Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Ninawasilimia wana Jf wote. Baada ya mapumziko ya kuandika hapa na kuwa kwenye kundi la wasomaji, leo nimerejea baada ya miaka miwili. Ninaomba mnipokee na msinifokee.
Niendelee na mada.
Katika maisha ya kila siku ya hapa Duniani kila mtu ni kiongozi, tofauti ni kuwa ni idadi ya watu unaowaongoza. Kuongoza watu wengi haimaanishi wewe ni bora kuliko kiongozi anayeongoza mtu mmoja, wawili, watatu n.k.
Unapokuwa kiongozi na ukajiona wewe ni bora kuliko wengine utegemee anguko.
Viongozi wengi waliofanikiwa kwenye maeneo Mbalimbali waliyoaminiwa ni wale walioamini mawazo shirikishi ili kukazia yale waliyonayo. Viongozi wengi walioshindwa kutoa matokeo waliyotegemea Kwenye nafasi zao ni wale ambao baada ya kupata Uongozi walibadili fikra, walibadili marafiki, walibadili watu wa kuwashauri, na walibadili Falsafa za maisha yao ya kawaida.
Sehemu yoyote inayoenda vizuri nyuma yake kuna kiongozi mzuri. Huwezi kuendelea kwenye eneo lolote lile kama sehemu hiyo hakuna uongozi mzuri.
Uongozi mzuri unaanzia na kujiongoza wewe mwenyewe nza. Huwezi kuwaongoza wengine kama wewe mwenyewe maisha yako yamekushinda.Ukiweza kujiongoza wewe mwenyewe vizuri, hata wale unaowaongoza watakuchukulia wewe kama mtu wa mfano kwako.
Kwenye kuwaongoza wengine, unapaswa kujua kwamba siyo watu wote watakupenda.
Kuna baadhi ya maamuzi utakayofanya yatawakera wengine na kuwafurahisha wengine.
Kwenye uongozi hauko pale kwa ajili ya kupendwa na kila mtu. Uko pale kwa ajili ya kusimamia maamuzi sahihi.Na kwenye kusimamia maamuzi sahihi hata kama yatakuwa na maumivu kwa baadhi ya watu.
Kazi moja ya uongozi ni kuweza kuwashawishi watu kufanya kile wasichotaka, ili kupata matokeo wanayotaka. Ukiweza kufaulu hilo, utaweza kufanikiwa sana kwenye uongozi.
Hatua ya kuchukua leo; jifunze misingi ya uongozi, kwa kuzijua tabia za watu, kujali na kutengeneza utamaduni mzuri kwa wale unaowaongoza na kuwaleta watu pamoja.
Wasaidie watu kuchukua hatua wasizozipenda kwa manufaa yao wenyewe. Na watakuja kukushukuru baadaye. Kiongozi ni pamoja na kuwa na maamzi magumu unayodhani yanaweza kuleta matokeo chanya hata kama wengine watapinga jitihada hizo.
Binadamu kwa asili ameumbiwa pia Wivu. Wapo ambao hawatatamani ufanye chochote chema, watapenda kukuona unakosea. Wao hata ukifanya vizuri watatafuta mahali pa kukukosoa. Hao usihangaike nao, wapo kwa ajili ya kukurudisha nyuma ili ushindwe kufikia malengo Yako.
Pima mawazo yao kama yanatija, kama hayanatija Songa mbele. Hii ni Falsafa ya kawaida kwenye utawala na Uongozi bora.