SoC03 Uongozi na vazi lake

SoC03 Uongozi na vazi lake

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 9, 2023
Posts
3
Reaction score
3
Uongozi ni jambo jema sana ndiyo maana uongozi upo ndani ya watu wote, na uongozi ni rafiki na shughuli za wanadamu.

Uongozi kwangu ni mamlaka ya kusimamia na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha palipo kusudiwa pafikiwe. Kuna uongozi wa aina mbili au tatu. Kuna uongozi wa kuchaguliwa, kuteuliwa, na uongozi wa majukumu binafsi.

Uongozi wa majukumu binafsi
ni uongozi binafsi wa mtu. Huu ni ule unaomfanya mtu atambulike kwa wengine, yeye ni wa namna gani, na ndio unao wapa watu imani kuhusu wewe ni nani, yaani ni wa ovyo au unafaa.

Baada ya uongozi wa majukumu binafsi kukamilika, ndipo unafata uongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa.

Uongozi wa kuchaguliwa huja baada ya watu kukuamini pale tu demokrasia itakapofanyika na kukupa kwa njia ya uchaguzi.

Na huu uongozi wa kuteuliwa huja kutokana na sifa nzuri za kuaminika, ambapo jopo hukaa na kuamua fulani anafaa kuwa kiongozi, ndipo mtu anateuliwa kusaidia kusimamia jambo fulani kama msaidizi.

Uongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa si uongozi wenye majibu ya moja kwa moja ya watu. Mimi nauita huo kuwa ni uongozi wa kutumainika, ambao pengine unaweza ukaleta majibu ya matumaini kwa watu.

Mimi napenda kusema uongozi ni vazi la kiongozi. Kama kiongozi akionekana uongozi wake ni mbaya, basi sisi tunaweza kusema kwamba kiongozi hastaili na wakati mwingine nauita uongozi kuwa ni tabia, na kiongozi ni mwili, kwa sababu tabia hutafasirisha mtu ni wa namna gani, na ndivyo ilivyo kwenye maisha.

Vazi la kiongozi ni lipi ?

Kwangu kiongozi anatakiwa awe na tabia hizi mbili Kama vazi lake.

1 TA-MA-(H)A
2 U-WA-JI-BI-KA-JI


Tamaa ( kiu) ni hali ya kupendelea, basi kama ni kiongozi anatakiwa apendelee nini ?

TA- Tanguliza maslahi ya watu wako,
Kiongozi anapswa awe mstari wa mbele kupigania maslahi ya watu wake, yaani kuona ni jinsi gani watanufaika, kupitia uongozi wake, mathalani kama mtu waliyekuamini kuwasaidia kuwaongoza na kufikia pale walipopatumaini.

MA- Maamuzi kuelekea kwenye maslahi. Ni kwel unaweza kuwa mstari wa mbele kutete maslai yao, lakini je, unawawajibishaje au unawashirikishaje katika maslahi yao ? Hii husaidia kuona atua za kimaendeleo unazozichukua juu yao, yaani kama mashuhuda wa safari ya majibu yao.

(H)A- Hakikisha maamuzi yako yanakuwa ya kimaslahi kwa wote, hii husaidia kuondoa matabaka, maana palipo na tabaka, na chuki zipo, ili mwisho wa siku usije ukaonekana uongozi wako ulikuwa umeegemea upande fulani tu.

Natoa mfano hai uliokuwepo wa viongozi wengi ambao huiga wa Hayati Mwl.J.K.Nyerere, alitanguliza maslai ya taifa, alifanyia mamuzi kwa yale alio yaona yana maslahi, na alihakikisha tumenufaika taifa lote bila kuegemea upande wowote, na ndiyo maana tuna amani na wala hatuna udini wala ukabila.
download.jpeg

Mwl.J.K.Nyerere

UWAJIBIKAJI, ni namna mambo ya yatakavyotekelezwa.

U- Uamuzi, Hii ni sifa au tabia kuu ya kiongozi kwani lazima awe na tabia ya uamuzi, kwa lengo zuri tu la kupiga hatua za kimaendeleo, na kiongozi akiwa na maamuzi ya kimaendeleo huonekana ni kiongozi mzuri, maana huchochea usikivu kwa anao waongoza.

WA- Wajibika na wawajibishe, yaani kiongozi anapo kuwa mwajibikaji na awawajibishe kwa lengo jema tu hili waweze kukamilisha uamuzi uliochukuliwa kwa ajili ya maendeleo.

JI- Jibu changamoto, au uwe jawabu lao. Hii ni tabia ya kiongozi bora. Tabia hii ya kuweza kutatua changamoto zao haraka bila wao kupaza sauti za kelele, zinakujengea heshima mbele yao na kuaminika zaidi kwani kiongozi anaye aminiwa hufanya kazi kirahisi Sana.

BI- Bidii, hii ni rahisi zaidi kwa kiongozi mwenye bidii kufikia malengo kwa maslai ya anao waongoza kwa haraka zaidi na ikitokea kiongozi hana bidii au hajitumii ili kuhakikisha hatua za maendeleo zinaenda haraka, wale anao waongoza hupunguza tumaini kwake, na huleta madhara haswa kwenye kuwaongoza, maana wanaweza wasiwe wawajibikaji tena.

KA- kamilisha mipango iliyokuwepo. Kiongozi anapaswa akamilishe mipango iliyo katika kipindi chake. Hii husaidia kuonyesha maendeleo.

JI- jipongezeni au furahini. Kiongozi mwenye tabia ya kufurahia matokeo mazuri ya kazi, huchochea maendeleo kwa jamii nzima. Ndio maana tunaweza kuona kwamba Kuna sherehe za Uhuru wa Tanganyika, sherehe za Mapinduzi ya Nzanzibar na sherehe za uzinduzi wa viwanda, na sherehe nyingine nyinyi.

Safari ya Taifa la Tanzania limepitia mikononi mwa maraisi walio na sifa za uongozi. Tumeona kwa Mwl. J.K Nyerere;Mh Ally Hassan Mwinyi; Benjamin Mkapa; Jakaya mrisho kikwete; John Pombe Magufuri; na Dr Samia Suluhu Hassan. Ongera kwao kwa makubwa walio yafanya katika Taifa letu.

images.jpeg

Hawa ni maraisi wa Tanzania

Kwa hawa viongozi, nimeona TA-MA-(H)A na U-WA-JI-BI-KA-Ji, hizi ni tabia au mavazi ambayo yeyote anayetaka kuwa kiongozi ajitathmini kama anazo tabia hizo Kabla ya kupata uongozi.

Nilisema Uongozi ni vazi au tabia, pia nikasema kiongozi ni mwili, asa kiongozi mwili wake ukoje na nini maana ya K-I-O-N-G-O-Z-I ?

K
- kubali kushauri na kushauriwa, ina maana kwamba kubali kuwasikiliza wanachotaka na pia usiache kuwashauri. Hii itasaidia masikilizano kati ya kiongozi na watu wake, na ni jambo linalowapatanisha viongozi na jamii zao pale tu wanapowasikiliza na kushauriana

I- ielewe tabia ya watu unao watawala. Hii husaidia kuendana nao Kama ni walevi basi wakati wa kuongea nao utaenda kilevi levi kama wao ili mpate kusikilizana, ila wewe usiwe mlevi kama wao (huu ni mfano tu)

O- onyesha mfano kwa vitendo. Kikawaida jamii na dunia nzima hupendelea kuona kiongozi anafanya nini ilo nao wafanye. Ndiyo maana lazima kiongozi awe mstari wa mbele kuhakikisha shughuli za kijamii au kitaifa zinaenda.

N- Nena kauli thabiti. Ni vyema zaidi kwa kiongozi kuwa na kauli thabiti, hii husaidia jamii kumwelewa, maana ulimi ni kiungo kiongozi ila huwakosesha wengi. Hivyo basi kiongozi anapaswa alinde ulimi wake hata, kama atachukizwa na watu wake.

G- Gawa madaraka kwa watu unao watawala. kiongozi anapo gawa madalaka kwa watu anao watawala husaidia kurahisisha shughuli za jamii. Ni ngumu kwa kiongozi kusimamia fedha, na hapo hapo akawalinda watu wake, huku akawa mshauri na kutatua changamoto kwa wakati mmoja. Hii ni ngumu, na haiwezekani. Kiongozi anapo gawa madaraka uongozi unakuwa rahisi Sana.

O- Ondoa uonevu,kwani katika jamii kuna tabaka mbili maarufu; wenye nguvu, na wanyonge, tabaka la wenye nguvu huwa linaonea sana wanyonge. Hivyo basi kiongozi, ni lazima aondoe uonevu ili pasije pakawa na chuki zitakazo leta migogoro katika uongozi wake.

Z- Zuia migogoro. Migogoro huja pale pande mbili zisipo elewana, hivyo ni muhimu kwa kiongozi kupatanisha ili kuongoza jamii iliyo na amani kwa lengo la maendeleo.

I- Inua maisha ya watu wako unao watawala, Hili jambo ni la lazima kwa kiongozi yeyote, kwani watu hukuchagua kwa lengo la kuwa jibu au matumaini katika maisha yao.Hivyo basi, jitaidi kadri uwezavyo maisha yao yainuke.

Sijapenda kuweka kasoro, ila nimependa kuonyeaha misingi ya kiongozi na uongozi wake yanavyopaswa kuwa. Kasoro zipo kwa sababu kukosea kupo na kusahihisha kupo pia. Kiongozi anapo kosea ni wajibu wake kuhakikisha anapasahihisha pale alipokosea kwanza kabla ya kuendelea na mengine, Kwenye jamii yangu huwa nasikia wakisema 'kheri mwisho mwema kuliko mwanzo mbaya'. asa ili neno kheri mwisho mwema naliona lina maana katika uongozi pale tu kiongozi anapokosea katika utendaji, anapswa asahihishe, ili mwisho uwe mwema, kwa maana kwamba jambo limetendeka vizuri japo kasoro zilikuwepo.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom