KERO Upasuaji kwa wajawazito imekuwa kama lazima, ni kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu nionyeshe na unitag picha ya mahali palipopasuliwa kupitisha mtoto kama hapaachi alama ya kupunguza mvuto wa muonekano wa mke! Kumbuka kunitag vinginevyo sitaona mbwangali
 
Hat

Siongelei vifo bali upasuaji usio wa lazma, nielewe tafadhali
Unajuaje wewe kuwa sio wa lazima?
Mbona ni kazi rahisi tu, kabla hajapasuliwa ndugu wa karibu anaarifiwa ili aweze kujaza fomu ya ridhaa,

Wewe kama unaona ni kitu ambacho sio cha lazima, haulazimishi jaza fomu ya kukataa kufanyiwa upasuaji usio wa lazima ili kwamba lolote litakalompata mgonjwa wako na mtoto wao hawatahusik.
 
Mmh.....
Mimi nilishuhudia,nurse midwife akimzuia dokta uchwara kuwa "Huyu si wa operation naweza msaidia akajifungua salama"
Dr uchwara akasusa"Akifa mama/mtoto utawajibika"
Yule nurse alipambana mama&mtoto wakatoka salama.
Jiulize ni wangapi wanapigwa visu isivyostahili?
Mbona previously wengi walijifungua salama tu bila operation?
Si kila mzazi ni wa operation!
Tuna madaktari wa hovyo sana siku hizi.
Tena wasio na uzoefu,na wamepewa dhamana kubwa.
Ambao kutibu mgonjwa tu mpaka wa google.
Hili nalo hulijui?
 
Mkuu, karibu sana hospital Tena kitengo cha akina mama ndo utaelewa maana yake
Kuongezeka kwa idadi ya kujifungua kwa kisu ni mambo mengi yanachangia
1. Nimeona wamama wao wenyewe wakitaka kujifungua kwa kisu, ni vle hawataki complications za kusukuma, kutanua uke,...
2. Msukumo (presha) kubwa ambayo serikali inaweka kwenye huduma ya akina mama
Hii nchi ni Bora mgonjwa wa sukari afariki(hata kama imetokana na uzembe) kuliko mama/mtoto afariki wakati wa kujifungua. Kwahyo watu wa afya wanaona ni Bora kufanya operation kuliko kuhatarisha maisha ha mama/mtoto
3. Medical reasons Kwa ajili ya cesarian section kama mtoto kuwa mkubwa, presha/kifafa cha mimba, kisukari cha mimba,
4. Wamama wengi wanabeba mimba katika umri mkubwa ambayo ni risk ya kupata Post partum hemorrhage, Moja Kati ya sababu kubwa ya vifo vya akina mama, kwahyo kuepusha hayo, ni Bora kuzaa kwa kisu
5. Grand multiparity. Unakuta mama amezaa mara 8, misuli ya mji wa mimba imeshachoka. Kwahyo kusukuma inakua ni ngumu
6. Previous scar. Upasuaji wowote katika mji wa mimba mfano, kujifungua kwa operation, kuondolewa uvimbe...unaacha kovu(scar) kwnwye uterus(mji wa mimba) hivyo ni hatari sana mama kuja kujifungua kawaida maana mfuko utakua kwenye hatari ya kupasuka (uterine rupture. Na hvyo njia inayobaki ni kujifungua kwa kisu Tena na Tena
 
Una makasiriko sana utakua single mother wewe .una uchungu wa Op na kukimbiwa
 
Ni kero sanaaa,why this miaka hii? Na usipokuwa na msimamo mkeo akifika tu hospital ni upazuaji tu hata hawafuati hatua za kumzalisha kawaida, why?
 
Una makasiriko sana utakua single mother wewe .una uchungu wa Op na kukimbiwa
Labda mama ako ndie singo mama, mimi ni mke na ni mama mwenye watoto kadhaa, wewe ambae hujawahi hata kutungisha mwanamke mimba ndie mwenye makasiriko, ukisoma michango ya wanaokandia op ni hawana hata watoto wa kusingiziwa wazee wa kupanda mnazi kwa mkono
 

Marco Polo jibu lako hilo

under timer kama na hapo hujaelewa basi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…