Uongozi wa Taifa Bila Elimu ni Kama Kuvua Samaki Bila Uvuvi - Tunahitaji Mabadiliko Haraka!

Uongozi wa Taifa Bila Elimu ni Kama Kuvua Samaki Bila Uvuvi - Tunahitaji Mabadiliko Haraka!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Binafsi, ninahisi uchungu na maumivu makubwa kwa kuona taifa letu linavyoelekea kwenye matatizo makubwa ambayo tungeweza kuyazuia kama tungekuwa na viongozi walio na elimu na uwezo wa kutatua changamoto za kweli. Samia anaheshimika sana, lakini kwenye suala la kuongoza taifa lenye zaidi ya milioni 64 ya watu, nadhani ni dhahiri kwamba elimu pekee haitoshi.

Yaani, mtu anavyoongoza taifa bila elimu, ni kama kuendesha gari bila leseni. Huwezi kutegemea nchi ipige hatua mbele kama viongozi wanakosa uwezo wa kimsingi wa kuendesha mabadiliko ya kweli. Ukiangalia, rais wetu sasa hivi amekuwa ni furaha ya machawa, huku akizungukwa na watu wanaoendelea tu kula bata huku taifa likiwa linazidi kuangamia.

Nashangaa, kweli hamuoni ndugu zangu? Hamuoni jinsi uchumi wetu unavyoshuka, ajira zinavyozidi kupungua na vijana wakiwa wanakosa matumaini kabisa? Tunasikia ahadi kila mwaka, lakini hakuna kinachoendelea. Tumechoka na maneno ya watu wanaoishi kwenye mazulia, huku wakiwa hawana mawazo ya kuboresha hali yetu.

Vijana tumejaa uchungu! Tunavyoendelea kuvua samaki kwenye bahari ya ajira, tunaona kama tunaingiza mitindo ya kimarekani, lakini tunazama zaidi na zaidi! Ni vipi tutakubaliana na mfumo huu wa kuridhika na maisha ya chini, huku tukiendelea kufichwa na kivuli cha uongozi wa division zero? Tena wakati taifa letu linahitaji viongozi wa kiwango cha juu kabisa. We can't keep doing the same thing expecting different results.

Yaani, inasikitisha kuona kwamba mtu mwenye master's degree kama mimi hawezi kuishi kwa amani kwa sababu ya mifumo ya kifisadi, huku wengine wakiwa wanatumia vyeo vyao kututawala kama watoto wa mtaani. Lakini sijajua ni kwa nini tunamvumilia mtu ambaye anayeongoza nchi kwa kutegemea tu maneno, ahadi za hewa, badala ya kutekeleza.

Wazee, hii hali inatufikisha pabaya! Vijana wanaishi kwa maumivu ya kuona taifa letu linavyoenda chini, na sisi tumekufa kwa kifo cha kimya, tukijua kuwa tunahitaji mabadiliko makubwa. Tunahitaji mabadiliko ya kweli, mabadiliko ya kuleta ajira, mabadiliko ya kukuza uchumi na mabadiliko ya kuzuia mifumo ya kifisadi ambayo inaua ndoto za vijana wengi.

Hatuwezi kuendelea kuridhika na hili. Tunahitaji viongozi wenye elimu, wenye uwezo na ambao wanaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Kila mmoja wetu anapaswa kuamka na kupigania haki yetu, tuache kuburuzwa na mifumo hii potofu.
 
Kijana umesoma na una Elimu nzuri ya Master's halafu nchi wanafaidi machawa wa fom foo failure Huku ndugu na watoto wao wakila mema ya nchi. HAKIKA INATIA HASIRA SANA YAANI MNO.

Watawala wanalipana mishahara minono na marupurupu kibao Huku WATUMISHI wengine wakiishi kwa madeni makubwa.

VIONGOZI WETU NI MAKANJANJA NA HAWANA HURUMA WALA UTU.
 
Back
Top Bottom