Uongozi wa klabu ya Simba SC jitahadhalini, Ajibu wa Yanga anawarubuni wachezaji wa Simba

Uongozi wa klabu ya Simba SC jitahadhalini, Ajibu wa Yanga anawarubuni wachezaji wa Simba

kimarabucha

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
791
Reaction score
621
UONGOZI wa Klabu ya Simba mnapaswa kuwa makini na WACHEZAJI wenu kwani Klabu ya Yanga ina mtumia Mchezaji wake Ibrahimu Ajibu kuwarubuni WACHEZAJI wenu wajiunge na Yanga.
 
UONGOZI wa Klabu ya Simba mnapaswa kuwa makini na WACHEZAJI wenu kwani Klabu ya Yanga ina mtumia Mchezaji wake Ibrahimu Ajibu kuwarubuni WACHEZAJI wenu wajiunge na Yanga.
Umechanganyikiwa wewe, inamaana wachezaji wa Simba hawajitambui kiasi cha kuweza kurubuniwa na Ajibu? Uwatake radhi wachezaji
 
HAWAJIFUNZI TU KUNA WAKATI YANGA ILIKUWA INAITWA SIMBA B WAKAANZA KULALAMIKA KUWA MAMLUKI NI WENGI,WALIMCHUKUA YONDANI,KASEJA,OKWI,BARTHEZ,DEO MUNISHI TUKAWA TUNAWAFUNGA KILA MECHI WAKASEMA WANAHUJUMIWA.MSIVYO NA KUMBUKUMBU MNATAKA KURUDIA KOSA!
 
Sasa kama Ajibu alikuwa na maisha magum msimbazi lakin kajiunga Yanga anafurahia maisha je inahitaji nini tena ili wachezaji wa Simba wapende kuchezea Yanga?

MAISHA MAZURI NDIO HAYA
yanga-moro.png
 
HAWAJIFUNZI TU KUNA WAKATI YANGA ILIKUWA INAITWA SIMBA B WAKAANZA KULALAMIKA KUWA MAMLUKI NI WENGI,WALIMCHUKUA YONDANI,KASEJA,OKWI,BARTHEZ,DEO MUNISHI TUKAWA TUNAWAFUNGA KILA MECHI WAKASEMA WANAHUJUMIWA.MSIVYO NA KUMBUKUMBU MNATAKA KURUDIA KOSA!
mkuu muda utasema tena

wamesahau tena
 
Ni uzwazwa kusema wachezaji wa tanzania wana Maisha mazuri. Maisha gani haya. Nimeamini Didi watanzania kufikiri kwetu kuna matatizo. Hv Ajibu kupewa lile gari linalobwia mafuta km jini mnasema amepatia Maisha. Ajibu au wachezaji wa tanzania kupewa mikataba ya 60 million mnaona wamepatia Maisha. Inasikitisha Sana kushabikia na kubishana mchezaji Kama Ajibu at mkude achezee yanga au simba. Nilidhani tutawahimiza waenda waongeze juhudi waende ulaya. Ndugu zangu watanzania Tuache ushabiki wa kijinga. Dunia imebadilika. Wachezaji wa magharibi au Brazil wanazungumzia mabilon sisi tunashabikia milion50 na gari la hovyo la Ajibu eti ameyakwaa Maisha. Didi watanzania Nani ameturoga.
 
baadaye msilalamike tukiwafunga kuwa mamluki ya samba yanawafungisha.mbona wasahaulifu sana nyie
Mchezaji yeyote anahitaji nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza! Siku hizi mpira wa mahaba umekwisha! Wachezaji kutoka na kuingia hizi timu walianza zamani! Kina Steven Names, Lunyamila, Kipese, Kizota, Chinga one, Yusufu Macho na wengineo walitoka Yanga enzi hizo wakaenda Simba! Itakuwa ajabu gani Mkude, Ndemla au Mo kwenda Yanga! Nyie si mnaye Niyonzima? unajua alikuwa timu gani kabla ya kwenda simba! 'This is football brother' yote yanawezekana! Kama mchezaji hatumiki ipasavyo mwacheni aondoke! Hizo porojo za sijui hujuma zinatoka kwa mashabiki maandazi kama nyie!
 
Na huyu Ajibu kutwa kucha na wachezaji wa Simba SC kwani Ndala huko hakukaliki?
 
Rage hakukosea kuwaita 'mbumbumbu' maana hata hamueleweki,mnasema Yanga kuna njaa wachezaji hawalipwi alafu mnalia kua wachezaji wanarubuniwa waende Yanga ivi kweli mchezaji anaweza kufuata kukopwa mshahara uyo Ajibu alirubuniwa na nani kuja Yanga.
Mbumbumbu acheni visingizo safari ni lazima hili kombe tugombanie wote upuuzi wa kututegea tushachoka kila mwaka tunabeba sisi tu naona mnaanza visingizio mapema kisa uoga wa kua mabingwa na sisi tunataka changamoto jamani kwani hii ligi ni Yanga tu.
 
Back
Top Bottom