Yule ni gaidi aliyepania kuterrorise (kutia hofu) jamii ya polisi bila kujali yupi kamfanyia ubaya au yupi hahusiki. Hakuwa akilenga polisi fulani mwenye ugomvi naye kulipiza kisasi. Hakuwa na lengo la kuiba au kunyang’anya.
Ugaidi ni Kuua/kujeruhi jamii fulani kwa lengo la kuwatia hofu kubwa na kuvuruga shughuli na maisha yao kwa ujumla. Sio mashambulizi yote ya risasi ni ya kigaidi hata yakiwa mengi. Lengo ndilo hubainisha ugaidi au la.
Polisi waanze kukaa chonjo. Watanzania wengi ni watu wema lakini sio wote ni “wapole”. Yule ni mmoja tu tena kajiendea recklessly. Sasa kizazi kipya kinaingia taratibu. Siku kagenge ka “vichaa” wawili watatu hivi walionyanyaswa na polisi wakiamua kufanya maangamizi kwenye target maalum itakuwa tabu sana.