Upandikizaji wa moyo wa Nguruwe kwa binadamu

Wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani wamesema chini ya kipindi cha miaka 3, wataanza kutumia Moyo wa Nguruwe kuokoa maisha ya binadamu ambao wanahitaji moyo ili kuishi.

Je hawaoni kama huyo nguruwe atakayedhurumiwa uhai wake kwaajili ya binadamu hatakuwa ametendewa haki?
Je kule nchi zisizokubaliana na nguruwe haya yatafanikiwaje?
Je hawajaona kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu zaidi kutatua tatizo la moyo husika badala ya kutwaa moyo wa kiumbe mwingine?
 
Kuna boss wangu somewhere alikuwa anatumia kiungo kimojawapo changuruwe sikumbuki vizuri kama ni moyo ama kitu kingine. Utaalamu huu ni wa tangia zamani maana hiyo ilikuwa miaka ya mwisho ya 90.


Unaona sasa!!! nitashangaa sana kusikia mtu anakula nyama ya nguruwe, kama nguruwe ameweza kutatua shida yake, huyo ni ndugu, kwanini mtu umle ndugu yake
 
Kama Yehova witness hawataki kuchangiwa damu na dini nyingine zitaridhia kuwekewa moyo wa nguruwe?
Watalazimishwa kuwekewa moyo wa nguruwe kama ambavyo watu hao hao wanataka Jehovah's witnesses walazimishwe kuwekewa damu!

Nadhani sasa ndio itaeleweka Jehovah witnesses wana maana gani wakisema utashi wa kidini usipingwe kwa kulazimisha kitu ambacho ni kinyume na imani ya mtu. Hata Shehe Mkuu akipata ugonjwa wa moyo atalazimishwa kupewa moyo wa nguruwe hadi kieleweke!
 
Moyo wenye afya utatolewa wakat mnyama huyu anachinjwa kwa ajili ya kitoweo.

Mioyo hii itahifadhiwa hospitali had itakapotumiwa.
 
mkuu samahani bali wanasanyansi wa uingereza sio marekani
source:sky news
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…