Uongozi wa Simba wakiri Mgogoro wa Makocha

Uongozi wa Simba wakiri Mgogoro wa Makocha

Kizibo255

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
515
Reaction score
376
Kaimu Rais wa Wekundu wa Msimbazi Salim Abdallah (Try Again) amethibitisha kuwa makocha hao wana mgogoro na imeshindikana kupata suluhu
IMG-20181006-WA0018.jpg
 
Fyekelea mbalii msaidizi, mwache kocha mkuu atafute wa kumsaidia yeye mwenyewe, siku zote msaidizi ni msaidizi sasa ukakasi wa nini kumfyeka!???😂😂😂
 
Kwa ninavyoijua hii timu ya mambumbumbu kocha mkuu atafyekelewa mbali kimya kimya atabakishwa kocha msaidizi kisha ataletwa kocha mkuu mwingine, uyo masoud ni kocha msaidizi wa kudumu hapo mbumbumbu fc
 
Haya ma migogoro ndio siyapendagi kabisa
hakunaga msimu ukaisha bila kusikia migogoro kwenye timu zetu Bongo
kulikoni
 
Sukumia mbali aliyeishusha kiwango Simba.
Tunahitaji kuiona Simba ikicheza vizuri na kwa mafanikio na sio kumwona Kocha fulani.
Viongozi lazima mtafakari nani bora kati ya hao wawili.
Fukuzeni huyo mbovu wala msiogope lawama.
 
Haya ma migogoro ndio siyapendagi kabisa
hakunaga msimu ukaisha bila kusikia migogoro kwenye timu zetu Bongo
kulikoni
Tatizo hizi timu kubwa za bongo ni miradi ya watu kupigia pesa.Mfano kwenye migogoro kama hii watu ndipo hupiga hela (fukuza kocha leta kocha 10% yangu)
 
Tatizo hizi timu kubwa za bongo ni miradi ya watu kupigia pesa.Mfano kwenye migogoro kama hii watu ndipo hupiga hela (fukuza kocha leta kocha 10% yangu)
Safari bado ipo
 
Fukuzia mbali mzungu
Bado kuna tatizo la kuwaamini sana, Wazungu.
Napenda kuwapongeza Yanga fc kwa kumchagua kocha mkuu Zahera.
Kwakweli ni kocha bora kabisa na hadi kachaguliwa na wadau wa michezo kuwa kocha bora wa mwezi.
Zahera kaibadili sana Yanga na ni kocha anaye ujua mpira wa Afrika mashariki na kati. Mpira unaochezwa ki-ndondo style zaidi.
Ikiiangalia yanga unaona wazi kabisa ina mipango ya kubeba ubingwa wa TPL. Yanga imabadilika sana.
Kama sio kuihofia Simba, mechi iliyopita wangeweza kushinda kabisa, tatizo waliingia na hofu na kuanza kulinda goli.
Kwa mfumo wa huyo mzungu wa Simba, Simba isahau kutetea ubingwa wake msimu huu.
Kama viongozi wangemwamini Juma na kumletea Matola kama msaidizi wake moto ungewaka hapo Msimbazi.
Kama wanamtaka mzungu basi wamwondoe Juma ili huyo mtashi aje na msaidizi wake kama anavyotaka kocha mkuu ili waharibu kabisa.
Tujifunze kuwaamini makocha wetu wa Kiafrika kama Yanga na TFF walivyofanya.
 
Huyo Masoud ni kirusi kwenye timu yenu 'simba'! Haiwezekani makocha 03 washindwe kufanya kazi na yeye! Fyekeleeni mbali huyo masudi Juma!
 
Huyo Masoud ni kirusi kwenye timu yenu 'simba'! Haiwezekani makocha 03 washindwe kufanya kazi na yeye! Fyekeleeni mbali huyo masudi Juma!
Sio kweli.
Kocha Amog alimaliza mkataba wake, na viongozi walishindwa kumwongezea mkataba mwingine baada ya kuifundisha Simba kwa miaka mitatu bila kuipatia Ushindi wa Ligi iliyoitwa VPL.
Lechante alisaini mkataba wa kuinoa Simba kwa muda wa miezi sita tu. Uongozi haukushawishika kumwongezea mkataba mwingine.
Huyu Aussein wa sasa anataka amlete kocha aliyemchagua yeye ili awe msaidizi wake. Masudi hakumchagua yeye, hivyo hataki kifanya naye kazi.
Ile mechi na Yanga alimweka Juma ktk benchi lake la ufundi kwakuwa aliogopa endapo Simba ingefungwa mashabiki wa Simba wange mfanyia fujo kali sana.
Huenda huyo kocha ana CV kubwa kuliko Juma.
Lakini ukweli unabaki palepale kuwa Juma ni Kocha bora kuliko Aussein.
 
Tatizo ni msaidizi anataka nafasi ya Bosi wake, ndo anatumia wafuasi wake kuharibu mambo. Bosi naye kasema hamtaki awe msaidizi wake, keshaona hatari ya kibarua chake kisa nafasi aliyopo.


Massudi aache uzuzu, anaihujumu timu kisa tamaa zake za kutaka kuwa kocha mkuu
 
Tatizo ni msaidizi anataka nafasi ya Bosi wake, ndo anatumia wafuasi wake kuharibu mambo. Bosi naye kasema hamtaki awe msaidizi wake, keshaona hatari ya kibarua chake kisa nafasi aliyopo.


Massudi aache uzuzu, anaihujumu timu kisa tamaa zake za kutaka kuwa kocha mkuu
Sina hii habari,
Ninavyojua kuna kutofautiana katika Falsafa ya kufundisha mpira kati ya Kocha mkuu Aussein na Masudi.
Angalia kote ulaya, Kocha mkuu huwa anakuja na kocha wake msaidizi ili waendane kiuwajibikaji.
Kocha Maurinyo wa Manchesta United alilazimika kumfukuza kocha msaidizi aliyemkuta, Rayn Gigs ili kuilinda falsafa yake ya ufundishaji.
Hapa waliokosea ni Viongozi wa Simba kwa kumlazimisha Aussein afanye kazi na Masudi ambaye kimpira hawajuani.
Kwa mfano Masudi anaweza kuipendekeza First Eleven ya Simba ambayo Aussein haitaki na vitu kama hivyo, na kupelekea kutoelewana kimipango.
Aussein yuko sahihi kabisa, yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuteua kocha msaidizi na sio kuletewa, ukizingatia lawama zote za timu kufanya vibaya atapelekewa yeye.
Mashabiki nao wamechangia kwa kuanza kumponda Aussein mapema na kumsifia Masudi, jambo ambalo lilimwudhi kocha mkuu kwa kusikia harufu ya kuhatarisha ajira yake.
 
Back
Top Bottom