Uongozi wa Yanga wakishukuru kikosi chao kwa sare na Nyasa big bullet ya Malawi

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Uongozi wa Timu ya Soka ya Yanga kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram wamekishukuru kikosi chao kwa kutoka Sare na Timu ya Nyasa Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa Kimataifa uliochezwa Malawi kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Taifa la Malawi na Yanga wakialikwa na Rais wa Taifa hilo.
 
Hii trip imenishangaza sana. Kwanza ulazima wake kufanyika wakati huu hadi timu kulazimika kuokoteza wachezaji. Pili Malawi mwaka huu wanaadhimisha miaka 59 ya uhuru, kawaida ungetegemea wawe wanajiandaa kwa maadhimisho ya mwakani wakati wanatimiza miaka 60 na siyo kuwekeza kupeleka timu mwaka huu.

Nahisi ombi la kuipeleka Yanga huko lilitokea upande wetu na kwa kuheshimu mamlaka wakashindwa kukataa.
 
Na mimi nadhani ni hivyo si uliona jezi zimekwenda kuzinduliwa ikulu ya Malawi
 
Hii trip imenishangaza sana. Kwanza ulazima wake kufanyika wakati huu hadi timu kulazimika kuokoteza wachezaji. Pili Malawi mwaka huu wanaadhimisha miaka 59 ya uhuru, kawaida ungetegemea wawe wanajiandaa kwa maadhimisho ya mwakani wakati wanatimiza miaka 60 na siyo kuwekeza kupeleka timu mwaka huu.

Nahisi ombi la kuipeleka Yanga huko lilitokea upande wetu na kwa kuheshimu mamlaka wakashindwa kukataa.
Upumbavu unakusumbua! Nani kakudanganya kuwa maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya uhuru ndiyo mialiko ya wapendwa wao lazima itolewe? Je unafahamu nini kinaweza kuwasibu mfano mafuriko makubwa kuliko yaliyowapata mwaka huu yanaweza kuwasibu?

Usiwachagulie mwaka upi waupe uzito mkubwa wacha raha wajipe wenyewe!
 
hivi unajua ulichoandika?
 
Sare / Draw sio Mbaya kwa kikosi cha tatu (YANGA - C)

Pia ni vema tumawaheshimu wenyeji katika sherehe yao ya uhuru, draw imetisha kabisa, kila upande umeshinda
 
Uongozi wa Timu ya Soka ya Yanga kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram wamekishukuru kikosi chao kwa kutoka Sare na Timu ya Nyasa Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa Kimataifa uliochezwa Malawi kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Taifa la Malawi na Yanga wakialikwa na Rais wa Taifa hilo. View attachment 2680288
Halafu kuna timu ilijisifia eti kwa kuifunga Nyasa Big Bullets!!

Maana hiki ni kikosi cha tatu cha Yanga, na bado wametoa sare. Vipi tungeingiza full mkoko kama wenyeji!!
 
uto mnasajili wachezaji kwa utaratibu wa vikosi?...manake kuna wachezaji wamesajiliwa kwa ajili ya kikosi cha kwanza, cha pili, tatu na nne?
 
Kwa hiyo mmeenda huko kucheza na wachezaji hawa wenye mvi? Masikhara yamezidi.

Screen Shot 2023-07-06 at 11.03.02 PM.png
 
uto mnasajili wachezaji kwa utaratibu wa vikosi?...manake kuna wachezaji wamesajiliwa kwa ajili ya kikosi cha kwanza, cha pili, tatu na nne?
Wachezaji kote duniani husajiliwa kutokana na viwango vyao. Ila mwisho wa siku kocha lazima awe na kikosi chake cha kwanza na cha pili.

Ila Yanga pekee ndiyo ina mpaka kikosi cha tatu! Na ndiyo hicho sasa kilichocheza ugenini jana, na kupata sare. Na ukumbuke wenyeji walichezesha kikosi chao cha kwanza.
 
Naweza kupata list ya wachezaji waliochexa Malawi?
 
Zaidi ya nusu ya wachezaji waliocheza walikodishwa kutoka kwenye vikundi vingine vya ngoma, si wachezaji ngoma halali wa Yanga. Wamalawi wamepigwa na kitu kizito mbele ya Rais wao.
 
Upumbavu unakusumbua! Nani kakudanganya kuwa maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya uhuru ndiyo mialiko ya wapendwa wao lazima itolewe? Je unafahamu nini kinaweza kuwasibu mfano mafuriko makubwa kuliko yaliyowapata mwaka huu yanaweza kuwasibu?

Usiwachagulie mwaka upi waupe uzito mkubwa wacha raha wajipe wenyewe!
Hahah. Dah!!
 
Zaidi ya nusu ya wachezaji waliocheza walikodishwa kutoka kwenye vikundi vingine vya ngoma, si wachezaji ngoma halali wa Yanga. Wamalawi wamepigwa na kitu kizito mbele ya Rais wao.
Inajulikana wengi wako vacation....no sawa kukodi nusu team 2 etc Uzuri viongozi walikuwepo....baadhi first eleven walikuwepo pia inatosha bana
 
first eleven ya Yanga unaijua?
 
Back
Top Bottom