Uongozi

Uongozi

BEAKER

Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6
Reaction score
1
Sera za Raisi wetu wa awamu ya tano ni nzuri sana kujenga Tanzania ya viwanda ili kuiwezesha kuingia katika uchumi wa kati lakini je swali la kujiuliza itawezekana kwenda sambamba na uwezo wa wananchi wake kwenye uwezo wa kufaidi au kumudu bidhaa zitokanazo na viwanda hivyo?. Mambo mengi yamekuwa yakijitokeza kwenye uongozi wa awamu hii ya tano ambapo wananchi wengi wamekuwa na kujiuliza moyoni na wali wenye uwezo wa kuandika wameandika kupitia mitandao ya kijamii na haya yote ni kwa ajili ya yatokanayo kwenye kizazi kijacho...
1. Kusinyaa kwa ajira kwa zaidi ya miaka miwili kuanzia sekta binafsi mpaka srekalini nikimaanisha wengi wanahitimu vyuo mbalimbali wakiwa na juzi tofauti lakini hawapati fursa mbalimbali za ajira ukiachana na wale walio kwenye mafunzo ya kiusalama zaidi.
2. Bila kushika kikotoaji au kufanya uchunguzi utagundua kwamba dalili mojawwapo ya kujua kama uchumi unakuwa au unayumba kiwango cha ongezeko la ajira sambamba na kiwango cha mishahara ...
3. Kukosekana kwa uwazi na ukweli kuhusu utendaji wa serekali pamoja na taasisi zake na ukweli ni kwamba kuweka wazi unaruhusu utoaji wa maoni na ukosoaji (wenye tija) na hapo ndipo ukiwa kiongozi unajipima je natenda kwa kufuata mategeo ya waloniweka au kinyume.
Yapo mengi sana lakini sisi kama vijana tunapaswa kutoa maoni na ushauri kwa wale watendaji wa mkuu wa nchi ili waweze kumshauri vyema maana Raisi anaweka au kuteua wasoma akitegemea watafanya mambo mazuri zaidi kuisaidia jamii lakini wakati mwingine inawezekana isiwe hivyo na hapo tunapaswa kukemea kwa nia njema bila kejeli wala matusi na sio kwa kupinga kila kitu na endapo unahoja yakupinga basi jaribu kuja ushauri wakuboresha kle unachohisi hakiendi sawa.
Naamini ukijiuliza kwa nini Mwalimu Nyerere alianzisha viwanda vingi lakini vikafa na kubakia magofu na ukapata jibu sahihi basi hapo ndipo uanze na ushauri kwa serekali ya awamu ya Tano ili wanapoanzisha uchumi wa viwanda amabao ndio chanzo kikubwa cha utajiri na uibuaji wa ajira Duniani waweze kuwa makini na vikwazo hivyo ili tusirudi nyuma miaka 50.
 
Back
Top Bottom