SoC03 Uongozi unaotakiwa na jamii

SoC03 Uongozi unaotakiwa na jamii

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 24, 2016
Posts
15
Reaction score
10
Create an image that showcases a group of people discussing matters of development and progre.png

Picha na Microsoft Designer

Uongozi ni sanaa ya kuwaongoza wengine ili kufikia lengo fulani. Ni mchakato wa kuhamasisha, kushirikisha, kuonyesha na kuongoza wengine kufikia mafanikio yanayokusudiwa.

Uongozi ni muhimu kwa kila aina ya jamii, kutoka kwa jamii hadi taifa, na mpaka mataifa makubwa yaliyoendelea. Uongozi ni nguzo kubwa ya kusaidia maendeleo endelevu.

Kwasababu hiyo, Tanzania siyo kisiwa ni taifa linalojitegemea nayo pia inahitaji uongozi mpya sasa na wa tofauti kulingana na mazingira ya sasa. Inahitaji viongozi ambao ni waadilifu, wenye uwezo na wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko.

Inahitaji viongozi ambao wataisaidia kujenga nchi yenye ustawi na usawa. Na kuwafanya wananchi kuwa wamoja katika kuleta maendeleo ya kweli na endelevu.

Sisemi kwamba viongozi wa naona hiyo hawawahi kutokea Tanzania, bali naweka msisitizo kuwa basi waendelee kutokea, na kuwa bora Zaidi, maana nyakati hizi kuna nyenzo mbalimbali za kiutandawazi na kidigitali zipo katika matumizi na wanaweza kuzitumia kuboresha kazi zao za kuongoza.

Aliwahi kuwapo mwasisi wa taifa, akiitwa sasa Baba wa taifa la Tanzania, aliwahi kusema katika miaka ya nyuma ya utawala wake, Aisema, ili tuendelee, tunahitaji mambo manne, mambo hayo ni Watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora. Nimeamua kuchukua kipengee chake kimoja tu cha uongozi bora.

Kauli hii Baba wa taifa aliisema mwaka 1971, nchi ikiwa na miaka kumi tuu tangia ipate uhuru wake, kutoka katika mikono wa wakoloni. Ikimaanisha kuwa alikuwa na dhamira thabiti ya kuyatekeleza hayo yote. Na la msingi Zaidi uongozi bora.

Maana hayo mambo mengie matatu yalikuwepo na yapo tayari. Hili la nne ndiyo linalopaswa kuimarishwa. Kama yeye alivyoongoza kwa mfano, kila mmoja ni shahidi wa hayo yote.

Aliongoza kwa kufuata misingi ya kuijamaa, akafanikiwa kuanzisha viwanda katika utawala wake. Na vilifanya vizuri mpaka mwishoni mwa utawala wake.

Kwa kuanza na suala la watu, Tanzania imebarikiwa kuwa na watu wengi takribani sasa 61,741,120. Pia,imebarikiwa kuwa na ardhi kubwa tena yenye rutuba na madini ya kutosha katika Maeneo mengi ya Tanzania. Ina eneo la kilometa za mraba 945,087.

Screenshot (8).png

Picha ni eneo lote la Tanzania.

Kwa upande wa siasa sitaongelea sana maana siyo mtalaamu wa mambo hayo.


Picha ni idadi ya watu Tanzania.
Lakini naweza kukiri kwamba kumekuwa na siasa ya kuridhisha ya mfumo wa vyama vingi na kumekuwa na tabia ya kubadilishana madaraka kwa chaguzi za Amani na usalama.

Kama jamii kasoro ndogo ndogo haziwezi kukosekana, ila lengo la Makala hii ni kuibua mjadala juu ya uongozi utakaoifaa Tanzania ijayo. Nasema Tanzania ijayo kwa maana ya uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

Uongozi wa Tanzania ijayo unapaswa kujikita na kutegemea maadili na uadilifu, uaminifu na haki. Viongozi wake wanapaswa kuwa wazi na wawazi, na wanapaswa kuwajibika kwa matendo yao.

Wanapaswa kuwa na uwezo wa kifikra wa kufanya maamuzi magumu, hata wakati wa Changamoto nzito.

Kuwa wawazi kwa maana ya kujulikana mali zao wanazomiliki na kutenganisha maslahi yao binafsi na maslahi ya jamii au taifa wanaloliongoza. Waongoze kwa vitendo zaida na siyo maneno na kila jambo lifanyike kwa kuzingatia maslahi ya wengi.

Kadhalika, unapaswa kutegemea ubunifu na uvumbuzi. Viongozi wa Tanzania wanapaswa kuwa na uwezo wa kuona fursa mpya na kufikiria nje ya boksi. Wanapaswa kuwa tayari kujaribu mambo mapya na kuchukua hatua na kujitoa mhanga kwa maslahi ya wanaowaongoza.

Lakini siyo kuona fursa tu, bali kuweza kuzitafsiri hizo fursa ili Watanzania wote waweze kuzipata, na hata walioko vijijini kabisa. Hiyo itasaidia hili ninaloliona sasa viongozi wengi wanasema watu wachangamke fursa.

Lakini hawesemi katika tafsiri halisi ni fursa zipi? Na zinachangamkiwa kwa njia zipi? Wananchi wanabakia njia panda. Hivi karibuni kuna kiongozi wa wizara Fulani alisema, wananchi wachangamkie fursa za kidigitali!

Bila kusema ni fursa zipi zinafaa kwa wananchi na jinsi gani ya kuzifanya na kujipatia vipato. Kwa walio mijini na hata walio vijijini. Haitoshi kusema tu kuna fursa, itoshe kusema kuna fursa zifuatazo na zinachangamkiwa hivi.

Kwa sasa, Tanzania inahitaji viongozi ambao ni waadilifu, wenye uwezo na wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko, kama nivyokwisha kusema awali. Inahitaji viongozi ambao watasaidia kujenga nchi yenye ustawi na usawa.

Ili kuondoa matabaka ya walionacho na wasionacho. Matabaka ya masikini na matajiri, ya wasomi na wasiosoma nakadhalika. Na narudia kusema siyo kwamba hatuna watu kama hao bali ni msisitizo wa kufanya wajitambue na wawe bora Zaidi maana kwasasa dunia ina nyenzo nyingi za kiuongozi.

Katika zama hizo za kiutandanawazi na kidigitali. Kwa msemo wa watu dunia imekuwa kijiji kimoja. Basi viongozi wa Tanzania wanapaswa kuchangamkia fursa ya kuwa kijiji kimoja na nchi kubwa, maendeleo yao ya kiuongozi yawe ya umma wa Tanzania.

Hapa kuna baadhi ya sifa muhimu za uongozi ambazo viongozi wa Tanzania wanapaswa kuwa nazo, nimeona si vibaya tuziangalie kwa pamoja na huu ni mjadala unaweza kutoa maoni yako.

Na kuchangia Zaidi juu ya uongozi unaotakiwa hapa nchini. Kwa kuandika maoni yako katika eneo la maoni, chini kabisa ya Makala hii.

Hebu tuanze na:

Uadilifu:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa waadilifu na wenye uaminifu. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu, hata wakati wa hali tete inayowazunguka.



Uwezo wa kuongoza:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa na uwezo wa kuona fursa mpya na kufikiria nje ya boksi. Wanapaswa kuwa tayari kujaribu mambo mapya na kuchukua hatua sitahiki hata kujitoa mhanga kwa maslahi ya umma.

Uwazi:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa wazi na wawazi katika mambo yao yote. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwasiliana na watu kwa ufanisi na kuwashirikisha katika maamuzi.

Haki:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa wa haki na wenye huruma. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwakilisha maslahi yote ya umma.



Ufanisi:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza maamuzi kwa ufanisi na kwa ubunifu mkubwa.

Ushawishi:

Viongozi wetu wanapaswa kuwa na uwezo wa kushawishi wengine kufuata maono yao. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwahamasisha na kuwatia moyo wengine.

Ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli nay a uhakika Zaidi.

Nimeanzisha tu mjadala wa uongozi wa Tanzania uvyopaswa kuwa, nimesema unapaswa kutegemea baadhi ya maadili haya niliyoyataja hapo juu ili kuunda nchi bora kwa kila mtu.

Kwa mjadala au nyongeza tuonane katika eneo la maoni hapo chini. Karibuni!
 

Attachments

  • Screenshot (7).png
    Screenshot (7).png
    91.7 KB · Views: 3
Upvote 0
Back
Top Bottom