Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ni kama vile kuna vita baridi ya kugombea Afrika kati ya Marekani (pamoja na mataifa mengine ya magharibi) dhidi ya China. Kila mmoja anajitahidi kuongeza ushawishi wake barani Afrika kupitia vitu kama uwekezaji, misaada N.K
Kwenye hili la mkataba wetu na DP World ni wazi kuwa mchina amepigwa bao dakika za majeruhi.
China ilikuwa na mpango kabambe wa kuwekeza katika bandari kubwa zaidi pale Bagamoyo, laiti wangefanikiwa kwenye hili basi ingewaongezea sana ushawishi wa kiuchumi na kisiasa nchini kwetu na ukanda mzima wa Afrika mashariki.
Sasa kwa masharti yale ya ule mkataba wetu wa IGA sidhani kama kuna mpango wowote wa kuendelea na ule mradi. DP World hawezi kuja kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye bandari ya Dar alafu mtu mwingine ajenge bandari pale Bagamoyo na kuleta ushindani.
Kama mnavyojua UAE ni mdau wa karibu sana wa Marekani, na Marekani ni bingwa wa kutumia mataifa mengine kulinda maslahi yake. Ni wazi kuwa kwenye hili Mabeberu wameibuka kidedea. Mchina na wadau wake waliokuwa wanaupigia chapuo ule mradi wa Bagamoyo wamepigwa bao la kisigino.