Hii shule,zamani ilikuwa nzuri, Mmiliki wa shule sasa amelewa sifa matokeo ya mitihani hovyo,Ada za shule ipo juu
Huwezi kuamini waliomaliza form iv 2015 walikuwa 875, hivi idadi kubwa namna hii ya wanafunzi katika darasa moja tu, unafuatiliaje maendeleo ya mwanafunzi darasani.
huu ni wizi wa fedha za wazazi tena wizi wa mchana kweupe, wazazi wanajua wamewakabidhi waalimu wanafunzi ili wafuatilie maendeleo yao darasani kumbe hata waalimu wenyewe wanapunjwa maslahi yao.
kielelezo kizuri ni matokeo ya form iv 2015 matokeo ni hovyo div.iv karibia watoto 360, kwa kifupi shule hii siyo ya kupeleka mtoto pale iko kibiashara zaidi sio kitaaluma.
kichekesho eti hata kutoa result slip za wanafunzi ni lazima mwanafunzi atoe 50,000/= kwanza huu si wizi jamani hivi serikali haioni wizi na dhuruma zinazofanywa na shule hii?