Uongozi wa timu ya Yanga wafunguka kuwa wana deni la zaidi ya milioni 200, wachezaji walioondoka watajwa

Tatizo la Yanga ni maono ya viongozi. Baada ya kubwa kuliko wao walijisahau wakadhani bakuli litadumu. Walisajili kwa mbwembwe wachezaji wa nje tena wale waliokuwa kwenye tetesi za kusajiliwa na mahasimu wao. Kumsajili mchezaji wa nje tena garasa kuna gharama sana tiketi za ndege, vibali TFF, uhamiaji, wizara ya kazi, gharama za kuvunja mkataba n.k. bado hujamtafutia nyumba. Halafu mchezaji huyo huyo anakuja kuwekwa benchi na Mapinduzi Balama.

Kama viongozi wa Yanga wangekuwa na maono ya mbali wangesajili angalau wachezaji wawili tu wa kimataifa Lamine Moro na Patrick Sibomana halafu pesa iliyobaki wangetafuta wakina Mapinduzi Balama wa kutosha hapa hapa bongo. Timu ingefanya vizuri kwa gharama ndogo tu.

Pia kuna suala la kamati mbalimbali zilizoundwa ambazo jumla yake zina wajumbe zaidi ya 100. Kamati zote hizo na wajumbe wake kweli wana umuhimu wowote kwenye klabu ambayo vyanzo vya mapato ni pamoja na kuwachangisha wanachama wake? Ningewaelewa viongozi wa Yanga iwapo kamati hizo zote na wajumbe wake wote wangekuwa ni maalum kwa ajili ya kuitafutia Yanga vyanzo vya mapato ya kuendesha timu.

Kuna Jengo la klabu pale Jangwani. Iwapo viongozi wangekuwa na maono wangetoa kiasi fulani cha pesa baada ya kubwa kuliko wakakarabati jengo likatumika aidha kukodisha kibiashara au kuweka kambi ya wachezaji kupunguza gharama za kukodi kambi kwenye hoteli.

Nilipata shida sana kumuona kiongozi mkubwa wa Yanga kwenye runinga anashabikia suala la kuvaa kipensi kumunga mkono Zahera wakati kafungiwa na TFF halafu tena kiongozi huyo huyo akasema watagomea nembo ya mdhamini kwa kuwa ina rangi nyekundu. Kwenye uendeshaji wa timu kubwa ya mpira kama Yanga haya ni mambo madogo sana kwa kiongozi mkubwa kwenda kwenye media na kuyapa sapoti badala ya kuumiza kichwa kuitafutia Yanga vyanzo mbadala vya mapato na kutafuta namna nzuri ya kupunguza gharama za uendeshaji wa timu.
 
Vyura wote njoon msome hii comment inawahusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tutavuka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…