Upandishaji wa madaraja kwa watumishi wa Serikali bado ni kizungumkuti

Upandishaji wa madaraja kwa watumishi wa Serikali bado ni kizungumkuti

Ni kweli, lakini tushukuru hata kwa hao baadhi waliozingatiwa. Na bado kwa hakika mchakato unaendelea.

Tupende maendeleo ya wengine na mafanikio yao, nasi tutafikiwa.
wengi tuna maslahi na huo upandishwaji, wake zetu wanafanya huko huko utumishiw a umma na tunapenda wapande vyeo. inavyosemekana, kwa fununu, kule utumishi anayeweka watu kwenye mfumo ni mmoja tu naye ana masomo yupo shule, kwa hiyo mara aingize watu mara aende kufanya mitihani. hivi kumbe unaweza kukabidhi dhamana kubwa kama hii kwa mtu mmoja? kwani hakuna wafanyakazi wengine, au huyo ndio kashika hirizi wa katibu mkuu? fukuzia mbali watu wanaofanya kazi kwa udhaifu namna hii ati kwa kutegemea mtu mmoja. nataka kufikia leo jioni wife akirudi kazini aniambie mmempandisha. acheni uzembe wenu huko.
 
Mwishoni mwa mwezi tano, Serikali ilitoa kibali cha upandishaji madaraja kwa watumishi wa serikali. Zoezi la upandishaji likaanza rasmi mwezi wa sita ambapo baadhi ya watumishi waliona mabadiliko katika mshahara na mabadiliko katika mfumo wa ESS.

Zoezi hili limegubikwa na sintofahamu kutokana na kuwa hadi sasa watumishi wengi hawajaona mabadiliko ya muundo katika Mfumo wa ESS katika kipengele cha Profile na kupelekea kuwa na MANUNG'UNIKO MAKUBWA .

Hadi sasa serikali kupitia utumishi haijatoa taarifa yoyote juu ya sintofahamu hii ya madaraja. Hali ya morali ya kazi imekuwa ndogo sana kwa watumishi.

TUNAOMBA SERIKALI ITOE TAMKO JUU YA JAMBO HILI.
Nadhani mwezi huu wengi wataona mabadiliko
 
Back
Top Bottom