Uongozi wa Watu

Uongozi wa Watu

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
Na Peter Mwaihola

Tafsiri Isiyo rasmi inabainisha Uongozi kuwa ni kuonyesha namna ya kufanya kitu, jambo kama vile kuonyesha njia.

Dhana ya Uongozi ilianza Miaka ya zamani Sana kutoka enzi za Ukabaila na ukoloni kwakua jamii lazima iende kwa kuwa na dira maalumu yenye muelekeo.

Uongozi mbalimbali uliwahi kutokea duniani na kisha ukaanguka ama kushindwa kupata uungwaji mkono kutoka kwà raia wake.

Uongozi wa kiyahudi ni miongoni mwa Uongozi imara kuwahi kutokea duniani lakini ukaanguka kutokana na baadhi ya raia kuuchukia, kuukimbia na kuushuhudia ubaya.

Kisa Cha Uongozi wa kiyahudi kuanguka ndicho kilichopelekea Dora ya kiyahudi kuyumba na kumezwa na Dora ya kiroma na kuacha kizazi Cha uyahudi kikizagaa barani ulaya.

Tuachane na mifano hiyo turudi kwenye hoja ya msingi.

Je, ni vigumu Uongozi kuwaridhisha raia wake?

Ndio Inaweza kuwa vigumu Uongozi kuwaridhisha raia wake kutokana na tabia halisi ya mwanadamu kutokubaliana na kila kitu.

Lakini Uongozi unaogusa maisha ya watu ndio hupendwa na watu wengi kwakua Uongozi wa namna hii hutatua matatizo yao kwà haraka Sana.

John F Kennedy alikua Rais kijana wa Marekani (1961-1963) aliamini katika Uongozi unaokaa karibu na tabaka linalo onewa Ili kulisaidia liweze kuungana kufurahia maisha na umma wa walio wengi.

Kennedy aliuwawa kwa sababu ambazo hazikujulikana lakini ilisemekana kuwa walio muua hawakupenda Kitendo chake kuwaunga mkono watu weusi kudai haki Sawa nchini humo.

Kwà maana hii Uongozi wa kila aina unaweza usipendwe kwa asilimia zote kwakua kila Kundi la wanao ongozwa Wana mahitaji yao yanayo tofautiana.

Lakini je mambo gani Uongozi ukifanya unaweza kuteka hisia za watu kwa kiasi fulani Cha kuridhisha? Baadhi ya mambo hayo yanatajwa kama misingi ya Uongozi Bora

Utawala wa kisheria (Rule of Law) unao fuata misingi ya kikatiba ya nchi husika na sheria za kimataifa.

Uongozi wenye kujali maumivu ya raia (feeling of Empathy) hii inapimwa na namna ambavyo Uongozi unavyo guswa na matatizo ya raia wake na kuwasaidia.

Uongozi Bora ni shirikishi (inclusive) huwapa nafasi raia kushiriki maamizi yanayo husu maisha yao na Maendeleo ya nchi husika.

Uwajibikaji. Uongozi Bora huwàjibika kwa raia wake pindi unapofanya makosa hukiri na kujisahihisha.

Uongozi bora uhusisha uwazi wa mambo (transparency Ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa usawa na uwazi na kuruhusu raia kuona na kukosoa.

Uongozi Bora hutokana jamii husika, huchaguliwa na watu kutoka kwenye jamii yao, lasivyo huo ni ukoloni.

Uongozi Bora huheshimu haki za binadamu.

Hii ni baadhi misingi Muhimu iwapo ikizingatiwa Somo la Uongozi litakuwa limetimia katika jamii.


Peter Mwaihola Ni Mwandishi, Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na jamii.
 
Back
Top Bottom