Uozo chuo kikuu St. John Dodoma

Mpunumpunyenye

Senior Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
114
Reaction score
50
Uingizwaji wa wanafunzi wasio na sifa kusoma, katika hili chuo hiki kimekuwa kikichukua wanafunzi wasio na sifa za kujiunga kimasomo totauti na taratibu za wizara, kwa mfano wanafunzi wanaoingia kusoma certificate wengine hata elimu ya secondary hawajasoma
Diploma ndio balaa kuna ambao wanaingia wakiwa na D 3 tu za form 4 bila ya kuwa na cheti kingine chochote

UCHAKACHUAJI WA MATOKEO

Kumekuwa na tabia wa wafanyakazi na walimu kupewa rushwa za pesa na ngono ili kuwapa marks wanafunzi wanaofeli kwa mfano kuna mwalimu anaitwa imma wa masomo ya IT huyu amekuw kinara wa kuchakachua matokeo kuna wanafunzi hasa wa diploma tangu wanaanza chuo wamefeli masomo yote kila semester lakini wamemaliza wakiwa na vyeti.

MWISHO


Ninaomba serikali kupitia wizara na idara husika kufanya uchunguzi hata kidogo ili kuepusha janga hili linaloletwa na chuo hiki.
 
Daah inasikitisha sama ndugu!! Ila jiandae kisaikolojia kuna watu watakubeza tu japokuwa unachokisema ni cha ukweli.
 
Tatizo Wa Tanzania tunakariri Sana.kuna dogo alisomaga Diploma DIT.alipoenda China akasoma masters karudi mwajiri wake anasema ataitambua masters yake pale atakapoleta Chet cha bachelor. Kupata D au ata F Tanzania sio kama mtu Ana akili.Mazingira yakiwa mazuri mtu aliepata D au F anaweza Fanya vizuri tu.
Last week Diamond just std seven na My Whether ambae ata kusoma ajui wametengeneza mamillions ambayo wenye ma PhD ata wakipewa 100 years ya kufanya kazi awatoweza yapata.tafakari chukua hatua
 
Chipukizi;

wee vipi,elimu ni elimu tu!elimu ina mpangilio wake-hayo mambo yakina Diamond sijui mayweather yapeleke huko huko msituletee huku kwenye elimu yetu!

Yaani unatoka DIT na diploma umarudi na Masters (bila first degree)alafu unataka ikubalike?!! Toa usaniii wenu hapa
 
Last edited by a moderator:
Chipukizi;

Kwa hiyo unataka tubadili mfumo wetu tuufanye uwe ki-diamond au Mayweather c ndio?! Ukikubali kusoma nchini lazima ufuate kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika za kusimamia Elimu ktk ngazi husika. Huo u-diamond wako upeleke huko huko. Kesho usije ukatuletea Uzarina hapa
 
Last edited by a moderator:
Chipukizi

wewe utakuwa umegushi vyeti ndiomana unaongea utumbo kama huu. nani alikudanganya elimu inalinganishwa inalinganishwa na fedha?

Thamani ya elimu hata vipande vya almasi haviwezi kulinganishwa. Pesa/mali yaweza kununua vyeti lakini kamwe haiwezi kununua elimu.

Ndiomana kuna mabilionea au marais ambao watoto wao au wao wenyewe wamefeli na fedha zao au vyeo vyao havikuwasaidia kubadili matokeo.
 
Last edited by a moderator:
Kabla hujaomba chuo kuna haja ya kuangalia chuo unachaohitaji na sifa zake vya kutosha, ndio maana na chuo lazima kikague sifa zako ili kukukubali kwenye chuo chao, sasa kama sifa zako ndizo zilizokupeleka huko then unalaumu nini? Hicho hicho chuo chenye uozo wenye mamlaka ya ku rank vyuo vikuu wamekiwepo kiwe cha 15 kati ya vyuo zaidi ya 60 Tanzania kwa takwimu za karibuni, sasa sidhani kama wewe upo sahihi kuliko wao
 

Good point anataka wote waishie la saba madaktari waalimu, wahandisi watatoka wapi wapi hapo. Amesahau kuwa kuna specialization ya mambo mbalimbali hasa kwenye fani .
 

Kumbuka kuwa utaratibu uliopo sasa waombaji wanaomba kupitia tcu. Tcu ndio wanakupangia chuo though wanakupangia chuo miongoni mwa vyuo vinne ulivyovipendekeza. Lakin vyuo unavyopenda na kuvifahamu vema yaweza kuwa ni viwili tu kat ya hivyo vi4, hivyo, hvyo vngne ukaviweka tu kama kamari bila kuvifahamu kwa undani..... vingine ukaviamini kwa kigezo cha kuwa chuo cha dini. So C kigezo cha kuhalalisha elimu holela, nadhani mamlaka husika bado wana wajibu wa kuvikagua kila mara ili kujiridhisha.
 
Hii kali...hiki chuo nasikia kuna mwl mmoja wa masomo ya sayansi anafundisha madarasa yote first year hadi third year kozi zaidi ya tisa kwa muhula...anawezaje..lazima atakuwa chini ya kiwango na atagawa A tu ili apendwe na wanafunzi....hii ni hatari
 
Hii kali...hiki chuo nasikia kuna mwl mmoja wa masomo ya sayansi anafundisha madarasa yote first year hadi third year kozi zaidi ya tisa kwa muhula...anawezaje..lazima atakuwa chini ya kiwango na atagawa A tu ili apendwe na wanafunzi....hii ni hatari

kama ndo hivyo mbona ni hatari sana
 
Hii kali...hiki chuo nasikia kuna mwl mmoja wa masomo ya sayansi anafundisha madarasa yote first year hadi third year kozi zaidi ya tisa kwa muhula...anawezaje..lazima atakuwa chini ya kiwango na atagawa A tu ili apendwe na wanafunzi....hii ni hatari

Duuuuh hahahahaaaaa noma sana kama ni kweli
 
mkuu sio kwamba wewe umefeli na huyu jamaa amekataa kukuongezee marks ndo ukaja hapa.Kimsingi Ukisoma kwa bidii na pili ukaweka malengo hutakuwa na haja za kuomba marks kwa walimu ila marks zitakuja zenyewe kutokana na juhudi zako.
 

Kaka hata kwa Diamond hapo unatubeza, Kumbe Diamond naye yupo levo za Floyd Mayweather kwenye kipato kitu ambaye itamchukua mtu wa phd kufukuzia kipato chake miaka 100.

Au hao ma PHD tunaowaona wanajilipa Dola 12,000/= kwa mwezi kwenye miradi yao watakua wanacheza makida tu Kumbe.

Are u in Tanzania kweli au umetoka hapa enzi za Nyerere.
 
St. John kwa non-degree programs hasa za science kuna tatizo kubwa.
 

big up mkuu umenena vyema
 

Hata mdogo wangu aliyeishia std IV ana majengo mawili ya ghorofa K'Koo, kweli pesa anayopiga ni ndefu kuliko mimi mtumishi wa serikali mwenye degree mbili. Kwa hiyo kuchakachua kunalipa tuendelee? Elimu haina maana eti? Sijaelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…