Kiongozi si lazima awe mtu aliye katika nafasi ya mamlaka au mwenye cheo. Kimsingi, dhana nzima ya nafasi na vyeo ni mpangilio wa muda, ambao wakati mwingine hukuzwa mno na kutiwa nakshi isiyo sahihi.
Kwa bahati mbaya, wengi wakishapata vyeo/madaraka ‘hupoteza fahamu’ waziwazi! Tumewaona wenzetu kadhaa ambao awali tuliwaona wakiwa watu wenye uelewa, uwezo mkubwa wa kufikiri na utambuzi lakini walipopata vyeo (uteuzi au kwa kupanda madaraja) wamejisahau na wengine kugeuka ‘Miungu-watu’. Madaraka na uwezo vimewalevya.
Mamlaka na nguvu inayoambatana na madaraka ni nzuri, tamu kwa kadiri inavyodumu; lakini wakati mamlaka na nguvu zinachukuliwa (ukivuliwa/tumbuliwa cheo), basi jina lako pia hushuka au kuporomoka wakati huo huo.
Ikiwa unaweza kufanikiwa kujishughulisha, basi fanya hivyo. Ni hakika utakabiliwa na vikwazo vingi njiani, pia kuna wakati utashindwa, lakini kuwa na subira na usonge mbele. Toa mchango, alama na ongeza thamani.
Mafanikio ya kudumu huchukua muda mwingi na si kwa wenye moyo dhaifu. Kumbuka: Ukuu hauji kirahisi, unakuja kwa gharama kubwa hivyo lazima mtu ujitoe kikamilifu.
Mwisho: Jitahidi kuwa kiongozi katika eneo lako, hasa wakati huna mapambo au cheo! Kuwa na uongozi unaoacha alama (legacy).