Uongozi wa Shabiby Bus Terminal waboresha vyoo vya Kituo cha Shabiby Bus Terminal - Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
​
Kampuni ya mabasi Shabbiy Bus imefanya maboresho ya vyoo katika Kituo Kikuu cha Upakiaji Abiria jijini Dodoma, ambavyo awali vilikuwa katika hali ya uchakavu, hatua inayolenga kuboresha mazingira na ustawi wa wasafiri.

Mbali na marekebisho hayo, kampuni hiyo inaendelea na ukarabati mkubwa wa kituo hicho ili kuhakikisha abiria wanapata huduma bora na za kisasa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni hiyo, ujenzi wa jengo kubwa la kupumzikia abiria pamoja na mgahawa mkubwa wa chakula unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza faraja, usalama na kurahisisha safari kwa maelfu ya abiria wanaotumia kituo hicho kila siku.

Hali ya vyoo ilivyokuwa awali ~ Hali ya vyoo Ofisi ya Mabasi ya Shabiby – Dodoma sio salama kwa Watumiaji

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.



​
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…