Uongozi wa Yanga uhusike na kulipa gharama zote za kuharibu mechi ya Derby iliyotakiwa kufanyika hivi leo. Uhuni kwenye soka haukubaliki

Uongozi wa Yanga uhusike na kulipa gharama zote za kuharibu mechi ya Derby iliyotakiwa kufanyika hivi leo. Uhuni kwenye soka haukubaliki

Kwa mujibu wa kanuni ya mpira
1. Timu ngeni inatakiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja siku moja muda ule ule ambao mechi itachezwa;
Kuzuiwa kutoshiriki mazoezi ni sawa na kuufuta mchezo usiwepo
Hiyo mistari miwili ya mwisho umeitoa wapi??
 
Haisemi lazima yafanyike ila inasema ni haki ya mgeni kikanuni. Pia kuna utaratibu wake. Lazima timu husika itoe taarifa kwa mwenyeji wa mchezo, kamishna wa mchezo kuwa watautumia uwanja kwaajili ya mazoezi. Simba hawakutoa taarifa popote ili waandaliwe mazingira. Hata taarifa ha bodi inakiri hilo. Msitafute sababu za kitoto. Leo simba kawaingiza watu hasara kubwa sana. Walipe gharama zote
Halafu, binafsi nina hili la kanuni ya 22(1) inayosema;

1741500605456.png


Swali, je! 51mba walipeleka malalamika kwa bodi ya ligi juu ya kuzuiwa kufanya mazoezi? Kama hawakupeleka, kwangu mimi, kikao kilichoghairisha mchezo ni batili. Hivyo, mechi ilitakiwa ichezwe. Ambaye hakuja uwanjani, kanuni ziseme naye..!!
 
Kwa mujibu wa kanuni ya mpira
1. Timu ngeni inatakiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja siku moja muda ule ule ambao mechi itachezwa;
Kuzuiwa kutoshiriki mazoezi ni sawa na kuufuta mchezo usiwepo
Hapo kwenye bold, WEWE NI MUONGO KULIKO SHETANI. Kanuni ipi inasema hivyo?
 
Ahlan bik

Football ukipenda iite Soccer ni mchezo wa kiungwana sana unaozingatia sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa na shirikisho la mpira duniani kwa maana ya FIFA na shirikisho la mpira katika nchi husika.

Kanuni zipo wazi kabisa na uongozi wa Yanga unafahamu fika kuwa timu ambayo itakuwa ni mgeni inatakiwa iruhusiwe kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mechi tena kwa kuzingatia muda ule ule wa mechi.

Simba Sc kwa kulijua hili walifata sheria zote , cha ajabu uongozi wa timu ya Yanga umeamua kufanya uhuni kwa kuweka vikundi vya wahuni wanaodai kuwa ni Makomandoo wa Yanga kwa ajili ya kuulinda uwanja na kupelekea kuzuia timu ya Simba sc isiingie uwanjani kufanya mazoezi.


Wito wangu kwa TFF na Bodi ya Ligi iangalie namna ya kutoa adhabu kali sana kwa uongozi wa timu ya Yanga ili iwe fundisho kwa wahuni wote wanaolenga kuchafua taswira na hadhi ya Ligi kuu ya NBC.

Dunia nzima ilijiandaa leo hii kushuhudia moja kati ya derby kongwe na bora zaidi kutokea katika bara la Africa na dunia nzima. Ila jambo la ajabu na aibu kusikia kuwa mechi hii haitachezwa kutokana na viongozi na uongozi wa timu ya YANGA kufanya uhuni.

Watanzania wengi wamenunua ving'amuzi kwa ajili ya kushuhudia mechi hii , Je nyinyi viongozi wahuni wa Yanga ,mtawalipa nini watanzania waliopoteza pesa zao kwa ajili ya kulipia ada ya ving'amuzi??

Kuna wanachama na mashabiki wenu wamesafiri kutoka mikoa mbalimbali kuja Dar-es-salaam toka juzi kuja kushuhudia moja ya tukio hili la kihistoria ila chakusikitisha wanakuja kuambiwa kuwa mechi haitakuwepo. Je mnawalipa nini hawa wanachama wenu waliopoteza nauli, gharama za malazi na vyakula na kikubwa zaidi muda wao kuja kushudia mechi hii???

Uongozi wa Yanga umefanya makusudi kabisa kwasababu walikuwa na uwezo wa kuwasiliana na wahuni wao waliowaandaa kuharibu mechi kuwa waruhusu msafara wa Simba sc uingie uwanjani.Ila cha ajabu hawakufanya hivyo na ni wazi tukio hili limeonesha dhamira yao ya kuamini imani potofu za kishirikina na pia kuharibu mechi.

Kuna viongozi wa FIFA na CAF pamoja na waandishi wa habari wa kimataifa wamesafiri kutoka mataifa yao kuja kushuhudia mechi hii live ila cha ajabu wanaambiwa kuwa mechi haitafanyika.

TFF na TPBL msipochukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya timu ya YANGA ,tambueni kuwa taifa zima litajua kuwa mnashirikiana na wahalifu hawa wa jangwani kuchafua taswira na hadhi ya moja ya ligi bora zaidi hapa barani Africa.

Wapo mashabiki wa timu hizi mbili walionunua tiketi kwa ajili ya kuingia uwanjani kuishuhudia hii Derby..Je pesa zao mnawarudishia?

Wasimamizi wa uwanja pia wametumia gharama zao kwa ajili ya kuhakikisha mechi hii inachezwa katika mazingira mazuri, Je Yanga mtarudisha gharama zao.?

TFF toeni adhabu kali kwa Yanga unaoongozwa na mwenyekiti wa vilabu barani Africa , Hersi Saidi. ili iwe fundisho kwa wahuni wengine wenye lengo la kuchafua ligi yetu.
Uko na akili timamu kweli? Yanga wana kosa Gani hapo.? Timu imeenda bila taarifa. Meneja hakufungua milango. Polisi walikuwepo. Je walinzi wa yanga walikuwa na ubavu kuliko polisi waliokuwepo pale? Polisi pia walishiriki kuwazuia Simba. Yanga wanakosa Gani? Usiwe mjinga kwa maslahi ya mpira wa Tanzania.
 
Haisemi lazima yafanyike ila inasema ni haki ya mgeni kikanuni. Pia kuna utaratibu wake. Lazima timu husika itoe taarifa kwa mwenyeji wa mchezo, kamishna wa mchezo kuwa watautumia uwanja kwaajili ya mazoezi. Simba hawakutoa taarifa popote ili waandaliwe mazingira. Hata taarifa ha bodi inakiri hilo. Msitafute sababu za kitoto. Leo simba kawaingiza watu hasara kubwa sana. Walipe gharama zote
Na ni haki yao kuamua kutumia uwanja wa mwenyeji au uwanja mwingine wanaoona unaofaa. Na hapa ndio mawasiliano yanatakiwa kwa mwenyeji wa uwanja kuhakikisha kila kitu kipo sawa. Anayetakiwa kuwasiliana na meneja wa uwanja wa Mkapa ni timu mwenyeji ili wanapompokea mwenyeji mambo yote yawe sawa.

Simba hawakutaka kuwajulisha Yanga muda wa kwenda kufanya mazoezi kwa hofu ya ushirikina. Walitaka mambo yawe ya kushtukiza. Kwa tukio baya hawamkutaarifu hata meneja wa uwanja kuwa wanaenda eneo lile.
 
Back
Top Bottom