Uongozi wa Simba SC tafadhali kama Matola ni Kocha Msaidizi wa kudumu, mtueleze sisi mashabiki

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Sina tatizo na Juma Mgunda (Guardiola Mnene) kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC kwani natambua uwezo wake ila tatizo langu ni kwanini Matola Yeye haondoshwi Simba SC kama wanavyoondoshwa makocha wengine?

Uongozi wa Simba SC tafadhalini sana kama wenyewe kisirisiri kutokana na upumbavu wenu usiovumilika mmeamua Matola awe na Cheo cha Kocha wa kudumu (Milele Ijayo) ndani ya Simba SC mtuambie Sisi mashabiki ili tujue moja na tuache kila mara kupaza Sauti zetu za Hasira kuwa aondoshwe.

Kaka yangu Kocha Juma Mgunda jiandae kupigwa Zengwe na Matola, Kufitiniwa nae kwa Uongozi na kubwa zaidi atazungumza na Marafiki zake (Wachezaji Waandamizi) wa Simba SC ili wafungishe (waharibu) kwa makusudi ili ufukuzwe na apewe Yeye Timu na pia aendelee kuaminika na Uongozi wa Juu ambao wengiwWao ameshawafunika akili zao huko Kwao kigoma na hawana kauli juu yake.
 
Unaonaje tukupe mikoba ya timu wewe ndg Popoma?.
Mwenzako ndo mkuu wa mipingo idara ya kuroga
 
Huyo ni mwekezaji mwenzao hapo klabuni kwenu,hamna habari 🚶🚶🚶🚶🚶
 
Tukupe timu uifundishe ewe popoma mwandamizi.
 
Kimwaga udugu wewe uko Yanga mbona unaumia sana na mambo ya Simba? Tafadhali tuache na Simba yetu na wewe itumikie GSM yako kituo cha kazi kikiwa hapo utopoloni.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kuanzia September 1, 2022, Manara ameitaja Simba mara 26 na Yanga mara 1- Na wewe kwa siku unaianzishia Simba thread 6 na Yanga thread 0. Tofauti ya wewe na Manara ni wingi wa kinyesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…