Upasuaji wa Kujifungua: Kuokoa maisha au hofu ya uchungu?

Upasuaji wa Kujifungua: Kuokoa maisha au hofu ya uchungu?

UTPC

Journalists' Union
Joined
Apr 17, 2026
Posts
51
Reaction score
38
Kilio cha mama kinapochanganyika na sauti ya kwanza ya mtoto, mara nyingi huleta faraja na furaha isiyoelezeka. Lakini nyuma ya pazia hilo la matumaini, kuna nyakati ambazo maisha ya mama na mtoto huning’inia kwenye uamuzi mgumu wa kitabibu; uamuzi wa kufanya upasuaji wa kujifungua ili kuyaokoa.

Katika mkoa wa Njombe, simulizi hizi si nadra tena; zimekuwa sehemu ya mjadala mpana unaogusa hisia, imani na uelewa wa jamii kuhusu uzazi salama kama anavyosimulia Mwandishi wetu, Elizabeth John.

Wakati wengi wakiamini kuwa kujifungua ni mchakato wa kawaida kwa kila mwanamke, wataalamu wa afya wanaeleza kuwa hali hiyo inaweza kubadilika ghafla kutokana na sababu za kimwili zinazohitaji uingiliaji wa haraka wa kitabibu, ikiwemo upasuaji.

Kwa mujibu wa wataalamu, zipo sababu mahususi zinazosababisha madaktari kushauri upasuaji badala ya kujifungua kwa njia ya kawaida, hasa pale maisha ya mama au mtoto yanapokuwa hatarini.

Hata hivyo, hoja hii imeibua mjadala mkubwa mkoani Njombe, mkoa unaotajwa kuongoza kitaifa kwa idadi ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji. Baadhi ya sauti za jamii zimekuwa zikielekeza lawama kwa hospitali binafsi, zikidai kuna msukumo wa kifedha unaochochea ongezeko hilo.

Andiko la pendekezo la utafiti uliolenga kujua ukubwa (kiasi na uzito) wa Upasuaji wa Kujifungu (Caesarean Section – CS) katika Mkoa wa Njombe, hasa Hospitali ya Kilutheri Ilembula linabainisha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji linaonekana kuwa jambo la kawaida, hata zaidi ya kiwango kinachopendekezwa.

Upasuaji wa kujifungua ni njia muhimu ya kuokoa maisha ya mama na mtoto pale kunapokuwa na hatari kama vile uchungu wa kujifungua kushindwa kuendelea, mtoto kuwa katika nafasi isiyo sahihi, au matatizo mengine ya kiafya,”anabainisha Mlwalwe.

Hata hivyo, upande mwingine wa matokeo ya uchambuzi wake yanaibua changamoto ya kile kinachotajwa katika taarifa nyingi za tafiti kuhusu uwepo wa matumizi ya kupita kiasi ya upasuaji, mwngine ukitajwa kufanyika “bila sababu za msingi za kitabibu.”

Daktari Bingwa
Dk. Mhina Edward ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe, anasema hali ya dharura inaweza kumfanya mjamzito kufanyiwa upasuaji.

Dk. Mhina ambaye pia ni Mratibu wa tafiti na Mafunzo katika hospitali hiyo anasema katika huduma za uzazi, upasuaji unaofahamika ni Cesarean section (C-section) ambao hufanywa pale maisha ya mama au mtoto yanapokuwa hatarini na/au kujifungua kwa njia ya kawaida kunakuwa kugumu au hatari.

Katika andiko lake, Mwanafunzi Benedict Mlwale wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi, anabainisha kuwa tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuongezeka kwa kina mama wanaojinfugua kwa upasuaji; Barani Afrika (kutoka asilimia 0.6 hadi 18) na nchini Tanzania (asilimia 21.4 hadi hadi 31.8) katika maeneo mengine.

Kuhusu hali ilivyo mkoa wa Njombe hususan Hospitali ya Ilembula, andiko la Benedict linabainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko la idadi ya kesi za CS katika hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kilutheri. Pamoja na kwamba idadi kamili haijatajwa, lakini mtafiti anasema: “kumekuwa na matukio makubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.”

Hoja za Benedict katika andiko lake zinaungana na tafiti mbalimbali ukiwemo wa ule wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria (TDHS) 2022 wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), unaoonyesha kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa asilimia kati ya 29 - 32 ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji, ukifuatiwa na Dar es Salaam kwa asilimia 26 na Iringa kwa asilimia 24.

Kadhalika Ripoti ya Uchambuzi wa Viashiria vya Afya ya Uzazi, mama, mtoto na vijana (Analysis of Reproductive, Maternal, Newborn, Child and Adolescent Health Indicators) ya mwaka 2019-2024 inabainisha kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa kiwango cha juu ha C-section ukifikia asilimia 28.4 mwaka 2024 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2019.

Maelezo ya kitaalamu
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi, Dk. Mhina anataja baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha dharura ya upasuaji kuwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi wakati wa ujauzito au uchungu.

“Hali hii inaweza kusababishwa na kile ambacho kitaalam kinaitwa ‘placenta previa’, ambapo kondo la nyuma linakuwa limefunika mlango wa kizazi au placental abruption ambapo kondo la nyuma linajitenga mapema na ukuta wa mfuko wa uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa,” anasema Dk. Mhina na kwamba hatua za haraka zisipochukuliwa maisha ya mama na mtoto yanaweza kuwa hatarini.

Anaitaja sababu nyingine kuwa ni mtoto kupata shida akiwa tumboni, hali inayojulikana kitaalamu kama fetal distress. “Hapa madaktari hugundua mabadiliko yasiyo ya kawaida katika mapigo ya moyo wa mtoto, yanayoashiria kuwa mtoto anaweza kuwa hapati oksijeni ya kutosha,” anasema Daktari bingwa huyo kuongeza: “Katika hali kama hii, upasuaji unaweza kuwa suluhisho la haraka la kuokoa maisha ya mtoto.”

Dk. Mhina anataja dharura nyingine kubwa kuwa ni kupasuka kwa mfuko wa uzazi (uterine rupture), hali mbayo hutokea zaidi kwa mama ambaye aliwahi kufanyiwa upasuaji wa kujifungua hapo awali na kovu la upasuaji likapasuka wakati wa uchungu. Anasisiza: “Tukio hili linahitaji matibabu ya haraka ili kuzuia madhara makubwa kwa mama na mtoto.”.

Anaendelea kueleza kuwa kuna hali ya uchungu kushindikana kuendelea inayojulikana kama obstructed labour. “Hapa mtoto hushindwa kupita kwenye njia ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali kama ukubwa wa mtoto au maumbile ya nyonga ya mama na inapogundulika mara nyingi madaktari hulazimika kufanya upasuaji ili kuepusha madhara zaidi,” anasisitiza.

Kadhalika daktari huyo ansema shinikizo la damu kali wakati wa ujauzito pia linaweza kusababisha upasuaji wa dharura. “Hali kama pre-eclampsia kali au eclampsia njia sahihi ni kujifungua kawaida tunalazimika kufanya upasuaji kama kutakuwa na viashiria vya hatari vya kumpoteza mtoto na kwa abruptio hufanyika pale kondo linapojiachia mapema na mtoto yuko hai”.

Vilevile anasema nafasi isiyo ya kawaida ya mtoto tumboni inaweza kufanya kujifungua kwa njia ya kawaida kushindikana. Mfano mtoto anakuwa amegeuka na matako au miguu ndiyo inayotangulia, amelala kwa upana tumboni na katika mazingira haya mara nyingi upasuaji huwa njia salama zaidi ya kujifungua.

Sauti za jamii
Sophia Issa, mkazi wa mjini Njombe, anasema ni kweli kuna mwenendo wa ‘kushadadia’ kujifungua kwa njia ya upasuaji miongoni mwa kinamama wajawazito, na kwamba alilishuhudia kwa rafiki yake ambaye hakutaka kusubiri uchungu, badala yake alitaka kufanyiwa upasuaji.

“Yeye alisema hayataki maumivu ya uchungu, mimi nadhani elimu ingetolewa kwa jamii na wanawake pindi wanapokuwa wajawazito. Wapo wale watu ambao ni lazima wajifungue kwa upasuaji, lakini kama haikulazimu, kwanini ukalazimishe,” anasema Sophia.

Kwa upande wake, Rabison Mahenge ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, anathibitisha kwamba kuna ongezeko kubwa la wanawake kujifungua kwa njia ya upasuaji katika mkoa wa Njombe.

“Kikawaida tumevuka lile lengo la muongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Sisi kama madiwani kwa jumla tunajua sababu zinazosababisha upasuaji ni nyingi lakini tunachojipanga nacho ni kuzuia,” anasema Mahenge.

Mahenge pia anaeleza kuwa halmashauri, kwa kushirikiana na wataalamu wa afya, itatoa elimu kwa jamii kwamba upasuaji unapaswa kufanywa pale tu ambapo kuna changamoto kiafya, na si kwa sababu za kuomba au hofu ya uchungu. Alibainisha kuwa ushiriki wa wanaume katika kliniki za uzazi umepungua, jambo linalohitaji uhamasishaji zaidi.

ANDIKO LA: Elizabeth John , NJOMBE
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.
 
Mwanamke anapitia mengi sana kuanzia mimba inaingia mpaka kufikia miezi tisa, ila watu hamridhiki mnafuatilia kuhakikisha amepitia mchakato wote wa kuteseka...hata hao wanaojifungua kwa kisu sio kwamba wanapata watoto kirahisi tu bila uchungu
 
Wanadhani kuzaa ni kama kutema mate. Mfyuuuuu hiyo mimba ya miezi nane tu mateso yake, bora kuingia labor
 
Mwanamke anapitia mengi sana kuanzia mimba inaingia mpaka kufikia miezi tisa, ila watu hamridhiki mnafuatilia kuhakikisha amepitia mchakato wote wa kuteseka...hata hao wanaojifungua kwa kisu sio kwamba wanapata watoto kirahisi tu bila uchungu

M ningekuwa daktar ningerecomment Opereshen kwa kila mwanamke ambae ni uzaz wake wa kwanza na yuko above 30+ years.

Inasaidia Mwanamke kutopata kifafa cha mimba , vifo na madhara mengne ambayo Mwanamke anakumbana nayo hasa akiwa na umri mkubwa.

Bora awe na kitambi huko mbeleni ila maisha yake na mtoto yameokolewa.

Sometimes sio kwamba hosp wanahitaj hela. Ila wanaona risk iliyoko mbele na wanakushaur nn cha kufanya.
 
Ni kweli kabisa. Lakini najiuliza umejuaje na wewe sio dakitari
 
🤔mengi yapo nyuma ya pazia wachunguze vizuri
 
Ni kweli kabisa. Lakini najiuliza umejuaje na wewe sio dakitari
Life is a mother Teacher.

Inatia huruma ukisikia habar kuwa Mwanamke amefariki wakat wa kujifungua. Au amepata kifafa cha mimba.

Au amefariki yeye pamoja na mtoto.
Imagin simanzi watakayokuwa nayo familia yake.

asilimia kubwa sana ya wanaopata changamoto za uzaz ni wale wanaozaa kwa mara ya kwanza wakiwa above 30's.

Ila mwanamke wa miaka 18 anashusha mzigo asubuh na jion anaruhusiwa kurud na mtoto nyumban.
Viungo vyake vya uzazi vinampa favour.
 
Mkuu,sio wote. Kuna watu wanazaa na umri mdogo na wanapata matatizo na kuna watu wanazaa na umri mkubwa hawapati shida. Uzazi ni very complex na factors zinazoaffect uzazi zipo nyingi, umri sio factor pekee. Ingekuwa umri ni factor basi nchi masikini kama Tanzania ambapo watu wanazaa wakiwa wadogo kungekuwa hakuna vifo au matatizo ya uzazi kulinganisha na nchi tajiri ambako watu wanazaa hadi na 40s mtoto wa kwanza. Cha kushangaza nchi masikini kama huku ambako watu wanazaa na umri mdogo ndo tunaongoza kwa matatizo na vifo vinavyotokana na uzazi.
 
Bongo utasikia mama mkwe ndo anatoa ruhusa kama mke wa mwanae azae kwa operesheni au kawaida,na anajibu kwa kiburi kabisa" watoto wetu hawazaliwi kwa kisu, asukume". Tuna ujinga mwingi sana yaani kuna mambo ukisikia unatamani madaktari kuchapa watu viboko ila ndo hivyo tu. Mama mkwe anapata wapi mamlaka ya kuamua mkwe wake ajifungue kwa njia gani? Yeye kama nani? Inatia hasira sana.
 
Mkuu,sio wote. Kuna watu wanazaa na umri mdogo na wanapata matatizo na kuna watu wanazaa na umri mkubwa hawapati shida. Uzazi ni very complex na factors zinazoaffect uzazi zipo nyingi, umri sio factor pekee. Ingekuwa umri ni factor basi nchi masikini kama Tanzania ambapo watu wanazaa wakiwa wadogo kungekuwa hakuna vifo au matatizo ya uzazi kulinganisha na nchi tajiri ambako watu wanazaa hadi na 40s mtoto wa kwanza. Cha kushangaza nchi masikini kama huku ambako watu wanazaa na umri mdogo ndo tunaongoza kwa matatizo na vifo vinavyotokana na uzazi.
Nilizaa na 26yrs, 32yrs,38yrs kawaida kaabisa. Zingatia ulaji wa ba,ia ukiwa mjamzito. Siku ya kujifungua ule television utakusaidia na hutokaa uchanike. Ukizaa pumzika walai miaka 5-6, uke unarud mwake
 
Back
Top Bottom