kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Sisi tunatoa tu maoni yetu hatujui yataisaidiaje nchi yetu leo na kesho, lakini ni heri kusema kuliko kunyamaza.
Nchi yenye watu zaidi ya 60m hawakosekani watu safi wenye sifa ya kuongoza wenzao kupata maendeleo. Kama ukiwekwa utaratibu na mfumo mzuri wa kuwapata viongozi bora unaofanana na mfumo wa kuwapata wachezaji mpira wazuri kwenye timu taifa letu litasonga mbele haraka. Kwenye mpira hata Rais wa timu au mmiliki wa timu hawezi kumsajili mtoto wake acheze mpira nafasi ya golikipa kama mtoto huyo hana sifa ya kuwa golikipa.
Taifa letu linadumaa kwasababu teuzi nhyingi za viongozi nchini ni za kulipana hisani na kuenziana bila kuzingatia vigezo vya sifa. Mfano, mimi sina uhakika kama watu kama Mwl. Nyerere, Mzee karume, Kawawa, Mzee Malecela, Mkapa, Kikwete, Warioba, Sokoine, Magufuli, nk walikuwa na watoto nma wajukuu ambao wana sifa (tabia, karama, uadilifu na uzalendo) kama wazazi wao kiasi cha kustahili lazima wawe viongozi wa nchi hii.
Tutafute mfumo wa uteuzi ambao utaruhusu watu wote wenge sifa wawe na fursa sawa na kuwa wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, wakurugenzi na nafasi nyingine za umma kuliko ilivyo sasa. Sifa na juhudi binafsi ya mtu iwe ndiyo kigezo pekee cha kuwa Mkuu wa Mkoa.