Uongozi wa Simba SC ule Upuuzi uliofanyika jana nje ya Uwanja wa Taifa usirudiwe tena tafadhali kwani Utatugharimu na kuja Kujutia

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Labda niwaambieni tu Uongozi wa Simba SC kuwa Rais mpya wa CAF Bwana Patrice Motsepe haungwi (hakuungwa) Mkono na Rais wa TFF Bwana Wallace Karia ambaye inajulikana alikuwa ni Mtu wa aliyekuwa Rais wa CAF Bwana Ahmad Ahmad.

Hivyo kwa hili Tanzania (hasa TFF) inatakiwa kuwa makini nae sana huyu Rais mpya wa CAF Bwana Motsepe kwani ameshaanza kuonyesha kuwa ana Kisununu (Kinyongo) na Rais wa TFF Bwana Karia na Tanzania kwa ujumla.

Pia Uongozi wa Simba SC tambueni ya kwamba huyu Rais mpya wa CAF Bwana Patrice Motsepe na aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bwana Senzo Mbatha Mazingisa ni Marafiki wakubwa, Washirika, walishakuwa pamoja katika Kamati kadhaa za Mashindano makubwa ya dunia (hasa ya AFCON na FIFA World Cup) ambayo nchi yao ilishaandaa lakini pia kumbukeni Wote hawa ni Raia wa Afrika Kusini wanakotoka.

Simba SC ama kwa kutokulijua hili au kulijua ila mmefanya Kusudi tu Juzi mliagizwa na Mamlaka za CAF kuwa Mechi yenu ya Jana dhidi ya El Merreikh Uwanja wa Mkapa mcheze bila Mashabiki na isitoshe hata nje ya Uwanja hakutakiwa Kuonekana Mtu yoyote ikiwa kama njia za Kuzuia Maambukizi ya Corona (Covid-19)

Cha Kushangaza na hata Mimi All - Rounder nimesikitika mno jana kwa Kiburi chetu cha Upumbavu na Ujeuri usio wa maana Sisi (Simba SC) tukawaona CAF chini ya Rais mpya Bwana Motsepe haina Akili na tunajua zaidi yao na Kukubali kutoruhusu Mashabiki kuingia (zaidi tu ya wale 200 walioruhusiwa) huku nje ya Uwanja tukaruhusu Mashabiki kuwepo kwa wingi tena Wakichagiza kwa Nyimbo zao huku wakipiga Kelele nyingi tu.

Mpaka hapa tu tayari tumeshaonyesha Dharau kwa CAF chini yake Rais wake mpya na Adui yetu Bwana Motsepe hivyo tujiandae mapema Kisaikolojia. Kama Ripoti ya Mtathmini wa Mechi inayotakiwa kwenda CAF akiliweka na hili Simba SC tutegemee Adhabu Kali au hata kuamriwa Kucheza Mechi zetu zilizobaki au nyinginezo katika Uwanja mwingine na wa nchi nyingine (siyo Tanzania)

Nanyi Mashabiki wa Simba SC hebu acheni Upuuzi na Kiburi cha Kijinga. Tujifunze Ustaarabu wa hasa kusikia Maelekezo ya Mamlaka za Mpira CAF. Tutakuja Kuigharimu Timu na hatimaye hata Ndoto zetu za Kufika mbali katika Michuano hii mikubwa Barani Afrika ikapotea na kuanza Kulaumiana na Kuwasingizia Mahasimu wetu wakubwa Yanga SC kuwa wamechangia Kutuhujumu (Kutusagia Kunguni) katika Kikombe.

Kwahiyo Mashabiki wa Simba SC ndiyo wanapenda Mpira na wana Uchungu zaidi na Timu yao kiasi kwamba hawawezi Kubakia Nyumbani na Kutii Mamlaka za CAF? Simba SC ina Mashabiki wenye Uchungu na Mapenzi kwa Timu yao kuliko wa AS Vita Club, Al Ahly, Mamelodi Sundowns na TP Mazembe ambao Wao walitii AMRI za Mamlaka ya CAF na hakuna aliyeenda Uwanjani au hata Kusogelea vilipo Viwanja vyao wakati wa Mechi zao.

Najua wanasimba Wenzangu Ukweli wangu huu Mchungu Kwenu unaweza Ukawakwaza ila All - Rounder sijazoea Unafiki au Kuipendelea Klabu yangu ya Simba SC hata kama inafanya vizuri ndani na nje ya nchi. Mimi ni Muumini Mkuu wa Nidhamu n Utaratibu na huwa nachukia mno Ujinga na Upumbavu. Tuvumiliane ila tubadilike kwa Faida kubwa ya Timu yetu Simba SC na nchi yetu Tanzania.

Kila Ia Kheri.

Wenu All - Rounder ( alias ) Brainiac.
 
Tafadhali naitwa All - Rounder na siitwi huyo uliyemtaja na siyo Mini pia 100% sawa Ndugu?
sawa mkuu haina shida...nimekuelewa na sitakufananisha tena..ila mkuu napenda kufahamu maana ya BRAINIAC na ALIAS....
 
CAF walisema tusiingie uwanjani hawakusema tusikae nje ya uwanja
Una uhakika? Wapinzani wetu tuliocheza nao Kwao Wao walipoamriwa kama tulivyoamriwa Sisi Jana uliona Kiumbe yoyote ( Mashabiki wao ) wowote nje ya Uwanja kama walivyofanya wa Simba SC jana? Tuacheni Upumbavu, Kiburi na Ushamba tafadhali.
 
sawa mkuu haina shida...nimekuelewa na sitakufananisha tena..ila mkuu napenda kufahamu maana ya BRAINIAC na ALIAS....
Bahati nzuri maneno yote Tajwa ya ALIAS ba good BRAINIAC yapo katika Kamusi zote Kubwa za Webster, Thesaurus na Oxford hivyo ni Jukumu lako kwenda huko ili uyaelewe ila kama Wewe ni JF Great Thinker halafu hayo maneno mawili huyajui unanipa Mashaka mno kama Wewe ni Intellectual na Wordsmith hasa.

Punguza / Acha Unafiki nitakudharau.
 
Una uhakika? Wapinzani wetu tuliocheza nao Kwao Wao walipoamriwa kama tulivyoamriwa Sisi Jana uliona Kiumbe yoyote ( Mashabiki wao ) wowote nje ya Uwanja kama walivyofanya wa Simba SC jana? Tuacheni Upumbavu, Kiburi na Ushamba tafadhali.
Sio kila walichookifanya wao nasisi tukifanye

Tulivoenda Nigeria kucheza na plateu walizuia kurusha mpira live, lakini hiyo haikumaanisha na wao wakija huku tufanye hivyo hivyo
 
Mkuu..unafiki umetoka wapi tena?...we kunidharau mimi hainipunguzii chochote...hadi kukuuliza wewe unazani sikujua kama kuna dictionary..acha mawenge mkuu...punguza stress na mipayuko isiyo na maana.. Naomba uendelee kunidharau.
 
Kwani walienda kufanya nini nje ya uwanja? kulikua na giant screen wanaangalia mechi live au walienda tu kurundikana nje ya uwanja?
 
CAF imeagiza mashabiki wasiingie. Na Simba imetimiza maagizo.

Hao waliorundikana nje ni ushahidi tosha kuwa wamezuiwa wasiingie uwanjani. Kukaa nje ya uwanja na kucheki soka kwenye TV hakuna aliyekataza.
 
Huyu rais wa caf dawa ni kuanza kumshambulia mitandaoni tofauti zake na Karia asituingize, hawa wasouth tuliwasaidia sana ili wawe huru lakini hawanaga shukrani heri tungewaacha wakaendelea kuwa chini ya makaburu
 
Sio kila walichookifanya wao nasisi tukifanye

Tulivoenda Nigeria kucheza na plateu walizuia kurusha mpira live, lakini hiyo haikumaanisha na wao wakija huku tufanye hivyo hivyo
Acha kupotosha mkuu, mechi ya nigeria hawakuzuia kurusha live bali dau lililotolewa na media halikufika kwa wenye mechi walilokuwa wanahitaji
 
Nimeliangalia tukio la Jana kwa umakini mkubwa. Nahisi kitu. Lakini si kwa sababu ya senzo na motsepe kuwa marafiki wala Karia kutokuwa na ukaribu na motsepe. Ni kwa sababu ilionekana kama wale mashabiki walikuwa kwenye aina fulani ya mgomo kupingana na maamuzi halali ya CAF. Sasa wanaweza kumtafuta namna na kujiridhisha kuwa Simba walikiuka agizo kwa makusudi.
 
Kuna wakati tujifunze kuelwa jambo kwanza ,sehemu ya taarifa inasema ndani ya uwanja, kama ni hivyo hata sokoni wasiwepo mashabiki wa simba!
 
Nadhani hii ni mitazamo yako na matamanio yako.....kwenye ujumbe wa CAF hakukuwa na hilo la kutokutaka mashabiki wasikae nje ya uwanja.......

This is Simba.....
 
Kwa hiyo Simba ina jeshi la polisi kuingilia Uhuru wa watu nje ya uwanja?
 
Halafu huyu Senzo anaweza kuwa kirusi hatari sana.

Je anastahili kupata vibali vya kazi?Maana hata huko utopoloni ameshawachanganya tayari ila kwa vile ana akili kuliko wao,hawatamuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…