Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Alisema na kuonesha picha pamoja na video na kuwa kuna majani yameota ovyo Chuoni hapo na hakuna Vimbweta kwaajili ya Wanafunzi kusomea.
Kusoma zaidi bofya hapa ~ Chuo Kikuu Huria - Singida kiboreshe mazingira yake, ni kama vile kimetelekezwa
MAJIBU YA CHUO KIKUU HURIA
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania - OUT), Adam Namamba amekiri uwepo wa hali hiyo na kusema wanafanyia kazi ushauri huo.
Anasema: Eneo hilo lina asili ya majimaji kwa kuwa lipo karibu na ziwa, hivyo kuna asili ya unyevunyevu.
Mvua ikinyesha ni rahisi maji kutuama au kuwa na unyevunyevu.
Tumeshawasilisha hiyo changamoto kwa Mkurugenzi wa Mipango ameeleza kuna ukarabati tunaenda kuufanya hivi karibuni.
Ni sehemu ambayo viongozi wengi wa taasisi wanapita kwa sana katika chuo hicho, tuna program tunaiendesha kwa vijana wanaosoma masomo ya Sanyansi na yanahusisha ana kwa ana.
Hilo eneo tulipewa na Serikali, tukafanya ukarabati wa awali lakini tunataka kurekebisha madhara ya eneo hilo.
Pia soma:
~ Chuo Kikuu Huria - Singida kiboreshe mazingira yake, ni kama vile kimetelekezwa
~ Chuo Kikuu Huria Tanzania lipeni Waajiriwa wenu pesa zao za kujikimu, mtawaua njaa na kuwafedhehesha mtaani
~ Wanafunzi mnaotaraji kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) nawatahadharisha tafuteni chuo kingine