Bado kuna tatizo la kuwaamini sana, Wazungu.
Napenda kuwapongeza Yanga fc kwa kumchagua kocha mkuu Zahera.
Kwakweli ni kocha bora kabisa na hadi kachaguliwa na wadau wa michezo kuwa kocha bora wa mwezi.
Zahera kaibadili sana Yanga na ni kocha anaye ujua mpira wa Afrika mashariki na kati. Mpira unaochezwa ki-ndondo style zaidi.
Ikiiangalia yanga unaona wazi kabisa ina mipango ya kubeba ubingwa wa TPL. Yanga imabadilika sana.
Kama sio kuihofia Simba, mechi iliyopita wangeweza kushinda kabisa, tatizo waliingia na hofu na kuanza kulinda goli.
Kwa mfumo wa huyo mzungu wa Simba, Simba isahau kutetea ubingwa wake msimu huu.
Kama viongozi wangemwamini Juma na kumletea Matola kama msaidizi wake moto ungewaka hapo Msimbazi.
Kama wanamtaka mzungu basi wamwondoe Juma ili huyo mtashi aje na msaidizi wake kama anavyotaka kocha mkuu ili waharibu kabisa.
Tujifunze kuwaamini makocha wetu wa Kiafrika kama Yanga na TFF walivyofanya.