Uozo kila mahali hakuna penye afadhali, tunaoumia ni sisi Wananchi

Uozo kila mahali hakuna penye afadhali, tunaoumia ni sisi Wananchi

KatetiMQ

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2022
Posts
249
Reaction score
506
Habari zenu wana JamiiForums,

Kwa kweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa habari mbalimbali hasa zinazohusu taifa letu la Tanzania kwa kweli tuna safari ndefu sana mpaka kufikia kile tunachokiita maendeleo na sisi kama wananchi inabidi tuamke kwa kweli.

Uozo kila mahari hakuna penye afadhali. Ukisoma ripoti za CAG utatamani kulia ukiwa kama mwananchi mpenda maendeleo. Haki ipo wapi nani awajibishwe tunaumia wananchi wa hali duni maji hakuna, umeme shida, bei za bidhaa juu alafu tujikwamue.

Hii leo pamoja na bei kubwa za bidhaa bado baba huyu mwenye watoto watatu na mke mmoja ataweza vipi kumudu gharama za chakula na kuwapatia elimu bora watoto wake kwa kweli inauma na inauma zaidi unaposikia shirika lako la mawasiliano linadai pesa nyingi tena linamdai mtu asiejulikana.

Hii leo mtu kula wali maharagwe uswahilini wanakuita Freemason. Nini mtazamo wako kuhusu mwenendo huu.
 
Tumia haki yako ya kikatiba, gombea uongozi wa kisiasa

 
Back
Top Bottom