Uongozi wa UDOM na fedha za majoho

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma uliwatoza wahitimu wa chuo hicho kiasi cha Tsh. 40,000/=ikiwa ni ada ya kuchukua majoho kwa ajili ya mahafali. Uongozi uliahidi kurejesha Tsh. 20,000/= kama mhitimu angerejesha joho baada ya mahafali. Wahitimu (Undergraduate na wale wa Masters) wakafanya hivyo. Walipoomba fedha yao danadana ikaanza hadi leo.

Uongozi wa Udom hauoni kwamba kufanya hivyo ni kujidhalilisha mbele ya jamii inayoamini kwamba chuo kikuu ni taasisi ya kuigwa. Kutokana na hili jamii inajifunza na kuiga nini?
 
si bora kwenu hapo ni sh.20 elf! Sisi wenzenu wa tumaini iringa,tumemaliza mwaka jana na baadhi,tunadai caution money elf 50! Hakuna tulichoambulia,zaidi wanatupiga tu dana dana! Inasikitisha sana tu
 
Ondfokeni na majoho maana mlitoa pesa mkapewa majoho, halafu mkatakiwa mrudishe mpewe hela, umliwapaje majoho bila kurudishiwa pesa? Mnawaogopa na mkiwagomea mnawaonea maana kila mahali uchakachuaji tu.
Daini chenu au acheni mliwe tu: Hiyo mmepigwa mimba::mimba::mimba::mimba::mimba:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…