Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Mhu 8:11 SUV
[11] Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.
Tunashuhudia watu wakifanya mambo mabaya, wakati mwingine tunajiuliza mbona wanaendelea kufurahia maisha yao huku wakimkosea Mungu.
Onyo linalotolewa katika mstari huu wa biblia ni la kiroho, vile ilivyo hatari ya mtu kuzoea uovu kwa sababu haoni athari za haraka kwa kile kibaya anakifanya mbele za Mungu.
Watu wanafikiri kuchelewa kwa hukumu ya Mungu kwa watenda mabaya, watu wanaofanya mambo yasiyofaa, sio kana kwamba Mungu haoni, na sio kwamba Mungu anawapendelea, na sio kana kwamba Mungu ni dhaifu, Mungu anawapa nafasi za kutubu na kuacha mabaya yao.
Nafasi hii wanayopewa na Mungu, wapo watu hutafasiri vibaya uvumilivu wa Mungu, huona ni udhaifu, na wengine huona ni ruhusa au kibali cha kuendelea kutenda uovu.
Mitazamo yetu mibaya, au kuchelewa kwa hukumu ya Mungu, haiwezi kubadilisha adhabu ya Mungu juu ya watenda mabaya, watu wanaomtenda Mungu dhambi mbaya.
Tunaweza kujifariji na kuona mbona hatupati madhara kwa yale matendo yetu mabaya, tujue hiyo ni fursa kwetu ya kubadilika haraka kabla ya hasira ya Mungu haijaanza kutenda kazi kwetu.
Maovu yetu Mungu anayaona, ule uvumilivu wake kwetu ndio unatufanya tusione madhara yeyote kwetu, ilipaswa kuwa fursa kwetu ya kuchukua hatua za kubadilika na sio kuendelea kutenda uovu.
Tukielewa ukimya wa Mungu juu ya yale mabaya tunayoyafanya ni nafasi kwetu ya kubadilika, hatutajivunia tena uovu wetu, wala hatutakaa tujisifie kwa matendo yetu mabaya.
Ukiona unatenda maovu, au ukiona mtu anatenda maovu na Mungu yupo kimya, elewa huo ni uvumilivu wa Mungu, hupaswi kutafasiri kuwa ni udhaifu wa Mungu kuacha maovu yaendelee kufanyika kwa watu.
Ogopa uovu kama ugonjwa unaotisha dunia, na ukimya wa Mungu usiufanye ni fursa kwako kuendelea kufanya machukizo kwake, badala yake iwe ni nafasi yako ya kubadilika kabla mambo hayajaharibika.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana