Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Siku mbili tangu ziibuke taharuki na malumbano katika Mtaa wa Mabibo Wilayani Ubungo Jijini Dar es salaam baada ya nyumba zaidi ya nne na fremu zaidi ya tano kuvunjwa licha ya Mahakama kutoa zuio kwakuwa eneo lina mgogoro kati ya Mume na Mkewe.
Anayedaiwa kununua eneo hilo amerudi tena na kuvunja nyumba 3 zilizosalia ambazo Mke huyo na Familia hiyo walikuwa wanaishi na kupelekea Mke na Familia nzima walale nje wakiwa na Watoto wadogo.
Eneo hilo ni mali ya Mzee Mwinjuma Mazige na Mkewe Aziza Selemani ambao walioana na kuishi kwa muda mrefu wakiwa na Watoto saba, kabla ya baadaye Mzee huyo kuoa Wake wengine wawili na kumtelekeza Mke na Familia na kuanza kuuza maeneo wanayomiliki bila kumpa mgao Aziza ambaye walitafuta mali pamoja na kupelekea Aziza kufungua kesi na Mahakama kuweka zuio kuwa eneo la Mabibo lisiuzwe lakini bado Polisi wameendelea kusimamia zoezi la uvunjwaji wakisema ni agizo la Boss wao.
Itakumbukwa juzi October 13,2024 baada ya kufika eneo hilo @AyoTV_ iliongea na DC Bomboko kwa njia ya simu na kukiri ni kweli alipopigiwa kuwa nyumba zinabomolewa akaagiza zoezi lisitishwe na amri ya Mahakama iheshimiwe lakini cha kushangaza jana October 14,2024 Mtu mmoja anayedaiwa kununua eneo hilo kwa zaidi ya Tsh. bilioni 1, alikaidi agizo la Mahakama na la DC na kumalizia kuvunja nyumba zilizosalia huku akisema yeye ni Mtu mzito na hakuna wa kumtishia
“Wametuambia sisi tuna mkono mrefu, nyinyi hamtufanyi lolote hata mkienda kwa DC au wapi hamtufanyi lolote tukawaambia kama hao hawatofanya lolote Mama yetu Samia atatusaidia, Mama asipopata haki huyu Wananchi hatuwapi kura, mnajali wenye hela Masikini hamtujali”
Bi. Aziza amenukuliwa akisema “Waandishi mlipoondoka juzi ileile usiku walikuja Watu wakaanza kuvunja nyumba kwa nyundo tukawaitishia Wezi wakakimbia, jana wakaja na gari na kuvunja, baadaye Polisi wakaja wakatupakiza kwenye Defender kutupeleka Police Oysterbay tukahisi watatusaidia badala yake tumefika Polisi wakatuambia tuache kelele, tusiharibu majina ya Watu kwamba eneo limeuzwa kihalali”
View: https://x.com/millardayo/status/1846280668059521404?t=POFdBxh7XVRF-bWSn_G4ng&s=09
DC Bomboko amesema leo amefika eneo hilo na atatoa tamko kesho kupitia @AyoTV_,…… jitihada za kuongea na aliyenunua eneo hilo zinaendelea.
#MillardAyoUPDATES