SoC04 Upangaji na Upimaji Ardhi kimkakati kuepukana na Changamoto ya Makazi holela katika Miji midogo, Miji, Manispaa na Majiji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Ukuaji wa miji kiholela nnchini Tanzania ni suala mtambuka ambalo limekua likitafutiwa muarobaini kwa muda mrefu. Kufuatia kasi ndogo ya upangaji wa matumizi ya ardhi na ujenzi wa kasi, makazi holela( makazi yasiyofata utaratibu pangwa) yamekua yakishuhudiwa sehemu tofauti tofauti.
Picha ya Makazi holela( Manzese, Dar-es-Salaam)
IMG_20240529_124046.jpg

Chanzo: Google Earth
Ujenzi holela una athari kubwa katika eneo zikiangukia katika nyanja ya kiuchumi,kihuduma,kimazingira na kijamii. Kesi za uvamizi wa maeneo ya umma,migogoro ya ardhi, mafuriko( kufuatia ujenzi kuziba mikondo ya maji na ukosefu wa miundombinu), ujenzi maeneo hatarishi, mlipuko wa magonjwa na mengineyo mengi.
Serikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo haina budi kuja na mpango mkakati maalumu wa upangaji na upimaji ardhi kabla ya uendelezaji wa eneo.

Upangaji na upimaji ardhi kimkakati kuendana na kasi ya ukuaji wa maeneo.
Upangaji maeneo kimkakati ni mpango wa upangaji wa matumizi ya ardhi kwa kuangalia vipaumbele vya eneo, mpango unafanywa kwa kuchagua eneo dogo la kimkakati na kulifanyia kazi.
Mpango huu utahusisha utambuzi wa maeneo yenye kasi kubwa ya ukuaji na kuandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi na kupimwa kwa haraka ili kuzuia ukuaji kiholela wa eneo. Upangaji na upimaji wa maeneo unafanywa kwa kutoka katika kitovu cha mvuto wa makazi kuambaa nnje kuelekea maeneo ambayo hayajaendelezwa.
Upangaji na upimaji utahusisha zoezi kuanzia eneo lililoendelezwa na watu kutoka nnje kwa umbali utakaoamuliwa na timu ya wataalamu kwa kuzingatia marejeo ya matokeo ya makadirio ya kasi ya ukuaji ya eneo. Upangaji huu utakua umegawanyika katika makundi matatu:
Maeneo yenye kasi kubwa ya ukuaji na uendelezwaji.
•Maeneo yenye kasi ya wastani ya ukuaji na uendelezwaji.
• Maeneo yenye kasi ya kawaida ya ukuaji.
Kufanikisha mpango wa upangaji na upimaji wa kimkakati wa ardhi mambo yafuatayo yatafanyika;

Utambuzi wa vichocheo vya ukuaji wa kasi wa maeneo katika halmashauri
Maeneo yanayokua kwa kasi hayakuibuka kama uyoga tu, bali kuna vichocheo vinavyoweka msukumo na kuvuta watu katika eneo husika, baadhi ya vichocheo hivi ni:
Bei ya maeneo
•Fursa za kibiashara(masoko na viwanda)
•Upatikanaji wa huduma( elimu,afya,maji,ulinzi,nishati namengineyo).
•Fursa za ajira, ardhi kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
•Upatikanaji wa malighafi na mengineyo.

Tathimini ifanyike kuainisha maeneo yote yenye kasi kubwa ya ukuaji na vichocheo vyake. Utambuzi ufanyike katika maeneo yote katika halmashauri na kuandaliwa taarifa.

Makadirio ya kasi ya ukuaji na utanukaji wa makazi katika eneo kwa miaka 5-10 mbele.
Hapa timu ya wataalamu wa mipango miji , watakwimu, mipango na maendeleo ya jamii zichanganue na kutambua maeneo, kasi yake ya ukuaji na makadirio ya ukuaji kwa siku zijazo.

Kuchagua maeneo ya vipaumbele kufanyiwa upangaji na upimaji kimkakati.
Maeneo yatakayoainishwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji baada ya tathmini ya makadirio ya kasi ya ukuaji yatachaguliwa. Mfano maeneo yenye viwanda,shughuli za uchumi, idadi kubwa ya watu, vituo vya biashara, maeneo yenye huduma nyingi za kijamii nakadharika.​

Bajeti kuweza kubeba gharama za zoezi
Kwa kuangalia bajeti iliyopo katika halmashauri, maeneo yenye uhitaji zaidi yataainishwa na kufanyiwa kazi kwanza.

Ushirikishwaji wa umma, upangaji wa matumizi ya ardhi na upimaji ardhi.
Maeneo yote yatakayokua yameainishwa kuwa ya kimkakati yataanza kufanyiwa kazi na idara ya ardhi katika eneo husika. Upangaji na upimaji utahusisha eneo zima lililoanishwa kwa kushirikiana na jamii husika(wamiliki wamaeneo). Punde baada ya mpango maeneo hayatachukuliwa na serikali/kampuni za upimaji bali yataendelea kuwa chini ya umiliki wa wanajamii husika.​

Upangaji na upimaji ardhi
Zoezi la upangaji na upimaji litakua limegawanyika katika makundi matatu kulingana na sifa ainishwa za eneo kwa kufuata mtiririko ufuatao:

Maeneo yenye makadirio makubwa ya kasi ya ukuaji na uendelezwaji.
Haya kutokana na kua na vichocheo vingi vya kuvuta wakazi utaandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi kilomita 20-50 toka usawa wa eneo la mvuto.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi na upimaji utaanzia mwisho wa eneo lililokaliwa na watu(makazi) na kuenda umbali wa kilomita 20-50 pande zote ili kuendana na kasi ya ukuaji wa eneo. Maendeleo mapya yote baada ya eneo lililoendelezwa yatafuata mpango wa matumizi.
Mchoro: Upangaji na upimaji ardhi 20-50 kilomita kuzunguka eneo la kimkakati.
IMG_20240528_155922.jpg

Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Maeneo yenye makadirio ya ukuaji wa wastani na uendelezwaji.
Haya yataandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi na upimaji kwa kuchukua eneo lenye umbali wa kilomita 10-20 baada ya eneo endelevu. Upangaji utahusisha pande zote za eneo ili kuwezesha maendeleo/ uendelezwaji mpya wa eneo kuingia katika eneo la kimkakati.

Mchoro: Upangaji na upimaji wa ardhi 10-20 kilomita baada ya eneo lenye watu kuzunguka eneo la kimkakati.
IMG_20240528_160007.jpg

Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Maeneo yenye makadirio ya ukuaji wa kawaida
Hapa upangaji na upimaji utachukua eneo la Kilomita 5-10 toka eneo lililoendelezwa na watu.

Mchoro: Upangaji na upimaji wa ardhi 5-10 kilomita baada ya eneo lenye watu kuzunguka eneo la kimkakati
IMG_20240528_160201.jpg

Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Upangaji wa matumizi ya ardhi na upimaji usisababishe kubaguliwa kwa wazawa. Mipango yote ya matumizi imeze shughuli za wazawa katika eneo, pasitokee changamoto ya ukuaji wa eneo kuwarazimisha wazawa kuhama toka katika maeneo yao ya asili kwa kigezo cha kushindwa kuendana na mipango ya matumizi, sheria na kanuni zinazoratibu maendeleo katika eneo. Mipango yote iwe ni jumuishi.

Muhimu:
Kwa kua maeneo yatakayokua yameandaliwa mpango na kupimwa hayatakua na maendeleo yoyote, usimamizi madhubuti hauna budi kuwepo kusimamia uendelezwaji wa maeneo hayo. Mamlaka ya idara ya Ardhi na watu wamazingira wataratibu zoezi zima.

Eneo la mpango liwekewe alama za kudumu kuonesha mgawanyo wa eneo na maeneo ya umma yawekewe alama za utambuzi( mabango) pamoja na uchongaji wa barabara katika eneo. Shughuli ndogondogo zisizohusisha ujenzi wa miundombinu ya kudumu zinaweza kuendelea chini ya uangalizi, mkazo ukiwa alama za upimaji kutokuharibiwa na kuzingatiwa pamoja na matumizi pangwa ya eneo.

Ili kufanikisha zoezi la uratibu wa shughuli za maendeleo katika eneo la mpango, mabaraza ya ardhi ngazi ya kata yatafanyiwa maboresho yafuatayo:
Elimu ya ardhi na sheria kwa wanabaraza.
•Uanzishwaji vitengo vya wataalamu wa ardhi katika kata.

Baada ya maboresho wajumbe wa baraza la ardhi na wataalamu wa ardhi wataratibu usimamizi wa ardhi, usuruhishi wa migogoro ya ardhi na kuratibu mauziano na umilikishaji ardhi kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi katika eneo.

Baada ya zoezi la upangaji na upimaji ardhi
•Nakala ya ramani ya eneo lililopangwa na kupimwa iwekwe ofisi ya kata. Hii itawarahisishia wananchi na wageni watakaohitaji kununua/ kufanya undelezaji wa maeneo katika eneo hilo kuwa na taarifa ya mgawanyo wa matumizi ya ardhi kwa kadri yalivyopangwa.
•Wataalamu wa ardhi watafanya zoezi la kuingiza na kuonesha katika ramani maendeleo yote mapya yatakayokuwa yakifanyika kwa kufata mpango wa matumizi.
•Taarifa za umiliki wa ardhi/mabadiriko ya umiliki na matumizi ya ardhi zitawekwa katika mfumo wa kidigitali na taarifa zote zitapatikana katani katika ofisi ya wataalamu wa ardhi.
•Elimu kwa umma juu ya mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo itolewe. Namba ya bure kupiga na kutuma ujumbe kuulizia masuala ya ardhi katika eneo la kimkakati kurahisisha upashanaji habari zigawiwe kwa wanannchi katika eneo husika.
•Mazoezi yote yahusuyo maendeleo ya eneo yaratibiwe katani, iwe ni ujenzi, mauziano, umilikishaji nakadharika, umma uzingatie hilo.

Faida za uwepo wa mpango wa matumizi ya ardhi uliotayari kabla ya eneo kufanyiwa maendeleo.
•Kutunza mazingira na kufanya maendeleo enderevu katika eneo.
•Kurahisisha usambazaji huduma(maji,barabara, huduma za dharula na nyinginezo).
•Kupunguza kesi za umilikishaji na uuzwaji wa ardhi kwa watu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
•Utambuzi wa wamiliki wa maeneo.
•Kuzuia uvamizi wa maeneo ya umma mfano maeneo ya wazi, soko, makaburi na mengineyo.
•Kuepuka maafa mbalimbali mfano mafuriko na mlipuko wa magonjwa wa mara kwa mara.​

Hitimisho
Tanzania tuitakayo ni ile yenye uratibu wa kimkakati wa shughuli kufikia lengo la maendeleo enderevu.
Mpango wa matumizi ya ardhi ni hatua muhimu katika kutatua changamoto ya ukuaji wa maeneo kiholela. Kasi ya ukuaji wa maeneo itafuata mpango ulioandaliwa hivyo ukuaji wa eneo ulioratibiwa. Maeneo ya kimpango yaendelee kuongezwa kadri maendeleo katika eneo yatakavyokuwa yakisogelea eneo la kimpaka la mpango. Kabla ya maendeleo hayajafika mpango wa kuyaratibu uwe tayari umeandaliwa.​
 
Upvote 10

Maeneo ambayo hayajaendelezwa ndiyo wakati mzuri sasa wa kuyapangilia......

Ndo matumizi mazuri ua akili kuona mbele.

Taarifa za umiliki wa ardhi/mabadiriko ya umiliki na matumizi ya ardhi zitawekwa katika mfumo wa kidigitali na taarifa zote zitapatikana katani katika ofisi ya wataalamu wa ardhi
Muhimu sana, maana wabongo kuuziana mara nnenne hawachelewi😆😆

Kabla ya maendeleo hayajafika mpango wa kuyaratibu uwe tayari umeandaliwa.
TUtaonekana nchi yenye akili sana tukiweza hili
 
Maeneo ambayo hayajaendelezwa ndiyo wakati mzuri sasa wa kuyapangilia......

Ndo matumizi mazuri ua akili kuona mbele.

Muhimu sana, maana wabongo kuuziana mara nnenne hawachelewi😆😆

TUtaonekana nchi yenye akili sana tukiweza hili
Akili tunazo saana mkuu! Swali ni tunazifanyiaje kazi🤗🤗🤗.
Kuna viutafiti vya IQ...sijui n vya kweli vinadai watu wengi hawajatumia angalau 10% ya uwezo wa akili zao
 
Wadau mnaonaje maeneo yetu yakipangwa na kupimwa pawe na ki utaratibu cha kuchonga mabarabara na kuweka miundombinu kabla ya kutumika?....ikitokea barabara zinafutika, zinachongwa tena, yaani kuwe na muundombinu unaoonesha alama ya kudumu.
 
Maeneo ambayo hayajaendelezwa ndiyo wakati mzuri sasa wa kuyapangilia......

Ndo matumizi mazuri ua akili kuona mbele.

Muhimu sana, maana wabongo kuuziana mara nnenne hawachelewi😆😆

TUtaonekana nchi yenye akili sana tukiweza hili
Naam Uhakika bro
 
Ukuaji wa miji kiholela nnchini Tanzania ni suala mtambuka ambalo limekua likitafutiwa muarobaini kwa muda mrefu. Kufuatia kasi ndogo ya upangaji wa matumizi ya ardhi na ujenzi wa kasi, makazi holela( makazi yasiyofata utaratibu pangwa) yamekua yakishuhudiwa sehemu tofauti tofauti.
Picha ya Makazi holela( Manzese, Dar-es-Salaam)
View attachment 3002620
Chanzo: Google Earth
Ujenzi holela una athari kubwa katika eneo zikiangukia katika nyanja ya kiuchumi,kihuduma,kimazingira na kijamii. Kesi za uvamizi wa maeneo ya umma,migogoro ya ardhi, mafuriko( kufuatia ujenzi kuziba mikondo ya maji na ukosefu wa miundombinu), ujenzi maeneo hatarishi, mlipuko wa magonjwa na mengineyo mengi.
Serikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo haina budi kuja na mpango mkakati maalumu wa upangaji na upimaji ardhi kabla ya uendelezaji wa eneo.

Upangaji na upimaji ardhi kimkakati kuendana na kasi ya ukuaji wa maeneo.
Upangaji maeneo kimkakati ni mpango wa upangaji wa matumizi ya ardhi kwa kuangalia vipaumbele vya eneo, mpango unafanywa kwa kuchagua eneo dogo la kimkakati na kulifanyia kazi.
Mpango huu utahusisha utambuzi wa maeneo yenye kasi kubwa ya ukuaji na kuandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi na kupimwa kwa haraka ili kuzuia ukuaji kiholela wa eneo. Upangaji na upimaji wa maeneo unafanywa kwa kutoka katika kitovu cha mvuto wa makazi kuambaa nnje kuelekea maeneo ambayo hayajaendelezwa.
Upangaji na upimaji utahusisha zoezi kuanzia eneo lililoendelezwa na watu kutoka nnje kwa umbali utakaoamuliwa na timu ya wataalamu kwa kuzingatia marejeo ya matokeo ya makadirio ya kasi ya ukuaji ya eneo. Upangaji huu utakua umegawanyika katika makundi matatu:
Maeneo yenye kasi kubwa ya ukuaji na uendelezwaji.
•Maeneo yenye kasi ya wastani ya ukuaji na uendelezwaji.
• Maeneo yenye kasi ya kawaida ya ukuaji.
Kufanikisha mpango wa upangaji na upimaji wa kimkakati wa ardhi mambo yafuatayo yatafanyika;

Utambuzi wa vichocheo vya ukuaji wa kasi wa maeneo katika halmashauri
Maeneo yanayokua kwa kasi hayakuibuka kama uyoga tu, bali kuna vichocheo vinavyoweka msukumo na kuvuta watu katika eneo husika, baadhi ya vichocheo hivi ni:
Bei ya maeneo
•Fursa za kibiashara(masoko na viwanda)
•Upatikanaji wa huduma( elimu,afya,maji,ulinzi,nishati namengineyo).
•Fursa za ajira, ardhi kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
•Upatikanaji wa malighafi na mengineyo.

Tathimini ifanyike kuainisha maeneo yote yenye kasi kubwa ya ukuaji na vichocheo vyake. Utambuzi ufanyike katika maeneo yote katika halmashauri na kuandaliwa taarifa.

Makadirio ya kasi ya ukuaji na utanukaji wa makazi katika eneo kwa miaka 5-10 mbele.
Hapa timu ya wataalamu wa mipango miji , watakwimu, mipango na maendeleo ya jamii zichanganue na kutambua maeneo, kasi yake ya ukuaji na makadirio ya ukuaji kwa siku zijazo.

Kuchagua maeneo ya vipaumbele kufanyiwa upangaji na upimaji kimkakati.
Maeneo yatakayoainishwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji baada ya tathmini ya makadirio ya kasi ya ukuaji yatachaguliwa. Mfano maeneo yenye viwanda,shughuli za uchumi, idadi kubwa ya watu, vituo vya biashara, maeneo yenye huduma nyingi za kijamii nakadharika.​

Bajeti kuweza kubeba gharama za zoezi
Kwa kuangalia bajeti iliyopo katika halmashauri, maeneo yenye uhitaji zaidi yataainishwa na kufanyiwa kazi kwanza.

Ushirikishwaji wa umma, upangaji wa matumizi ya ardhi na upimaji ardhi.
Maeneo yote yatakayokua yameainishwa kuwa ya kimkakati yataanza kufanyiwa kazi na idara ya ardhi katika eneo husika. Upangaji na upimaji utahusisha eneo zima lililoanishwa kwa kushirikiana na jamii husika(wamiliki wamaeneo). Punde baada ya mpango maeneo hayatachukuliwa na serikali/kampuni za upimaji bali yataendelea kuwa chini ya umiliki wa wanajamii husika.​

Upangaji na upimaji ardhi
Zoezi la upangaji na upimaji litakua limegawanyika katika makundi matatu kulingana na sifa ainishwa za eneo kwa kufuata mtiririko ufuatao:

Maeneo yenye makadirio makubwa ya kasi ya ukuaji na uendelezwaji.
Haya kutokana na kua na vichocheo vingi vya kuvuta wakazi utaandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi kilomita 20-50 toka usawa wa eneo la mvuto.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi na upimaji utaanzia mwisho wa eneo lililokaliwa na watu(makazi) na kuenda umbali wa kilomita 20-50 pande zote ili kuendana na kasi ya ukuaji wa eneo. Maendeleo mapya yote baada ya eneo lililoendelezwa yatafuata mpango wa matumizi.
Mchoro: Upangaji na upimaji ardhi 20-50 kilomita kuzunguka eneo la kimkakati.
View attachment 3002621
Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Maeneo yenye makadirio ya ukuaji wa wastani na uendelezwaji.
Haya yataandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi na upimaji kwa kuchukua eneo lenye umbali wa kilomita 10-20 baada ya eneo endelevu. Upangaji utahusisha pande zote za eneo ili kuwezesha maendeleo/ uendelezwaji mpya wa eneo kuingia katika eneo la kimkakati.

Mchoro: Upangaji na upimaji wa ardhi 10-20 kilomita baada ya eneo lenye watu kuzunguka eneo la kimkakati.
View attachment 3002623
Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Maeneo yenye makadirio ya ukuaji wa kawaida
Hapa upangaji na upimaji utachukua eneo la Kilomita 5-10 toka eneo lililoendelezwa na watu.

Mchoro: Upangaji na upimaji wa ardhi 5-10 kilomita baada ya eneo lenye watu kuzunguka eneo la kimkakati
View attachment 3002625
Chanzo: Picha bunifu ya mwandishi.​

Upangaji wa matumizi ya ardhi na upimaji usisababishe kubaguliwa kwa wazawa. Mipango yote ya matumizi imeze shughuli za wazawa katika eneo, pasitokee changamoto ya ukuaji wa eneo kuwarazimisha wazawa kuhama toka katika maeneo yao ya asili kwa kigezo cha kushindwa kuendana na mipango ya matumizi, sheria na kanuni zinazoratibu maendeleo katika eneo. Mipango yote iwe ni jumuishi.

Muhimu:
Kwa kua maeneo yatakayokua yameandaliwa mpango na kupimwa hayatakua na maendeleo yoyote, usimamizi madhubuti hauna budi kuwepo kusimamia uendelezwaji wa maeneo hayo. Mamlaka ya idara ya Ardhi na watu wamazingira wataratibu zoezi zima.

Eneo la mpango liwekewe alama za kudumu kuonesha mgawanyo wa eneo na maeneo ya umma yawekewe alama za utambuzi( mabango) pamoja na uchongaji wa barabara katika eneo. Shughuli ndogondogo zisizohusisha ujenzi wa miundombinu ya kudumu zinaweza kuendelea chini ya uangalizi, mkazo ukiwa alama za upimaji kutokuharibiwa na kuzingatiwa pamoja na matumizi pangwa ya eneo.

Ili kufanikisha zoezi la uratibu wa shughuli za maendeleo katika eneo la mpango, mabaraza ya ardhi ngazi ya kata yatafanyiwa maboresho yafuatayo:
Elimu ya ardhi na sheria kwa wanabaraza.
•Uanzishwaji vitengo vya wataalamu wa ardhi katika kata.

Baada ya maboresho wajumbe wa baraza la ardhi na wataalamu wa ardhi wataratibu usimamizi wa ardhi, usuruhishi wa migogoro ya ardhi na kuratibu mauziano na umilikishaji ardhi kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi katika eneo.

Baada ya zoezi la upangaji na upimaji ardhi
•Nakala ya ramani ya eneo lililopangwa na kupimwa iwekwe ofisi ya kata. Hii itawarahisishia wananchi na wageni watakaohitaji kununua/ kufanya undelezaji wa maeneo katika eneo hilo kuwa na taarifa ya mgawanyo wa matumizi ya ardhi kwa kadri yalivyopangwa.
•Wataalamu wa ardhi watafanya zoezi la kuingiza na kuonesha katika ramani maendeleo yote mapya yatakayokuwa yakifanyika kwa kufata mpango wa matumizi.
•Taarifa za umiliki wa ardhi/mabadiriko ya umiliki na matumizi ya ardhi zitawekwa katika mfumo wa kidigitali na taarifa zote zitapatikana katani katika ofisi ya wataalamu wa ardhi.
•Elimu kwa umma juu ya mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo itolewe. Namba ya bure kupiga na kutuma ujumbe kuulizia masuala ya ardhi katika eneo la kimkakati kurahisisha upashanaji habari zigawiwe kwa wanannchi katika eneo husika.
•Mazoezi yote yahusuyo maendeleo ya eneo yaratibiwe katani, iwe ni ujenzi, mauziano, umilikishaji nakadharika, umma uzingatie hilo.

Faida za uwepo wa mpango wa matumizi ya ardhi uliotayari kabla ya eneo kufanyiwa maendeleo.
•Kutunza mazingira na kufanya maendeleo enderevu katika eneo.
•Kurahisisha usambazaji huduma(maji,barabara, huduma za dharula na nyinginezo).
•Kupunguza kesi za umilikishaji na uuzwaji wa ardhi kwa watu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
•Utambuzi wa wamiliki wa maeneo.
•Kuzuia uvamizi wa maeneo ya umma mfano maeneo ya wazi, soko, makaburi na mengineyo.
•Kuepuka maafa mbalimbali mfano mafuriko na mlipuko wa magonjwa wa mara kwa mara.​

Hitimisho
Tanzania tuitakayo ni ile yenye uratibu wa kimkakati wa shughuli kufikia lengo la maendeleo enderevu.
Mpango wa matumizi ya ardhi ni hatua muhimu katika kutatua changamoto ya ukuaji wa maeneo kiholela. Kasi ya ukuaji wa maeneo itafuata mpango ulioandaliwa hivyo ukuaji wa eneo ulioratibiwa. Maeneo ya kimpango yaendelee kuongezwa kadri maendeleo katika eneo yatakavyokuwa yakisogelea eneo la kimpaka la mpango. Kabla ya maendeleo hayajafika mpango wa kuyaratibu uwe tayari umeandaliwa.​
Wataalamu wa ardhi pitieni makala hii.
 
Maeneo ambayo hayajaendelezwa ndiyo wakati mzuri sasa wa kuyapangilia......

Ndo matumizi mazuri ua akili kuona mbele.

Muhimu sana, maana wabongo kuuziana mara nnenne hawachelewi😆😆

TUtaonekana nchi yenye akili sana tukiweza hili
Kuuziana mara 2 mbili haitakuwepo....maana kila kitu kitaratibiwa KATANI. Na mie msisitizo naweka kwenye kua na ofisi za waratibu ardhi KATANI tuachane na utaratibu wa huduma mpaka HALMASHAURI.
 
Tuendelee kusoma na kupata shule humu! Wananchi wanaweza kujipangia wao wenyewe na kuachia barabara+ miundombinu mingine.....hata kama hawajafikiwa na mradi. Mifano hai ni vijijini kule hakuna wataalamu wa Ardhi ila pamepangika. Wana vijij oyeee👊👊
 
Na

Naona miaka ya hivi karibuni Utekelezwaji wa upimaji ardhi kimkakati unafanyika hadi vijijini
 
Ule wanafanya kwa ujumla!(Tuite "Master plan") Wanapanga matumizi...sio upimaji! Sasa ukipanga tu kwa eneo kubwa pasi na kuligawa ni hatari saana. Mfano useme hapa ni makazi kule kilimo....hapo unakua bado, tunachotaka ni kupanga na kupima....maeneo yagawiwe katika mfumo wa vipande vya ardhi vidogo vidogo vyenye alama za utambuzi na upimaji ("Neighbourhood plan") za kimkakati.....yaan ziwepo poote punde baada ya makazi endelezwa.
 
Back
Top Bottom