fix, imagine kwamba unajua mtu yuko jangwani na unajua jangwani ni kukame halafu unamuambia nakutabiria changamoto zako kabla hujaniambia, changamoto yako inayokusumbua hapo ulipo ni uhaba wa maji.
Sasa huu nao ni utabiri au utapeli?
Simu ya pili jamaa akapiga simu kataja majina yake matatu naye mganga hakuchukua muda kutoa majibu.
Round hii alianza kwa kusema kua wewe bwana ni mbishi sana yani hukubali kitu hata uambiwaje, jamaa kanyuti tu anaskilizia aambiwe matatizo yake.
Mganga akamuambia kua siku chache zilizopita ulikua na mgogoro na mke wako. Jamaa akasema awapi mbona mi sina mke bwana mganga?
Mganga akasema kama nilivyosema mwanzo kua wewe ni mbishi hua hukubali ukweli utakaoambiwa, mtangazaji akacheka sana.
Jamaa akaendelea kusisitiza kwamba hapana mganga nachosema namaanisha mimi sijawahi kuoa na niko serious.
Labda kama majina yangu umeyatafsiri vibaya na ndio maana yameleta majibu kutoka kwa mtu mwingine jamaa akataja majina yake upya kwa msisitizo huku akiendelea kusema tatizo langu ni ugonjwa.
Nina miaka mitatu naumwa ugonjwa ambao hata siujui ni nini, na kuna sometimes napata nafuu unatulia lakini kuna muda tena hali hubadilika.
Nimepiga simu hapo redioni ili nipate ufumbuzi wa hili tatizo langu basi.
Mganga naye akawambishi kua jamaa anapinga ukweli wa mganga kutokana na tabia yake ambayo mganga kamtabiria sa ikawa kila mtu kashikilia tawi lake kua ye ndiye mkweli.
Hapo utagundua kua mganga alisha-set mazingira akiwa kwenye camp yake kabla hajafika hata studio. Jibu lake alilolitanguliza mwanzo kua mshkaji ni mbishi lilikua ni break ya hoja yeyote ambayo jamaa angeileta.
Na ndio maana jamaa kila akijitahidi kupinga kua hakuwa na mgogoro ye na mkewe kwasababu hakuoa mganga ana-apply lile jibu lake la mwanzo kua nilisema we ni mbishi hutaki kukubali ukweli utaoambiwa.
Dakika ya mwisho mganga anatoka studio na point tatu huku yule jamaa akiwa yuko high kapenyezewa taarifa ya uongo na madai yake ya kujisafisha kujionesha yumkweli yanakua ni affected na propaganda za mganga.
Hebu vuta picha mganga ndio kasema maneno ya uongo mbele za watu wanaokuheshimu na uongo huo wa mganga unaweza kupelekea maelewano we na ndugu zako kutokua mazuri. Utatumia mbinu gani kukwepa hilo tego um-prove wrong bwana mganga kwa umma uliokuzunguka aonekane ye ndiye muongo?