KERO Uongozi wa Stendi ya Buzuruga - Mwanza uweke vifaa vya kuwekea uchafu

KERO Uongozi wa Stendi ya Buzuruga - Mwanza uweke vifaa vya kuwekea uchafu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Stand ya Buzuruga iliyopo Wilaya wa Ilemela Mkoani Mwanza ina changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa vya kuwekea uchafu jambo linalosababisha Wadau wa stendi hiyo kumwaga uchafu chini ikifika usiku, kabla ya kuzolewa kesho yake asubuhi.

Licha ya uzuri na usafi wa stendi hiyo ya daladala ila ukosefu wa vifaa vya kuwekea uchafu unachafua taswira nzima ya eneo na kuhatarisha afya ya watumiaji wakati wa usiku na asubuhi kabla hazijaondolewa na wafanya usafi.

Ushauri wangu ni kwa wasimamizi wa stendi hiyo iliochini ya Halmashauri ya Ilemela kuweka vyombo vya kuwekea uchafu ili kuzuia utupaji holela wa taka na kurundika taka maeneo yasio stahiki.

IMG_3234.jpeg
 
Back
Top Bottom