SoC01 Uongozi bora kwa maendeleo ya Taifa

SoC01 Uongozi bora kwa maendeleo ya Taifa

Stories of Change - 2021 Competition

Tycoon44

New Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
3
Reaction score
0
UONGOZI BORA KWA MAENDELEO YA TAIFA”

Wengi tunajua sifa mbalimbali za viongozi bora waliopo na hata waliopita, basi sasa naend kueleza vitu vichache kwa upana zaidi juu ya viongozi ama uongozi bora kwa maendeleo ya familia,ukoo,mtaa,kijiji,kata nk mpaka kwa ngazi ya Taifa.
>Kwanza, Kiongozi ni nani? Hili ndilo swali kubwa la kujiuliza na kupata majibu yake kabla ya kuendelea na vitu vingine. KIONGOZI: Ni mtu mwenye mamlaka ama karama ya kuonyesha watu njia kwa vitendo kwa kuwajibika na kushughulika na kikundi alichokarimiwa. Hii ndio maana fupi ya kiongozi. Basi kwa kujua maana ya kiongozi ni nani? jee? Tunamjua KIONGOZI BORA NI YUPI? La hasha! Inabidi naye tumjue.
Kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wengi ama miaka mingi katika uongozi ?LA HASHA ! Kiongozi bora hujengwa kwa sifa anuwai na nzuri zenye ukweli ndani yake.

Ni rahisi kufikiri kuwa kiongozi bora hutokea kwa bahati au hakuna haja ya kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi bora ama kujua yupi kiongozi bora .
Wewe kama mtu unayehitaja kusimamia na kuratibu shughuli fulani ni lazima ufahamu sifa zinazomfanya mtu kuwa kiongozi bora ili uwe na MAFANIKIO.
Ningependa kunukuu maneno ya “JOHN QUINCY ADAMS” alisema..

“”KAMA MATENDO YAKO YANAWAHAMASISHA WENGINE KUPATA NDOTO ZAIDI,KUJIFUNZA ZAIDI,KUFANYA NA KUWA ZAIDI,WEWE NI KIONGOZI.””

Kama nilivyosema awali nitasema sifa chache ama wasifu mfupi wa kuongozi bora mwenye uwezo wa kuleta maendeleo,mshikamano na amani katika Taifa. Sifa/Wasifu huo ni kama ufuatavyo;-

1.UADILIFU
Ili uwe kiongozi bora huna budi kuwa mwadilifu.Heshimu kazi,tunza muda,tunza fedha na mali pia tumia nafasi yako kwa njia ambayo siyo ya kibadhirifu.
Ni rahisi mtu kushawishika kutumia ofisi au nafasi ya uongozi aliyonayo kwa maslahi binafsi jambo ambalo hupekea kupoteza dira ya watu awaongozao hata sifa za uongozi wake kupotea.



2.UJASIRI.
Huwezi kuwa kiongozi bora kama hautakuwa na ujasiri juu ya mambo mbalimbali .Unahitaji ujasiri wa kutosha katika kufanya maamuzi katika taasisi ama nyanja mbalimbali kama vile:-kufanya uwekezaji mpya,kubadili mfumo wa utendaji katika taasisi uliyopo n.k.

Lazima kiongozi aonyeshe ujasiri kwa watu anaowaongoza katika nyanja zote anazosimamia na katika maamuzi yake ya kila siku.


3.UBUNIFU/MBUNIFU.
Mafanikio katika kila taadisi ama kampuni yeyote duniani inahitaji ubunifu wa njia mbalimbali za kufikia malengo ya juu hivyo kiongozi bora anahitaji kuwa mbunifu mwenye mawazo na mbinu mpya kila siku za kufikia malengo waliyojiwekea.
Kiongozi huna budi kuepuka kuwa na mawazo yaleyale ya kila siku hata kama yanaleta faida kwani mambo hubadilika pasi habari.
Kama Bwn:STEVE JOBS alivyosema
“”UBUNIFU UNATOFAUTISHA KATI YA KIONGOZI NA MFUASI”””

4.UWAJIBIKAJI/UTUMISHI.

Bwana:ALLEN WEST alisema..
“”UONGOZI NI KUWA MTUMISHI KWANZA””
Hivyo kuwa kuongozi bora huambatana na uwajibikaji. Ni lazima kiongozi uwajibike kutimiza katika mbio zz kutimiza majukumu na njonzi zako zote ulizojiwekea.
Kwani kuwajibuka kwako kutafanya hata wale uwaongozao wawajibike sawasawa na nyendo za kiongozi wao kwani kiongozi ni kichwa .

5.UWAZI NA UKWELI.
Kiongozi huna budi ya kuwa muwazi na mkweli katika kila neno lako kwani kiongozi hupaswi kuwa msiri na muongo kwa kufanya hivyo utakuwa kiongozi bora mwenye nafasi njema katika idara yako.
Ukweli nz uwazi ndio gwaride pekee la mafanikio kwani uongo na siri hurudisha maendeleo nyuma kwa kasi ya ajabu.


6.MAONO.
“Kiongozi ni yule anajejua njia,Anaiendea njia na Anaonyesha njia””

Hayo ni maneno ya Mh:John C Maxwell
Maono ni picha inayojengeka katika fikra ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa.

Kama wewe ni kiongozi na huna maoni ya kule uendako basi htaweza fikia malengo ama mafanikio yanayohitajika hivyo huna budi kuwa na maono juu ya kule uendako .

7.MAWASILIANO.
Mawasiliano
ni jambo kubwa sana linalojenga utawala mzuri na wenye nguvu katika kila taasisi ama kampuni na mahali popote kule hivyo kiongozi unapaswa kuwa na mawasilia Mazuri na watu wote wale unaowaongoza na hata usiowaongoza.
Nyanja kuu ya uongozi ni mawasiliano mazuri kwa kila rika na kila jinsia hivyo kama kiongz huna budi ya kuwa na mawasiliano mema.

8.NIDHAMU.
Kuna mambo ambayo hutoruhusiwa na hutakiwi kufanya hatakama wengine wanafanya na unavutiwa nayo.Wewe kama kiongozi epuka kila tabia isiyoendana na cheo chako kama ulevi,ugomvi,umbea,uvivu,anasa,kuongea hovyo n.k. Kwa kufanya hivyo utaimarika na utajenga boma/utawaka ulioimara.

9.SUBIRA/UVUMILIMU.
Kila jambo katika maisha linahitaji subira na uvumilivu kwani vitu vingi havitokei kama mwanga ila huchukua mda sana . Kama kiongozi unapaswa kuwa na subira na ubumilivu katika kila jambo ili uweze kufikia makengo jwa kushindo na uweza wa hali ya juu ..
Wakati mwingine waweza pata hasara amz usione mafanikio katika kengo ama jambo uliendeao ila kuwa na subra na uvumilivu kwani utavuka.

10.KUFIKIRI NA KUWA SABABU.
Hapa ni sehemu moja kubwa mno katika uongozi kwani kiongoz anapaswa kuwa mwenye uwezo wa kufikiria na kutoa sababu mbalimbaki za mambo tofautitafauti na sio sababu tuu bali sababu zenye mshiko na nguvu na zenye kuwa na uwazi ndani yake.
Kiongozi bora anapaswa kuwa mwenye uwezo nzuri wa kufikiria ili aweze kusulihisha mambo tofautiyofauti katika jamii aiongozayo..

HITIMISHO,
Hapa nimekueleza sifa 10 zitakaweza kumjua na kukufanya kuwa kiongozi bora.Ni wazi kabisa hakuna mafanikio yeyote yatakayotokea katika jamii ama Taifa pasi kuwa na viongozi bora hivyo ni muhimu kujua ni zipi sifa za kiongozi bora kama nilivyoweza kuzifafanua kwa ufupi hapo mwanzo.

je unamaoni ama unashida mbalimbali juu ya uongozi bora,ukulima,ufugaji,biashara waweza nitafuta kwa simu namba:
0694301909-
Ama insta tycoon de Mubezy
ASANTENI.

 
Upvote 0
Back
Top Bottom