Anonymous
Senior Member
- Apr 6, 2006
- 118
- 339
Kwa Kiswahili kinajulikana kama CHOMBO CHA KUSIMAMIA UBORA TANZANIA (TBS)
Jina zuri lakini la kizungu.. Sio tatizo sana
Jengo zuri la viwango
Mazingira mazuri ya Kazi
Vitendea Kazi bora
Maslahi, marvellous na mishahara yakuvutia LAKINI
Watendaji wake ni waovu, wanuka rushwa wasio na chembe ya uzalendo wa nchi yao
Asilimia 90 ya bidhaa za Tanzania zenye nembo na muhuri wa TBS ni magumashi tupu,, kuanzia kupeleka sampuli, kuzichakata majibu mpaka kupata cheti cha ubora ni rushwa na magumashi mwanzo mwisho
Jaribu kufuata taratibu halali za kupata cheti cha ubora uone utakavyosoteshwa kwenye zile corridor za lile jengo refu la ghorofa pale Ubungo Mataa.
Unaweza kumaliza mwaka hujapata cheti kutokana na sampuli kufeli, kuharibika ama kupotea na usumbufu mwingine mwingi tuu.
Kupata cheti kimoja cha ubora cha TBS ukiachana na ada halali rushwa ni kati ya milion 2 mpaka 5 kwa viwanda vya kawaida Wafanyakazi wa hii taasisi hawaishi kwa mishahara bali kwa rushwa na wanashindana kuvaa kubadili magari na simu za bei mbaya, bado mijengo na party za kila weekend.
Bidhaa nyingi zenye nembo ya ubora ya TBS hazijatimia zimepunjwa ujazo ama zimetengenezwa kwa malighafi hafifu ndio maana miradi mingi yenye ufadhili wa wazungu na inayosimamiwa na wazalendo wenye uchungu na nchi yao vifaa na malighafi za ujenzi huagiza nje ya nchi
Tunapohubiri uhujumu uchumi tusiwawazie tu wafanyabiashara bali na hawa waangalizi wa ubora tuliowaamini.
Soma Pia: Utitiri wa viwanda vya bati Tanzania na paa za nyumba zenye bati mijini kuwa na kutu ni Udhaifu mkubwa uliopo TBS
Inawezekana hii habari ikapata upinzani mkali lakini huo ndio ukweli na uhalisia
TBS imeoza..