ADOLPH EMMANUEL
Member
- Sep 22, 2020
- 7
- 1
Uongozi wa Edeni
Rushwa kama upepo wa kusi, inavuma kwa kasi,
Inakita mizizi kila kona, inaibomoa Edeni,
Kila mtaa kila kijiji, maendeleo yanabuma,
Watu wanasaga meno na kulia, haki haipatikani.
Uzembe kazini unatisha, unaenea kama magugu,
Wafanyakazi wanalala, huduma zinakuwa mbovu,
Ufanisi unakuwa ndoto, maendeleo yanakuwa hewa,
Edeni inadorora, wabarikiwa na wadhambi wamekaa.
Madaraka yamepitiliza, wabarikiwa wanajivuna,
Wanaishi peponi, wadhambi wanaamia jehanam,
Hakuna anayesikia sauti, za swala wa ngorongoro,
Madaraka yamekuwa fahari, kama mali ya familia.
Manung'uniko yanajaa, kwenye ofisi za umma,
Watu wanapanga foleni, wakihangaika kupata huduma,
Huduma zinakuwa duni, hakuna anayejali,
Wabarikiwa wanakula, wadhambi wanakufa njaa.
Wadhambi wanadhalilika, furaha kwao wabarikiwa,
Wanaonesha utu wao, kwa haki kuiminya,
Wadhambi wapo gizani, wakingojea nuru.
Ni lini watasikia, nakufungua macho yao?
Wakati umefika, wadhambi kuokoka,
Kuwajibika kwa dhati, na si kwa njaa,
Rushwa kuiweka kando, na haki kuitafuta,
Edeni kutolewa gizani, na kuingia nuruni.
Mifumo imara ijengwe, ili iweze kusimamia,
Uadilifu kazini, uzembe usivumilike,
Wafanyakazi wenye bidii, wachukue nafasi,
Ili huduma ziboreke, na maendeleo yatujie.
Wabarikiwa tafadhali elewa, nyie ni watumishi,
Si watawala wa kupokea, bali wa kutoa,
Ongozeni kwa hekima, na si kwa nguvu,
Tangulizeni maslahi ya umma, si ya familia zenu.
Mbarikiwa ni yule anayejua njia, kuiendea nakuionesha,
Hekima ya Maxwell, iwaongoze wabarikiwa,
Wasiwe wa kulala, bali wa kujitoa kwa dhati,
Kwani maendeleo ni ya wote, si ya wachache tu.
Lakini wabarikiwa wa Edeni, hawana masikio,
Hawana macho ya kuona, mustakabali wa Edeni,
Wanajifungia ndani, wakila na kushiba,
Wakisahau wajibu wao, kwa kuudhuria fungate.

Na Adolph Emmanuel
Attachments
Upvote
0