KERO Uozo na ukiritimba Mahakama ya Mwanzo Ilala

KERO Uozo na ukiritimba Mahakama ya Mwanzo Ilala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

activist

Senior Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
180
Reaction score
281
Ni jambo la kusikitisha kwamba mahakama ya Mwanzo Ilala haina njia mbadala ya kufanya shughuli zanazotegemea umeme kuendelea kama kawaida pale umeme unapokatika. Kuna watu waliahidiwa kufuata nakala za hukumu ila wameshindwa kupata kwa kuwa umeme hakuna. Kinachokera zaidi kituo cha polisi Pangani ambacho kipo pembeni ya mahakama hii wao wana jenereta. Kuna watu ambao muda wao wa ku file rufaa Mahakama ya Wilaya unaisha leo hivyo kwa kukosa hukumu maana yake hawawezi tena kukata rufaa.

Pamoja na hivyo, kwa kuwa umeme umekatika mtaa wote wa pangani na Tanga nilijaribu kuwauliza kama wamewasiliana na Tanesco walichonijibu ni kuwa wao hawana mamlaka ya kuwapigia huduma kwa wateja tanesco kuwa wenye wajibu wa kuwasiliana nao ni mahakama kuu. Kwa mambo haya Tanzania ina safari ndefu sana bado. Yaani kuwapigia tanesco huduma kwa wateja ili kutoa taarifa ya tatizo la umeme ni mpaka mahakama kuu iwasiliane nao. 🙌😭😭
 
nilijaribu kuwauliza kama wamewasiliana na Tanesco walichonijibu ni kuwa wao hawana mamlaka ya kuwapigia huduma kwa wateja tanesco kuwa wenye wajibu wa kuwasiliana nao ni mahakama kuu. Kwa mambo haya Tanzania ina safari ndefu sana bado. Yaani kuwapigia tanesco huduma kwa wateja ili kutoa taarifa ya tatizo la umeme ni mpaka mahakama kuu iwasiliane nao. 🙌😭😭
 
Back
Top Bottom