Upangaji wa matokeo na rushwa itaangamiza soka Zanzibar Kimataifa

King Leon 1

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
245
Reaction score
342
Katika hali ya kushangaza sana ,Club ya Uhamiaji FC ya Zanzibar inayoshiriki mashindano ya Shirikisho Africa imekubaliana na Al ahly Tripoli ya Libya kuwa mechi zao zote zitapigwa Libya kwa sababu ambazo hazina mashiko kuwa za kiusalama na makubaliano baina ya timu izo mbili.

Sasa kati ya Zanzibar na Libya wapi kuna usalama? Mseme ukweli tu mmepewa rushwa na kupanga matokeo . Ndio maana mpira wa Zanzibar haukui na wote wanashabikia timu za bara tu. Zanzibar ijitafakari na CAF iingilie kati huu upangaji matokeo wa wazi.

Soma Pia:TFF na ZFF zimejaa Rushwa, tuzidi kuziripoti moja kwa moja FIFA na CAF
Snapinsta.app_454623152_1568124174133018_5091130328943015467_n_1080.jpg
 
Katika hali ya.kushangaza sana ,Club ya Uhamiaji FC.ya Zanzibar inayoshiriki mashindano ya shirikisho Africa imekubaliana na Al ahly Tripoli ya Libya kuwa mechi zao zote zitapigwa Libya kwa sababu ambazo hazina mashiko kuwa za kiusalama na makubaliano baina ya timu izo mbili. Sasa kati ya Zanzibar na Libya wapi kuna usalama? Mseme ukweli tu mmepewa rushwa na kupanga matokeo . Ndio maana mpira wa Zanzibar haukui na wote wanashabikia timu za bara tu. Zanzibar ijitafakari na CAF iingilie kati huu upangaji matokeo wa wazi
Wazenji ni wabobezi wa rushwa na huwa hawajali kabisa kuuza utu wao kwa ajili ya fedha. Angalia uzwaaji wa bandari zetu, misitu, Loliondo umefanywa na viongozi wakuu Wazanzibari!
 
Katika hali ya kushangaza sana ,Club ya Uhamiaji FC ya Zanzibar inayoshiriki mashindano ya Shirikisho Africa imekubaliana na Al ahly Tripoli ya Libya kuwa mechi zao zote zitapigwa Libya kwa sababu ambazo hazina mashiko kuwa za kiusalama na makubaliano baina ya timu izo mbili.

Sasa kati ya Zanzibar na Libya wapi kuna usalama? Mseme ukweli tu mmepewa rushwa na kupanga matokeo . Ndio maana mpira wa Zanzibar haukui na wote wanashabikia timu za bara tu. Zanzibar ijitafakari na CAF iingilie kati huu upangaji matokeo wa wazi.

Soma Pia:TFF na ZFF zimejaa Rushwa, tuzidi kuziripoti moja kwa moja FIFA na CAF
Sio Uhamiaji tu hata JKU mechi zake zote mbili dhidi ya Pyramids kaamua kuchezea Misri.
 
Kwa taarifa za sasa ni uhamiaji tu ila Kama ni mkazi wa Zanzibar tuelezee kwanini team zenu zimekuwa na hii tabia ambayo inaua sana na kudidimiza maendeleo ya soka
 
Usiseme kwa taarifa za sasa, sema kwa taarifa unayojua wewe hadi sasa.
Mechi ipo chini ya CAF na timu mwenyeji hutoa taarifa wiki moja kabla kuhusu uwanja na muda wa mchezo. Tayari ratiba ya mechi ya JKU vs Pyramids ipo wazi kuwa inachezwa Cairo Misri japokuwa JKU ndiye mwenyeji.

Mimi sio mkazi wa Zanzibar bali nimekufahamisha kulingana na ratiba iliyopo ya mchezo husika, kuhusu sababu sijui kiundani ila nahisi hizo timu zimechikua pesa
IMG_20240814_125034.jpg
 
Usiseme kwa taarifa za sasa, sema kwa taarifa unayojua wewe.
Mechi ipo chini ya CAF na timu mwenyeji hutoa taarifa wiki moja kabla kuhusu uwanja na muda wa mchezo. Tayari ratiba ya mechi ya JKU vs Pyramids ipo wazi kuwa inachezwa Cairo Misri japokuwa JKU ndiye mwenyeji.

Mimi sio mkazi wa Zanzibar bali nimekufahamisha kulingana na ratiba iliyopo ya mchezo husika. View attachment 3069681
Asante kwa taarifa. Nimesema ivo kwasabb uwa naongea vitu nauhakika navyo na Uhamiaji FC ndio wamekiri na kuweka wazi kwa kutoa barua ila kuhusu klabu nyingine bado sijajua .
Ni suala la aibu na kukemea vikali sana
 
Hapo wa kuwajibika kwanza ni baraza la michezo Zanzibar, na shirikisho la soka Zanzibar, zipo sababu ya timu kwenda kuchezea mechi nje ya nchi yako na sababu huwa ni machafuko na miundombinu ambayo haina hadhi ( uwanja)
Kwenye hii swala kwa muono wangu kwanza kabisa Zanzibar walielekezea kwenye udini timu zote zinazocheza nazo ni za kiarabu hivyo wameweza kushawishika kutoka na udini japokuwa pesa ndicho kitu ambacho watakacho kipata maana lazima gharama za kula, kulala na usafiri watalipiwa tu na wenyeji wao na mwisho watapewa na chochote kitu.
 
Kwa taarifa za sasa ni uhamiaji tu ila Kama ni mkazi wa Zanzibar tuelezee kwanini team zenu zimekuwa na hii tabia ambayo inaua sana na kudidimiza maendeleo ya soka
Sio Uhamiaji tu hata JKU mechi zake zote mbili dhidi ya Pyramids kaamua kuchezea Misri.

Hali ya kifedha ya timu za zanzibar ni mbaya sana, ni tofauti sana bara, kule hakuna hela ya TV wala mdhamini wa ligi, nauli za kwenda huko nchi za nje pia ni tatizo. gate collection za viwanjani ni 2000/- na hiyo pia viwanja vinakuwa vitupu.

Kwahiyo wakicheza sehemu kama nchi za kiarabu wananufaika zaidi.
mechi yao ya home ikichezwa arabuni uwanja unapata mashabiki vizuri tu hivyo wanapata mgao mzuri wa gate collection. na pia usikute wapinzani wao pia huwagaia chochote mana mechi zote mbili wanapata kucheza kwao nao wana save gharama za kuwafata,
 
Hapo wa kuwajibika kwanza ni baraza la michezo Zanzibar, na shirikisho la soka Zanzibar, zipo sababu ya timu kwenda kuchezea mechi nje ya nchi yako na sababu huwa ni machafuko na miundombinu ambayo haina hadhi ( uwanja)
Kwenye hii swala kwa muono wangu kwanza kabisa Zanzibar walielekezea kwenye udini timu zote zinazocheza nazo ni za kiarabu hivyo wameweza kushawishika kutoka na udini japokuwa pesa ndicho kitu ambacho watakacho kipata maana lazima gharama za kula, kulala na usafiri watalipiwa tu na wenyeji wao na mwisho watapewa na chochote kitu.

Ficha ujinga wako.
 
Mzee hizi hoja zako Naona hazina mashiko, naomba tuweke kando udini Tafadhari
 
Hali ya kifedha ya timu za zanzibar ni mbaya sana, ni tofauti sana bara, kule hakuna hela ya TV wala mdhamini, nauli za kwenda huko nchi za nje pia ni tatizo. gate collectiion za viwanjani ni 2000/- na hiyo pia viwanja vinakuwa vitupu.

Kwahiyo wakicheza sehemu kama nchi za kiarabu wananufaika zaidi.
mechi yao ya home ikichezwa arabuni uwanja unapata mashabiki vizuri tu hivyo wanapata mgao mzuri wa gate collection. na pia usikute wapinzani wao pia huwagaia chochote mana mechi zote mbili wanapata kucheza kwao nao wana save gharama za kuwaf
Hali ya kifedha ya timu za zanzibar ni mbaya sana, ni tofauti sana bara, kule hakuna hela ya TV wala mdhamini, nauli za kwenda huko nchi za nje pia ni tatizo. gate collectiion za viwanjani ni 2000/- na hiyo pia viwanja vinakuwa vitupu.

Kwahiyo wakicheza sehemu kama nchi za kiarabu wananufaika zaidi.
mechi yao ya home ikichezwa arabuni uwanja unapata mashabiki vizuri tu hivyo wanapata mgao mzuri wa gate collection. na pia usikute wapinzani wao pia huwagaia chochote mana mechi zote mbili wanapata kucheza kwao nao wana save gharama za kuwafata,
Kama hali ni iyo mbaya kiuchumi, Basi inamaana viongozi hawalioni ilo kuwa litaua kabisa ata mapenzi kwa mashabiki wachache walionao na kupoteza matumaini kabisa maana baada ya kujitahidi kuzileta timu Zanzibar wawavute watu na kujenga upenzi wa wasiopenda mpira kuvutika kwenda kuona team za kigeni ila wao hawafanyi ivi,, Yaani ata km uchumi mbaya ila iyo sio njia sahihi ya kujipatia pesa
 
Back
Top Bottom