KERO Upasuaji kwa wajawazito imekuwa kama lazima, ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu kafanye research tena ....niko Hospital X ya serikali... Cesarean Section (C/S) tunazofanya kwa siku ni 30-40 na zote sio kua tumesema basi tuu tupasue zote zinafanyika kwa protocol...ninachotaka kusema hizi procedure wala sishabikii kabisa nazichukia sema ndio hivyo ni kazi
 
wengine wanapasuliwa kwasababu ya pesa tu, ukizalisha kwa kupasuliwa unapata pesa nyingi zaidi. wengine ni complication zenye justification. wengine wameingiliwa kinyume hadi wanaona noma kupush ndio wanaomba wenyewe wapasuliwe. kuna mengi sana, tusilaumu tu, vingine ni muhimu kupasua kuokoa maisha.
 
Nimekuelewa pote ila hapo mwisho kwenye alama ya mshono napinga siku hizi wanashona vizuri sana alama inakua kwa mbali sana nimeshuhudia mara kadhaa, japo mshono ni mshono ila hazina alama kama zile tulizokuwa tunazijua
 
Sababu kubwa ni nini inakua Dr?
Haya mambo sasa kwa asilimia kubwa utayakuta Private Hospital maana charges zina range mpaka 800K ..hiyo ni procedure fee bado gharama zingine za dawa n.k ..lakini pia kwa walengwa wenyewe bado wanataka sana hii C/S kama mdau hapo juu alivyosema... bila kujua madhara yake ya badae.
 
Wewe ulishawahi kubeba mimba na ukajifungua? Kama huijui mimba na huijui leba basi kaa kimya na uendelee kuwaombea wanawake wote wajifungue salama,

Halafu huo ujinga mnaolishana wa Marinda sijui nini inaonesha kabisa jinsi ugali na maharage ulivyoathiri Watanzania wengi hadi IQ zinakua ndogo.
 
Soma umuelewe vizuri.
Nimuelewe mtu ambaye sio daktari wala sio mwanamke, kapiga zake makande na uji anakuja kubeua humu halafu unataka nimuelewe nini labda,

Wiki ya jana tumepokea misiba minne ya watoto ambao mama zao walibisha kufanya upasuaji na kutaka kupush matokeo yake wamepoteza watoto, watoto wanne hao ni wa watu ninaowajua je kwengine vipi!? Huyu mmoja laiti angekua karibu yangu ningempiga makofi, mtoto ana kilo nne na nusu yeye anafosi kupush, madaktari wanamwambia apasuliwe anakataa matokeo yake kashindwa kupush mtoto kachelewa kutoka kafa na bado kachanwa chanwa kwa ujinga huo mnaolishana hapa eti ooh OP ni biashara, OP wanawake hawana marinda na ujinga ujinga mwingine
 
Pole.

Msiwe mnafanya kinyume na maumbile, kipindi cha ujauzito fuateni ushauri wa watalaam wa afya mtajifungua salama.
 
Nashukuru wale madaktari waliniokolea mwanangu atakam alivunja kioo na kutokea dirishani.
 
Mkuu hapo mwishoni uliyoyasema si kweli. Siku hizi operation sio kama zamani kovu lake ni mstari mdogo sana na limekaa mlalo sio wima kiasi kwamba haliharibu muonekano, upande wa kuwa na tumbo kubwa huo ni uzembe wa mama wala haihusiani na operation na pia mama anaweza kuzaa watoto mpaka 4 au 5 kwa operation za siku hizi
NB: Operation zinakera tu kwasababu zinamchukulia mama mida mwingi wa kurecover.
 
Hv kweli wewe ni mhudumu wa afya? Maana unatoa majibu kama matusi
 
Tunaitaji kutatua hii changamoto ya upasuaji isiwe kma utamaduni sasa haya matusi yako hayasaidii chochote, au wewe unafurah wenzio kupasuliwa kila leo kisa unaokoa vifo

Quote Reply
Report Edit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…