busha
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 1,712
- 2,577
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vyura wote njoon msome hii comment inawahusuTatizo la Yanga ni maono ya viongozi. Baada ya kubwa kuliko wao walijisahau wakadhani bakuli litadumu. Walisajili kwa mbwembwe wachezaji wa nje tena wale waliokuwa kwenye tetesi za kusajiliwa na mahasimu wao. Kumsajili mchezaji wa nje tena garasa kuna gharama sana tiketi za ndege, vibali TFF, uhamiaji, wizara ya kazi, gharama za kuvunja mkataba n.k. bado hujamtafutia nyumba. Halafu mchezaji huyo huyo anakuja kuwekwa benchi na Mapinduzi Balama.
Kama viongozi wa Yanga wangekuwa na maono ya mbali wangesajili angalau wachezaji wawili tu wa kimataifa Lamine Moro na Patrick Sibomana halafu pesa iliyobaki wangetafuta wakina Mapinduzi Balama wa kutosha hapa hapa bongo. Timu ingefanya vizuri kwa gharama ndogo tu.
Pia kuna suala la kamati mbalimbali zilizoundwa ambazo jumla yake zina wajumbe zaidi ya 100. Kamati zote hizo na wajumbe wake kweli wana umuhimu wowote kwenye klabu ambayo vyanzo vya mapato ni pamoja na kuwachangisha wanachama wake? Ningewaelewa viongozi wa Yanga iwapo kamati hizo zote na wajumbe wake wote wangekuwa ni maalum kwa ajili ya kuitafutia Yanga vyanzo vya mapato ya kuendesha timu.
Kuna Jengo la klabu pale Jangwani. Iwapo viongozi wangekuwa na maono wangetoa kiasi fulani cha pesa baada ya kubwa kuliko wakakarabati jengo likatumika aidha kukodisha kibiashara au kuweka kambi ya wachezaji kupunguza gharama za kukodi kambi kwenye hoteli.
Nilipata shida sana kumuona kiongozi mkubwa wa Yanga kwenye runinga anashabikia suala la kuvaa kipensi kumunga mkono Zahera wakati kafungiwa na TFF halafu tena kiongozi huyo huyo akasema watagomea nembo ya mdhamini kwa kuwa ina rangi nyekundu. Kwenye uendeshaji wa timu kubwa ya mpira kama Yanga haya ni mambo madogo sana kwa kiongozi mkubwa kwenda kwenye media na kuyapa sapoti badala ya kuumiza kichwa kuitafutia Yanga vyanzo mbadala vya mapato na kutafuta namna nzuri ya kupunguza gharama za uendeshaji wa timu.
tutavuka tu.Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla ametoa ufafanuzi juu ya mapato na matumizi ya klabu hiyo tangu uongozi wake ulipoingia madarakani, Juni 2019, huku akibainisha uwepo wa madeni ambayo wamerithi kutoka kwa uongozi uliopita.
Msolla amesema gharama za kuendesha timu ni kubwa, kuliko mapato yanayoingia, huku wakiwa wamerithi madeni makubwa kutoka katika uongozi uliopita ambayo inabidi yalipwe au kupunguzwa kadri inavyowezekana.
“Nimeamua kuja kwenu Waandishi ili nitoe ufafanuzi juu ya mapato na matumizi ya klabu yetu. Tulivyoingia madarakani tulikuta timu madeni makubwa ambayo tumejitahidi kuyapunguza huku bado tukitakiwa kuiendesha timu”, alisema Msolla.
Mwenyekiti huyo ametaja madeni makubwa ya aina nne waliyorithi kama ifuatavyo:-
1. Serikali (Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ shilingi milioni 800),
2.Ada ya uhamisho ya wachezaji waliosajiliwa miaka miwili iliyopita shilingi milioni 254.
3. Madeni ya makocha na wachezaji waliopita (Hans Van Pluijm, George Lwandamina, Youthe Rostand, Donald Ngoma na Obrey Chirwa) jumla shilingi milioni 600.
4. Watu binafsi shilingi milioni 237
5. Gharama za Usajili wa timu za wakubwa na ile ya Wanawake shilingi milioni 600.
Msola ametaja vyanzo vya mapato vya klabu hiyo ambayo ni SportPesa, KCB, Vodacom, Azam TV, GSM, Yanga TV na kampuni ya Maji ya Afya, ambayo kwa mwaka wanapata shilingi bilioni mbili wakati gharama za kuiendesha timu ni Bilioni nne.
Aidha Msolla amewaahidi wanachama wa timu hiyo kuwa, mpaka Mei 2020, watakuwa wameingia katika mfumo wa uwekezaji kwa njia ya hisa. Amesema watawashirikisha Wanachama katika kila hatua ili maamuzi yawe ya watu wote.